Omba omba katikati ya jiji

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Nimekuwa nikiguswa kama sio kukereka na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya ombaomba katikati ya jiji la Dar es salaam. Jumamosi hii nimetoka CRDB pale PPF Tower nikapokelewa na kundi la watoto wenye umri kati ya miaka minne mpaka 14 wakiomba hela ya chakula, kama walivyofanya kwa kila aliyepita maeneo ya karibu ya jengo hilo. Nilijaribu kuwahoji watoto kadhaa kwa nyakati tofauti kabla ya kuwaachia kianzio na walikuja na stori zinzofanana. Wote walidai kutokea Kigamboni, wanaishi na mama zao tu (aidha hawafahamu baba zao, au baba zao hawaishi Dar, walikufa etc. Watoto hao walidai kutumwa na mama zao kuomba kwa kuwa mama zao hawakuwa na ajira wala uwezo. Vilevile walikiri kukwepa masomo mara kadhaa kwa ajili ya kuombaomba na walidai kupata wastani wa Tsh 3,000/= kwa siku.

Baada ya kuachana na kundi hilo nikapita barabara ya Garden kuelekea NMB House. Mlangoni tu kabla ya kuingia nilikutana na dada mmoja mwenye kitoto cha miezi kumi mgongoni. Akanisalimia vizuri kisha "Kaka samahani, naomba unisaidie hela ya kula na mwanangu". Nikamuhoji inakuwaje dada mrembo kama yeye mwenye nguvu anaombaomba? Akasema alikuwa akiishi na bwana, alipobemba mimba bwana huyo akamkimbia. Alidai alikuwa akifanya kazi baa lakini alishindwa kuendelea kutokana na kuwa na mtoto. Akaogeza kuwa japo wenzake wanamcheka hawezi kujiuza, nami nikamwambia hilo ndo la mbolea. Wakati naendelea kumhoji nikaona kama machozi yanalenga lenga hivi, nikaamua kuziua na kumpa buku kama kianzio.

Nilibaki najiuliza kama kweli hawa ombaomba ni genuine au wametafuta njia rahisi ya kujiongezea kipato ukizingatia ugumu wa maisha ya Bongo. Mimi nilizoea wale walemavu wa viungo wanaokaa maeneo ya posta wakipewa mia mia na si hawa waliokamilika kila idara wanaodai hawana kazi wala kipato. Kuna haja ya serikali kuangalia suala hili kwa karibu kabla mambo hayajawa mabaya maana impression niliyoipata ni kwamba kwa asiyekuwa na kipato akawe ombaomba! Mwisho wa siku si tutakuwa na taifa la ombaomba wazoefu kama kina Matona? Nawasilisha
 
Back
Top Bottom