Okoa uchumba, ndoa na familia yako

NAXFRA

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
392
74
Uzoefu unaonesha kuwa, miaka ya hivi karibuni ulimwengu umekuwa ukishuhudia mabadiliko ya ajabu katika ndoa na familia hata na zile za wakristo.

Mabadiriko haya yanachagizwa na sababu nyingi ambazo zimepelekea familia za kikristo kuyumba sana na kusababisha aidha kuvunjika, kuwa na migogoro isiyokoma, watoto kutokuwa na maadili mema, mimba za utotoni kwa watoto, usaliti katika ndoa, uzinzi na ngono zembe kwa vijana, magonjwa ya kisaikolojia yatokanayo na changamoto za kifamili au vifo miongoni mwa wanafamilia kwa sababu ya maambukizi ya VVU.

Shetani amekuwa akitumia kila njia ili kuuondoa utakatifu na mfumo thabiti uliohalali wa ndoa aliouweka Mungu; kwani kwa miaka ya hivi karibuni pamekuwepo na ongezeko la ndoa za jinsia moja, tendo la ndoa kufanya kinyume na maumbile, talaka katika ndoa huku madhehebu baadhi ya kikristo na imani nyingine zikiunga mkono bila ya kujua kuwa wanafanya kufuru kwa Mungu Muumbaji wao.

Kitabu hiki chenye jina la Uchumba na Maisha ya Ndoa Katika Misingi ya Kikristo ni kitabu ambacho kimeandikwa kwa makusudi mazima ya kutoa elimu, ufahamu, ujuzi na maarifa jinsi ya kujenga urafiki na mahusiano bora, kuuelewa uchumba wa kweli na hatua zake katika misingi ya kibiblia, madhara ya kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa na jinsi ya kuacha au kuepuka kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa,

kanuni za kibiblia katika kujipatia mchumba anayepaswa kuwa mwenzi wa maisha, mambo ya kuzingatia kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia katika ndoa, utakatifu wa ndoa na makusudi ya Mungu kuasisi ndoa kwa wanadamu, vyanzo vya migogoro katika ndoa na namna ya kufanya ndoa kuwa zenye ustawi mzuri, jinsi ya kuwa mke au mume mwema katika ndoa na familia, jinsi ya kuifanya familia kuwa ya kiroho na yenye furaha na amani, malezi sahihi ya watoto katika misingi ya kikristo, kiasi na uwakili katika familia za kikristo.

SOMA HIKI KITABU RAFIKI MDAU: "Uchumba na Maisha ya Ndoa Katika Misingi ya Kikristo" by MWL. Frank Philemon
 

Attachments

  • Uchumba_na_Maisha_ya_Cover_for_Kindle.jpg
    Uchumba_na_Maisha_ya_Cover_for_Kindle.jpg
    166.8 KB · Views: 88
Back
Top Bottom