Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 59
Ndugu zangu Watanzania wenzangu, katika vitu vinavyo niumiza akili yangu ni hili la Omba omba wa wanawake kutumia watoto wao wachanga kupata huruma kwa wapita njia barabarani.
Hii hali imekuwa ikindelea kuongezeka kila siku hapa jijini na Serikali yetu imelinyamazia kimya hili swala, Mtoto mchanga kabebwa mgongoni na mama yake anatembezwa barabarani mchana kutwa jua lake mvua yake, haki ya huyu motto ni nini hasa? Ustawi wa jamiii kazi yake nini katika Nchi yetu hii. Hawa watoto nani atawasaidia ili waweze kupata haki zao za msingi kama watoto?
Watunga sheria kwanini wasitunge sheria inayowahusu hawa watoto wanaotumiwa kama mradi na wazazi wao, Ukisimama barabarani anakuja mama na mototo wake mgongoni anaomba msaada, hana kilema cha aina yeyote, ukimuuliza baba wa mototo yupo wapi utasikia amekufa, au alinipa mimba akanitelekeza kumbe uongo mtupu baba zao wapo na wanaishi pamoja. Kuna Yule mama mwingine kule ocean road anayeshinda na kulala pale ufukweni alianza na mototo mmoja na sasa wamefika wane(4) hivi hii ni bahati mbaya kweli, kuna kituo cha redio kimoja waliwahi kumchangishia hela ya mtaji ili arudi kwao Kigoma akafanye biashara ndogondogo imfae na wanae hakwenda kokote mpk leo yupo, aliwahi kushauriwa awapeleke watoto ustawi wa jamii wapate kulelewa na wasome amegoma akijua wale ndio mtaji wake wa kujiingizia pesa.
Hii ni haki kweli, wale watoto wakikuwa watafanya nini au na wao ndio wawe ombaomba au ndio vibaka wajao?
Mimi nadhani Sheria ingechukua mkondo wake kwa kuwafikiria hawa watoto na future yao wakikuwa.
Njia rahisi ni kila mama anayeingia barabarani na mototo mgongoni kuombaomba Serikali/Ustawi wa jamiii wampokonye mototo na akalelewe kwenye vituo maalulu vya kulelea watoto.
Hii itasaidia kama mtu anataka kuwa omba omba aache motto nyumbani atangetange peke yake .. hii haingii akilini mtu mungu kakuumba na viungo vyako kamili kwa nini ukae barabarani na motto kuomba. Kwa nini usitafute biashara ndogo ndogo ufanye uweze kulea motto.
Huu ni uzembe na serikali yetu kwa ujumla inachangia hili kwa kuwafumbia macho hawa wazazi.
Sijui wenzangu mnalionaje hili swala kwa upande wenu.
Nawakilisha.