Olimpiki ya msimu baridi yaanza Sochi

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Mashindano yaliyo gharimu Kitita kikubwa zaidi katika historia ya Olimpiki yatafunguliwa Urusi leo huku medali 98 ziking'ang'aniwa katika siku kumi na sita.
Sochi, ambayo iko katika pwani ya Urusi itakuwa ukumbi wa takriban wanariadha 2,900 kutoka kote duniani wakishindana katika fani kumi na tano.
Maandalizi ya mashindano hayo yamekabiliwa na tishio uslama, wasiwasi kuhusu haki za binadamu mbali kucheleweshwa maandalizi.
Lakini kwa gharama ya kwa kima cha dola bilioni 30 za Marekani ,Sochi ndiyo michezo ghali zaidi kuwahi kuandaliwa katika historia ya mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi ikijumlishwa.
Canada, Norway Marekani ndizo nchi zinazopigia upatu kuongoza katika jedwali la Medali huko Sochi bila ya kuwasahau wenyeji wa mashindano hayo Urusi.
Uingereza inapania kushinda medali zisizopungua tatu za dhahabu.
Iwapo itafaulu basi itakuwa timu ya kwanza ya nchi hiyo kuandikisha matokeo bora katika mashindano hayo ya msimu wa baridi tangu mwaka 1936 .

chanzo:
Olimpiki ya msimu baridi yaanza Sochi - BBC Swahili - Michezo

Afrika tumewakilishwa na nchi tatu tu,
1.Morocco
2.Togo na
3.Zimbabwe

kwa mnaotaka kuangalia ufunguzi Live Basi unaweza kuangalia kwa kupitia link hii hapa
http://u-stream.me/bbc-2.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…