Olengurumwa, nani kakwambia Rais Samia Suluhu atagombea Urais mwaka 2025?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,788
218,420
Olengurumwa amesikika akiwaambia vyama vya upinzani wasigombee Urais wa Tanzania, na kwamba ushauri wake huo unataka kinyang'anyiro hicho aachiwe Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa akili ya Olengurumwa ndiye mgombea wa CCM wa 2025.

Hatuna shida yoyote na Mwanaccm Olengurumwa kumpigia kampeni Mwenyekiti wa chama chake cha ccm Samia Suluhu Hassan, maana ni wajibu wa kila mwanachama kuhakikisha anampigia kampeni Mwanachama mwenzake, ili ashinde na kutwaa madaraka.

Bali anachopaswa kukumbuka ndugu Olengurumwa ni hiki, Samia Suluhu hakuwahi kuchaguliwa na yeyote ili awe Rais wa Tanzania, ni Rais wa kikatiba tu, kingine ni kwamba Mgombea yeyote wa Urais wa Tanzania ni lazima aombe Urais huo kupitia kwenye chama chake, na baadaye apitie mchujo wa Kamati Kuu na Mkutano Mkuu umpitishe kuwa Mgombea.

Ni kweli kwamba Samia Suluhu ameachana na siasa za kikatili za mtanguliI wake, na ni kweli kwamba nchi ina amani, na ni kweli kwamba kuna maridhiano mezani , lakini vitu hivi havimfanyi yeye kuwa mgombea pekee wa Urais 2025, lakini kingine ni hiki, je, Samia Suluhu ana nia ya kugombea Urais 2025? Mtu ambaye hatogombea awezaje kuwa mgombea pekee?

Kimsingi Olengurumwa amekurupuka ili kupata chochote, bali sisi watu wa Demokrasia tunamuonya aache uchawa, vinginevyo tutaingia vitani naye na hatoweza.

Kama unampenda mtu kwa sababu ya sura yake basi nenda kanywe naye chai - JK Nyerere
 
Tena namuonya huyo Onesmo anayejifanya mpigania haki za binadamu kupitia genge lake la kupigia misaada kutoka kwa mabeberu mpumbavu kabisa.

Kule Ngorongoro alienda kugombea ubunge kisirisiri wajumbe wakamkaanga leo analeta ushenz wake kwa watu wenye akili; huo upumbavu wake apeleke kwa uvccm na sukuma gang ambao kwao hata mwendawazimu anaweza kuwaongoza kama walivyoongozwa na kichaa aliyekuwa na file mirembe kama tulivyoambiwa na DIALLO.

Kifupi Olengurumwa aende akaungane na wenzake wa UVCCM Lumumba.
 
Mh. Rais wetu kwa mahaba, upendo wa dhati, utu, ubinadamu, faraja na uongozi thabiti aliotuonyesha, atake asitake lazima agombee, akikataa tunaandamana kumlazimisha, akiacha kuchukua fomu tunaenda kuchukua, akiletewa fomu asipojaza tunamjazia, asipo sign tunaiga saini yake tunasaini, asiporudisha fomu tunamrudishia, akiona jina lake limepita na kupiga kampeni labda ni kazi, sisi tutapiga kampeni kufa kupona nchi nzima.

Vyama vyote, maskini kwa matajiri, watanzania wote, huku tukimuomba Mungu amlinde Mama huyu aliyeletwa na Mwenyezi Mungu, awe na afya tele na matumaini yetu, roho zetu, mioyo yetu, upendo tunamkabidhi kwani imani na upendo mkubwa sana katuonyesha, na sisi tunampa mahaba yote..

Mungu mbariki Mama Samia Suluhu Hassan, amen, amen 🙏🙏🙏
 
Mungu amlinde Mama huyu aliyeketwa na Mwenyezi Mungu, awe na afya tele na matumaini yetu, roho zetu, mioyo yetu, upendo tunamkabidhi kwani imani na upendo mkubwa sana katuonyesha, na sisi tunampa mahaba yote..

Mungu mbariki Mama Samia Suluhu Hassan, amen, amen
yaleyale ya mwarabu wa nkasi ALLY KESSY aliyegongwa na mwanamke had leo hajulikan hata yuko wapi.
 
Dah

Uko bitter sana

Mola ayafanyie mateso yako wepesi …. For 20 years now unateseka
JamiiForums195514995_540x540.jpg
 
Back
Top Bottom