Olemedeye ashindwa kufanya kampeni arumeru

FRANK MICHAEL

Senior Member
May 17, 2011
151
46
Naibu waziri wa Aridhi na mbunge wa Arumeru magharibi mh Godluck Olemedeye ashindwa kumnadi mgombea wa chama cha kwenye kampeni zinazoendelea jimboni kwake.

Hii inatokana na watoto kumzomea na kumwagia vumbi kwenye moja ya mikutano yake, taarifa za ndani ya CCM zinasema mh huyo ameamua kutoshiriki kwenye majukwaa ya hadhara ikiwa ni kwa nia ya kulinda heshima yake.
 
aisee kule arumeru ccm wasikanyage kabisa hata EL mwenyewe alishindwa kumnadi mgombea wake wa ubunge wakati ule wa uchaguzi..yaani arumeru yote ile ni full cdm...wasithubutu na huyu naibu waziri ajue mwaka 2015 asithubutu kugombea tena maana arumeru magharibi ile itaangukia cdm
 
Kama ni kitunza heshima yake ni bora angejiondoa kwenye chama na serikali angeeleweka.
 
Lol. At least watoto wawaumbue.manake.wakubwa hatujawashughulikia vya kutosha. Mafisadi ooooo!
 
Huyo ni mzigo kwa jamii na hatakiwi hata kidogo na wanainchi kwa kweli wanamchukia haswa!

Tangu achaguliwe hajawahi kuwasalimu wanainchi na hapo akaaribu hali ya hewa kwa wanainchi flu!
Mi nimeshawahi kuwasikiwa wanainchi wa kata moja ya Mussa wakilalama sana na wakaahidi kamwe mafisadi hawakanyaga hapo kamwe na wapate kura!

Kwa ujumla kazi ipo kwa huyu naibu!
 
Nakumbukaga zile za watoto kulia kila wakiona ngua za ccm kule Arumeru Mashariki
 
"Moyoni utaikubali tu"

Ile Range Rover was made for West Meru. Medeye Usirudi, hata Ng'ombe Watazomea
 
Anajua alishindwa hata huo ubunge aliopewa! Anajua wananchi hawakumchagua! Anajua wananchi wanahasira kwa kuwachakachulia kura zao, akishirikiana na el. Anajua hawezi kuhudhuria mkutano wa hadhara jimboni humo.
 
Rubbish! Mimi nimehudhuria karibu mikutano yote ya kampeni an waziri Olemedeye alikuwa akishangiliwa sana kwenye hotuba zake. Nimepita kwenye mikutano ya Chadema, mikutano karibu yote in watoto ndio wanaohutubiwa. Tena wanaambiiwa mkiwaona wanachama wa CCM wakipita muwazomeeni! Na kweli ukipita msafara wa magari ya CCM makundi ya watoto na vijana hujitokeza nakuwazomea. Hapa mimi najiuliza ni kitu gani tunachowafundisha watoto wetu, leo wanawazomea watu wazima, kesho is watawazomea hata baba zao? Acha kujidangaja, mgombea udiwani wa CCM Olais Mfere anakubalika na wengi. Wiki moja imebaki sasa, ni wakati wa kuweka mikakati mizuri ili Chadema iweze kushinda.
 
Hueleweki mara CDM mara CCM

KUna baadhi ya majimbo mwaka 2015 CDM itapita bila kupingwa. Hii nawahahakikishia.
 
Tarehe 18 alikuwa mirongo ktk ziara yake ya jimbo,lakini kashindwa kujibu kero na ahadi alizotoa haswa umeme,alikuwa na jasba wananchi walitawanyika wakamuacha kwa aibu kubwa.
 
Kwa kuwa watoto hawapigi kura kidogo inatia mashaka lakini wananchi tupeni raha kwa kutupa diwani ili iwe salamu kwa Olemedeye 2015.
 
Rubbish! Mimi nimehudhuria karibu mikutano yote ya kampeni an waziri Olemedeye alikuwa akishangiliwa sana kwenye hotuba zake. Nimepita kwenye mikutano ya Chadema, mikutano karibu yote in watoto ndio wanaohutubiwa. Tena wanaambiiwa mkiwaona wanachama wa CCM wakipita muwazomeeni! Na kweli ukipita msafara wa magari ya CCM makundi ya watoto na vijana hujitokeza nakuwazomea. Hapa mimi najiuliza ni kitu gani tunachowafundisha watoto wetu, leo wanawazomea watu wazima, kesho is watawazomea hata baba zao? Acha kujidangaja, mgombea udiwani wa CCM Olais Mfere anakubalika na wengi. Wiki moja imebaki sasa, ni wakati wa kuweka mikakati mizuri ili Chadema iweze kushinda.

SIO Arumeru tu, hata hapa Dar es Salaam watoto wanaimba nyimbo za kashifa dhidi ya viongozi wa CCM waliopo na waliopita, mfano watoto wa shule moja iliyopo mjini kati Dar wanaimba wimbo wa taifa hivi,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu Usimbariki Mkapa,
Ameiba fedha,
ameficha kwenye Kwapa..."

Hali ni mbaya, the old generation is passing away with its CCM-ism and Nyerereism.
Ugumu wa maisha ndani ya familia unahusishwa na CCM na viongozi wake. Watoto wanawasikia wazazi wao wakilalama, redio, magazeti, television vyote vinalalamikia ufisadi na rushwa ndani ya ccm. WATOTO WATAZOMEA, WATAIMBA, WATAWATUPIA MAWE mafisadi kama ilivyokuwa mbeya.
 
Back
Top Bottom