Nimependa thread yako na jinsi ulivyosisitiza kubadilika kwa mwanadamu katika ulimwengu wa sasa ambapo dunia imekua kijiji. Umekata tamaa mno katika maelezo yako juu ya mwanadam, kana kwamba hakuna wenye utashi na wanaoweza simama wenyewe. Huku ukikataa kua maisha hayajawa rahisi, mazuri na salama.
Nazingatia katika eneo la Rahisi, Mazuri na Salama
Haya mambo sio rahisi kiasi hicho, naomba utambue kwamba urahisi wa maisha sasa hivi ndo unaleta matatizo yoote hayo ambayo umeainisha katika thread yako kwa baadhi ya wanadamu.
Vitu vimerahisishwa mno mpaka wakati mwingine mtu ana lemaa kwa kila kitu, unashida na Fulani basi unampigia simu una haja ya kumfuata wengine wanapigiana na wako wote nyumba moja wakati huo huo; msomi kapewa assignment katika level ya chuo hataki kusoma vitabu aelewe na kutafakari mwenyewe badala yake ana google kisha ana copy na kupaste.
Watoto saizi michezo badala ya kwenda kucheza mpira amebwagiwa playstation hapo na kila aina ya game unategemea hio product ya watu hao inakua aina gani?
Ni kweli hivyo vitu vinafaa lakini kwa kiwango, tusipoangalia tunaelekea siko. Hivyo tunapozungumzia urahisi nafikiri tusi egemee urahisi wa watu kuishi bali urahisi wa mambo mengi kurahisishwa na jinsi yanavyopelekea kuharibu maisha huo urahisi ukiendekezwa.
Tunapozungumzi uzuri kwa upande wangu ni ile hali ya kusema walau wengi tunajua nini kinaendelea duniani (utandawazi), jinsi gani tunaruhusu na tunakubali kunyonywa na pia jinsi gani tunamapungufu na madhaifu katika maamuzi na uendeshaji wa sekta muhimu hapa nchini.
Utashi wa kutatua matatizo utatoka wapi na hali viongozi wa jana ni wasomi wa juzi, viongozi wa leo ni wasomi wa jana, wasomi wa leo ni viongozi wa kesho
makundi yote hayo matatu yalikua yakililia haki ya kila raia wa Tanzania wakati wakiwa katika kundi la usomi.
Lakini hayo hayo makundi (wasomi) wanapopata nafasi ambayo wanaweza mtumikia mtanzania na kumbadilisha maisha yake anasahau machungu yake na anakua hapo kwa manufaa ya wachache pamoja na familia yake. Uzuri hapo unakuja kua tunajua yote haya - hapo kale wazazi walikua hawana bahati ya kuelewa nini kinaendelea ndani na nje.
Sisi tunajua NDIO lakini haina maana yoyote sababu ukweli unabaki palepale kua watanzania sisi sio wazalendo. Naangalia wapiga kelele humu nchini ni wale wenyewe hatuna kitu cha uhakika ili kuendesha maisha yetu haya ya kudimba.
Ninapozungumzia usalama sina haja ya kwenda mbali, tukiendelea hivi tulivyo sisi Watanzania, wanajamiii, wasomi, viongozi na kukosa uzalaendo kuna USALAMA KWELI?