Okwi Aanza Kupekenyuliwa

Okwi Aanza Kupekenyuliwa

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
mg1134.jpg
 


Mahmoud Zubeiry
12/28/2013 03:10:00 PM
0 comments


[h=1]OKWI AMEANZA TABIA ZAKE ZA SIMBA NA ETOILE HATA YANGA SC?[/h] Home » Unlabelled » OKWI AMEANZA TABIA ZAKE ZA SIMBA NA ETOILE HATA YANGA SC?
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
UNAKUMBUKA ile tabia ya Emmanuel Okwi Simba SC kuchelewa kurejea mazoezini baada ya kuruhusiwa kwenda kwao Uganda kupumzika au kujiunga na timu ya taifa?
Na si ndiyo tabia hiyo hiyo imechangia mgogoro wake na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia? Basi ni kama anataka kuileta na katika klabu yake mpya, Yanga SC.
Mshambuliaji huyo pamoja na Mganda mwenzake, Hamisi Kiiza ndiyo pekee ambao hawajarejea nchini kujiunga na timu kati ya wachezaji wa kigeni, baada ya ruhusa ya muda mfupi kurejea nyumbani kwao.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Ameanza kuwazingua na Yanga? Emmanuel Okwi hajarejea kujiunga na wenzake baada ya ruhusa ya mapumziko mafupi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Yanga imeanza jana mazoezi chini ya kocha Freddy Felix Minziro, lakini Okwi na Kiiza hawakuwepo na taarifa zinasema hawajarejea nchini kabisa na haijulikani watakuja lini, wakati timu ipo kwenye maandalizi ya Kombe la Mapinduzi, michuano inayotarajiwa kuanza Januari 1, mwakani.
Mbali na Okwi na Kiiza, wachezaji wengine ambao hawajaripoti mazoezini ni kipa Juma Kaseja, ambaye na ruhusa maalum hadi Jumatatu na viungo Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Hamisi Thabit na Hassan Dilunga ambao wote wanaumwa Malaria na Daktari Nassor Matuzya amethibitisha.
Okwi alikuwa mchezaji wa Simba SC ya Dar es Salaam tangu mwaka 2010 hadi alipouzwa Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka huu kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akavurugana na klabu yake hiyo mpya wa tuhuma za kuchelewa kujiunga na timu baada ya kuruhusiwa kurejea Uganda kuichezea timu yake ya taifa.
Inadaiwa, Okwi aliporejea Tunisia Etoile ikamkata mshahara na kumuamuru akafanye mazoezi na kikosi cha pili, lakini akagoma kufanya hivyo kurejea kupumzika kwao Uganda, akidai halipwi mishahara na kufungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Baada ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya huko ili kunusuru kiwango chake jambo ambalo alifanikiwa na mwezi huu amehamia Yanga.
Tayari Yanga imepata ITC ya mchezaji huyo, lakini klabu yake ya zamani, Simba SC inapinga usajili wake kwenda Jangwani akitokea SC Villa kwa sababu ni mchezaji wa Etoile.
Wakati huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa FIFA, huku mustakabakali wa usajili wake Yanga ukiwa mikononi mwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Je, Okwi ndiyo amehamia Yanga na usumbufu wake aliokuwa anawafanyia Simba SC na Etlile du Sahel?
​
 
[h=1]JOSEPH OWINO AMWAGA SIRI ZA EMMANUEL OKWI[/h]




Beki wa kimataifa wa Simba, Joseph Owino amemtaka Mganda mwenzake aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni, Emmanuel Okwi kuachana na vitendo vya starehe ili aweze kuwa katika kiwango kizuri kwa muda wote atakaokuwa na klabu hiyo kwa kuwa hiyo ndiyo siri pekee ya mafanikio yake.



Owino amesema kuwa endapo Okwi hatafanya hivyo, itakuwa ni vigumu kwake kufikia mafanikio aliyoyapata awali wakati akiwa Simba.


Alisema anaifahamu vilivyo tabia ya Okwi kuwa ni mtu wa mambo mengi tangu walipokuwa pamoja SC Villa Uganda na baadaye Simba, ambapo amesisitiza kuwa huu ndiyo muda wa mabadiliko ili afanye kazi na hakuna siri ya ziada ya mafanikio zaidi ya hiyo.


"Kama asipokuwa makini na kuendekeza starehe, mambo yanaweza yakamwendea vibaya na kujikuta asifikie kiwango chake kama alichokuwanacho wakati ule akiwa Villa na baadaye Simba.


"Namjua vizuri sana Okwi, kuwa ni mtu wa mambo mengi lakini anatakiwa kupunguza mambo hayo kwa faida ya soka lake lakini pia asichukiwe na mashabiki wa timu yake mpya ya Yanga," alisema Owino.


Okwi ametua Yanga akitokea SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na tayari ameanza kuonyesha makali baada ya kuifungia bao timu hiyo katika mechi dhidi ya Simba, Jumamosi iliyopita katika mechi ya Nani Mtani Jembe, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 
Sio kila habari ya kwenye hivyo viblog uchwara inastahili kuwekwa hapa JF.JF ina standard zake mkuu punguza hizo copy &paste
 
Sio kila habari ya kwenye hivyo viblog uchwara inastahili kuwekwa hapa JF.JF ina standard zake mkuu punguza hizo copy &paste

Hivi kinacho-matter ni ukweli wa habari au source ya habari?Mkuu hebu wewe tupia basi hizo news zenye hadhi yakuwa JF kutoka kwenye hizo blog makini.
 
Michezo Ni nidhamu ndani na nje ya kiwanja kama halijui Hilo litamcost maisha yake yote michezoni.Team imewekeza pesa halafu unaleta usharobaro!Hata world class players hawafanyi hiyo.he should change.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom