Habari wana jamvi naomba tujikumbushe nyuma kidogo, maisha ya shule ya wakati uleee
Nakumbuka wakati namaliza shule ya msingi mwaka 1989 nilikuwa na miaka 16. Nilionekana mdogo sana darasani kwetu kwani wakati huo hasa vijijini watu walikuwa wanaanza darasa la kwanza wakiwa na pubic hair (mav...ziii). Nilipomaliza shule shule ya msingi nilifauli masomo na kuchaguliwa kujiunga shule ya sekondari Mazengo (Dodoma) na ikawa bahati kusoma kwenye mji wa posho ya kukalia viti vya kunesanesa. Hii si mada yangu ngoja niwaambie waskaji zangu, si mnajua tena stori za old-skool zinaanza na historia fupi!!!
Basi washkaji zangu pale Matesesco ambayo baadae ilikuja kuitwa Mazengo Complex na baadae ikabatizwa Dodoma University kwa majigambo ya walimu wake, nilijikuta naingia shule kusoma na mibaba mizima. Kuna watu walikuwa wanamaliz form four huku watoto wao wakifanya mtihani wa darasa la saba na wengine wakioza mabinti zao wa kwanza. Unashangaa nini, ndo ilivyokuwa wakati ule wa elimu ya kuhimizana. Kwenda shule lazima uwe umepata wa kuku-leave kwenye machungo ya ng'ombe (ukikosa no skool).
Shule yetu ilikuwa ya midume mitupu ikichukua wanafunzi wa O-Level na A-Level. Basi bwana kulikuwa na mgawanyo wa kazi ambapo kuna kazi zilikuwa zinafanywa na form one tu. Palikuwa na form one wa masika (Form One kweli) na form one wa kiangazi (Form Five). Hawa walikuwa na kazi ya kusafisha vyombo vya kitchen kwenye muhula wao wa kwanza wanapojiunga na shule. Basi wale wasiosafisha vyombo na meza wakimaliza kula wanachafua mazingira ili kuifanya kazi iwe ngumu kwa wenzao.
Kulikuwa na T.M.O bana wakati huo hakuna cha mobile phones na hata landlines zilikuwa kwenye maofisi na kwa watu wenye uwezo tu. Basi kila siku kabla ya kuingia kwenye bwalo la chakula unapitia kwenye ubao kusoma kama jina lako limo ili ukchukue hela zako za matumizi. Kama jina lako halija-display mpaka mnapokaribia kufunga inabidi ujiandikishe kubaki shule. Mawasiliano nayo yalikuwa kwa njia ya barua tu na kulikuwa na kitu kinaitwa pen-pal (rafiki wa kalamu). Hicho ndo kilikuwa kikikutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali na hasa wavulana kwa wasichana.
Pesa ilikuwa shida lakini barua zilikuwa zinazunguuka tu, kulikuwa na mtindo wa kufuta mhuri kwenye stamp kwa mafuta na kuitumia tena. Ukitumiwa barua yenye stamp mpya, stamp huikuti. Kuna wengine walidiriki hata kurudisha barua kwa kutumia bahasha ya awali kwa kusingizia barua iliotumwa imepotea njia irudi kwa sender.
Basi wana jamvi kuna jamaa mmoja tulikuwa tunasoma darasa moja. Jamaa huyo alipenda sana kwenda kuchukua barua na kuja kuzisoma mbele ya wanafunzi. Jamaa alikuwa na vioja sana. Alikuwa na kofia moja (cap) ya blue ameandika kwa wino Zairwaz, huyu jamaa ilikuwa kila siku lazima apate barua. Na akikosa barua alikuwa anafunga bahasha ya barua zilizopita na kuzisoma upya. Huenda huko mtaani anakoishi (hasa km amepanga) atakuwa anakusanya maganda ya mayai na kuyatupa jalalani mbele za majirani zake.
Kuna mengi sana ya kukumbuka wakati huo .........