Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Alisema ameanza kupata wasiwasi wa namna shauri hilo linavyoendeshwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambayo alidai imepelekewa shauri hilo na Dk. Tulia ambaye ndiye mdaiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Millya alihoji uhalali wa kamati hiyo kushughulikia shauri hilo ilhali mwenye mamlaka ya kulisikiliza ni Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye yuko India kwa matibabu.
Mbunge huyo alisema ameshangazwa kesi hiyo aliyoipeleka kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inafanywa kwa usiri na upendeleo wa wazi ambako wajumbe wa kamati hiyo wanaotokana na Ukawa wameondolewa kinyemela bila hoja za msingi.
“Juni Mosi mwaka huu nilipeleka mashtaka dhidi ya Naibu Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 138, kwa kuwa ndugu Ndugai hakuwapo,Katibu wa Bunge alipokea kama utaratibu ulivyo. Hadi sasa spika hajarudi ofisini,” alisema.
Akielezea kile alichokiita kupigwa danadana na Kamati hiyo, Millya alisema aliitwa kuhudhuria kikao na kamati hiyo Juni 18 saa 4.00 kamili mwaka huu,lakini hakuitwa kuingia kwenye kikao hicho hadi saa 9.00 alasiri na baadaye alipewa taarifa kuwa kikao hicho kiliahirishwa hadi Juni 23, mwaka huu.“Hata hivyo leo (jana) Juni 23 mwaka huu Katibu wa Kamati hajanipa taarifa ya kufika mbele ya Kamati hadi saa 5:15 asubuhi.
“Nilimtumia ujumbe wa simu kujua ni muda gani ninatakiwa kuhudhuria kikao hicho,cha ajabu katibu alikaa kimya na baadaye aliniambia ni saa 5:00. Nilimjibu mbona muda huo umeshapita, alijibu kwamba akidi imetimia na kikao kimeshaanza,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa madai hayo, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, alisema si kweli kwamba Kamati ya Mkuchika inashughulikia suala hilo kwa maagizo ya Naibu Spika Dk. Tulia, bali ni agizo la Spika,Ndugai ambaye aliwaagiza waendelee na shauri hilo.
Chanzo: Mtanzania