Ikiwezekana basi tpendekeze,
Kanzu au Joho la shemazi,
liwe vazi la kukimbilia!
A Lubega ya Masai?
Hata Masai mara nyingi pale Dar,
nimeona watu wakikwazika na mavazi yao.
Mavazi ambayo ni asili yao.
Watu hukwazika na Uchezaji wa Sindimba,
ile ngoma ya kimakondo,
Wamakonde hawakuiiga ngoma ile toka Ulaya.
Kuna ngoma ya Kiha nimesahau jina,
mwanamke hukaa chini,
kisha kukata kiuno kwa sana,
viongozi kadhaa wamedai ngoma hii,
ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania,
Mtanzania yupi?
Watu wanatembea wamevaa nguo zote,
na kuacha makabati tupu,
wasikileze maneno yao mdomoni,
mara 100 wangekaa uchu wangesetirika.
Ni kivazi tu,
Taabu yote iko akilini mwetu.