Okwi avunja rekodi ya mabao ya Yanga na Azam

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Okwi2.jpg

NAMBA hazidanganyi bwana. Hakuna shabiki yeyote wa soka kwa sasa anayehoji tena ubora wa Emmanuel Okwi. Hata waliokuwa wakimuita Mhenga sasa wamenyamaza baada ya Mganda huyo kuwanyamazisha mashabiki hao.

Dakika 180 alizotumia katika mechi mbili kati ya tatu ambazo timu yake imecheza imethibitisha kuwa Okwi sio mtu wa mchezomchezo.

Mganda huyo alitupia kambani mabao mawili safi wakati Simba ikichapa Mwadui mabao 3-0 na kumfanya kufikisha mabao sita. Manne aliyafunga katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ruvu Shooting, Simba iliposhinda mabao 7-0.

Mabao sita ya Okwi ni mara mbili ya yale yaliyofungwa na kikosi kizima cha Yanga chenye mabao matatu tu katika mechi tatu.

Kama haitoshi ukiyachanganya mabao ya Yanga na mawili ya Azam, bado hayafikii idadi ya magoli yaliyofungwa na Okwi.
 
Hivi OKWI anaweza akawa anaongoza kwa wafumania nyavu duniani eeeee?? Maana akina morata wana goli tatu mechi 4, makaku ana goli 4, Messi ana goli 3 sijui, cavan ana goli 4 sijui, Harry Kane ana goli 2,

OKwi goli 6 mechi 2
 
Mfungaji bora wa msimu uliopita alikuwa na goli 14,ina maana ndani ya mechi 5 za mwanzo Okwi anaweza kamfikia
 
Mfungaji bora wa msimu uliopita alikuwa na goli 14,ina maana ndani ya mechi 5 za mwanzo Okwi anaweza kamfikia
Huyu OKWI ni mnyamaaaa! Upande wa pili naona wamepigwa na kitu chenye ncha Kali, wametuliiiiiaaaaa tuliiiii! Hatusikii Tena maneno kwamba Okwi ni mhenga???
 
Back
Top Bottom