Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Ndugu wanJF,
Jana katika kipindi cha tuongee asubuhi cha startv, kulikuwa na mjadala kuhusu baraza la mawaziri lililoundwa na Rais JK hivi karibuni.
Kulikuwa na wachangiaji watatu studio ya mwanza akiwemo Singo Kigaila wa cdm, Kerebe Lutele kada wa ccm na mwingine wa tatu.Studio ya Dsm walikuwepo mwanaharakati Bw. Marcus Albano na mwanaJF Omarilyas.
Kwa ujumla watu wote walikubaliana kwamba baraza la mawaziri la JK ni kubwa sana na uendeshaji wake utachukua karibia takribani 80% ya bajeti, wakati bajeti ya maendeleo inakuwa ni takribani 20%. Bw. Omarilyas na mwenzake Kerebe pamoja na kukubaliana na hoja ya ukubwa wa baraza wao wakasema inatokana na mahitaji ya wakati huu kitu ambacho walishindwa kukithibitisha.
Jambo moja ambalo binafsi lilinishangaza ni pale bwana Omarilyas alipodai kwamba baraza la mawaziri linaweza kuwa kubwa lakini matumizi yakawa madogo, akitolea mfano kwamba kunaweza kuwa na baraza la mawaziri lenye watu 100 wakawa na matumizi madogo sawa na baraza la watu 50.
Swali ambalo nilikuwa najiuliza na ambalo ningependa wanajamvi wenzangu tushirikishane kufahamishana ni hili; kwamba inawezekanaje kuwa na baraza kubwa la mawaziri lakini tukatumia fedha kidogo kwa shughuli za uendeshaji katika nchi kama yetu ambayo tumeelezwa kwamba magari waliyokabidhiwa juzi mawaziri baada ya kuapishwa yameigharimu serikali kiasi cha Tsh. 9.3 bilioni. Je ni kweli kwamba chini ya serikali ya JK na ccm tunaweza kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha? Je chini ya serikali ya JK na ccm wanaweza kuelekeza fedha nyingi za bajeti katika maendeleo kwamfano 50% ikaenda kwenye miradi ya maendeleo?
Wadau naomba mawazo yenu.