Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Simanjiro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka, amepinga vikali matukio ya utekaji yanayoripotiwa kutokea nchini, akiyataja kuwa ni vitendo vya hovyo na visivyokubalika katika taifa linalothamini haki na utu wa binadamu
Akizungumza Oktoba 12, 2025 jijini Arusha katika mkutano na waandishi wa habari, Ole Sendeka amesema vitendo hivyo havina nafasi katika jamii inayotaka kuendelea kwa amani na kuheshimu misingi ya demokrasia
“Utekaji ni jambo la hovyo, halikubaliki kabisa kwa nchi inayojali misingi ya haki na utu,” amesema Ole Sendeka
Amesema si kweli kwamba kila anayekosoa Serikali au chama tawala hujikuta akitekwa, akieleza kuwa yeye binafsi amewahi kutoa maoni makali ya kukosoa Serikali mara kadhaa bila kukumbwa na hali hiyo.
“Kama wangekuwa wanateka wale wanaokosoa na mimi siningetekwa?. Maana kama kuna mtu amekosoa Serikali hii, mimi ni mmoja wao"
Katika maelezo yake, Ole Sendeka pia ametetea uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema hawezi kuhusishwa na vitendo vya namna hiyo kutokana na hulka yake ya upendo na utu
“Rais Samia kwa jinsi alivyokuwa na upendo hawezi kubariki Serikali yake ikajihusisha na vitendo hivyo kama wengi wanavyosema.”
Ameongeza kuwa “Sisi tunaoujua moyo wa Rais Samia na alivyo Muungwana hawezi kutenda dhambi hiyo”.
Akihitimisha, mwanasiasa huyo amewataka Watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha mazungumzo na hoja badala ya hofu na uvumi
Soma pia GE2025 - Ole Sendeka: Utekaji ni jambo la ovyo, na tunapaswa kufahamu ni nani anafanya hivi