Okoa hii ndoa.

chetuntu

R I P
Jan 10, 2011
949
109
Habari wana JF, naomba mchango wa mawazo yenu. Kuna kaka ameoa na familia ya watoto 2, mke wake ni mfanyakaz pia anasoma evening classes. Tatizo huyo bibie hapatikani home kuanzia monday to sunday. Weekdays anawahi misa za alfajir hata watoto wanaandaliwa na house girl na baba yao.kurudi ni saa 4 na mafoleni. Dada amejikita kanisani jumamosi anaenda misa ya alfajiri kumi na moja, akitoka anaunganisha shule, jioni anaunganisha kanisani pia ni katibu wa kinamama, mzee wa kanisa kwa maandalizi ya jpili, then anaunga mazoez ya kwaya na kusalimia wagonjwa. Kurudi ni saa 2 au 3. Jumapili anaenda misa ya kwanza, akitoka ni kutembelea wagonjwa, kurud ni jioni kabisa. Watoto mama yao kawa house girl. Ameshaonywa sana, sasa ni miezi mingi.
 
Mambo my dear, sijakuonaona ulijipa mapumziko? Kwa mada yako,Hapo hata sala anazoomba sidhani kama mungu anazisikia, maana imeandikwa tupende vyetu na kujali vyetu kwanza ndio unaweza wafanyia wengine, au kuna kitu anakikimbia hapo nyumbani. Mume amuitie wazee watu wazima ili waweze mpa darasa. anawanyima watoto wake haki ya msingi.
 
My Dear mumewe ndo kakutuma? Mwambie aongee na mkewe kwanza. Mambo ya ndoa magumu sana unaweza ukashauri wakakugeuka baadae. Maoni yangu yashanikuta haya
 
nipo dear majukumu, yani dada kawa busy mno na kanisa ,thanx kwa ushauri
 
Kila kitu kwa kiasi wapendwa!!
Huwezi kutumikia kanisa tuuuuu na kanisa la nyumbani (familia) inakusubiri.
Huyu mama ukweli wa kwa nini anafanya hivyo anaujua, na kama ni mtumishi wa Mungu na anajua anachokitumikia kwa kweli,
hapa inabidi arudi ajitazame vizuri.
 
nipo dear majukumu, yani dada kawa busy mno na kanisa ,thanx kwa ushauri

We mwache tu atakija kuta housegirl kamaliza kila kitu, wamama huwa wanajisahau sana tunapoolewa, huu ni uselfishness flani hivi. hapoakikuta mume kachukuliwa atamlaumu nani?
 
My Dear mumewe ndo kakutuma? Mwambie aongee na mkewe kwanza. Mambo ya ndoa magumu sana unaweza ukashauri wakakugeuka baadae. Maoni yangu yashanikuta haya

Dear tuliombwa ushauri na kaka keshasema sana na bibie.
 
We mwache tu atakija kuta housegirl kamaliza kila kitu, wamama huwa wanajisahau sana tunapoolewa, huu ni uselfishness flani hivi. hapoakikuta mume kachukuliwa atamlaumu nani?

Halafu atarudi kanisani kulia. Haya makanisa yetu ya nyakati hizi ni hatari.
 
shida ya haya makanisa ni wabinafsi sana...

sasa hapo ni kumwachisha hilo kanisa kwa nguvu...
 
Mwambie huyo kaka ampe likizo housegirl.
Akakae kwao kama mwezi hivi.
Akiondoka huyo mama hatokwepa majukumu yake ya umuhimu.
 
Nawaonea huruma watoto wanakosa kabisa mapenzi ya mama..
Mshauri huyo baba aongee sana na mkewe na asimame kama kichwa cha familia!!!
 
My Dear mumewe ndo kakutuma? Mwambie aongee na mkewe kwanza. Mambo ya ndoa magumu sana unaweza ukashauri wakakugeuka baadae. Maoni yangu yashanikuta haya

Dena umenena vyema nshasutwa na dadangu wa baba mmoja mpaka nkaloa,ndoa za watu si za kuingilia kabisa akiona yamemshinda atachukua hatua bila ushauri wa mtu,tukae mbali tuangalie kwa macho....
 
Chetuntu; Huyo Baba ajaribu kuenda na move ya mkewe kwa at least wiki moja kuanzia j'pili, ili aone hicho kizuri kinacho mkeep busy mke wake, I hope atapata mengi sana then atakuwa kwenye position ya maamuzi. Ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze mydear
 
mwambie huyo baba ajichunguze mienendo yake! kuna kitu atakuwa amefanya kilichomkwaza mkewe,i guess nyumbani huyo mwanamke ameikosa amani she turned to church kama vile watu wanavyoturn to alcohol ama smoking to avoid problems,i think pia hakuna communication baina yao,ajitahidi avunje ukimya aongee na mkewe amwambie hamzuii kwenda church ila awe na kiasi.
 
Uko sahihi..
Tatizo linaweza kuwa hapo. Kuna kitu kina m-turn off hapo nyumbani! Wajaribu kuangalia ni tatizo gani
 
mwambie huyo baba ajichunguze mienendo yake! kuna kitu atakuwa amefanya kilichomkwaza mkewe,i guess nyumbani huyo mwanamke ameikosa amani she turned to church kama vile watu wanavyoturn to alcohol ama smoking to avoid problems,i think pia hakuna communication baina yao,ajitahidi avunje ukimya aongee na mkewe amwambie hamzuii kwenda church ila awe na kiasi.

thanx dear kwa mchango alishamwambia apunguze ndo kaacha kwenda kwenye mikesha
 
Habari wana JF, naomba mchango wa mawazo yenu. Kuna kaka ameoa na familia ya watoto 2, mke wake ni mfanyakaz pia anasoma evening classes. Tatizo huyo bibie hapatikani home kuanzia monday to sunday. Weekdays anawahi misa za alfajir hata watoto wanaandaliwa na house girl na baba yao.kurudi ni saa 4 na mafoleni. Dada amejikita kanisani jumamosi anaenda misa ya alfajiri kumi na moja, akitoka anaunganisha shule, jioni anaunganisha kanisani pia ni katibu wa kinamama, mzee wa kanisa kwa maandalizi ya jpili, then anaunga mazoez ya kwaya na kusalimia wagonjwa. Kurudi ni saa 2 au 3. Jumapili anaenda misa ya kwanza, akitoka ni kutembelea wagonjwa, kurud ni jioni kabisa. Watoto mama yao kawa house girl. Ameshaonywa sana, sasa ni miezi mingi.

Ushauri huu wa Paul mtume unaweza kusaidi "HAKIKA IKIWA YOYOTE AWANDALII WA KWAKE MAHITAJI YAO NI MBAYA KULIKO YULE ASIYE NA IMANI" 1Tim.5:8, pia Mfalme sulemani alibainisha sifa za mke bora kwenye kitabu cha Mith. 31:10-31 natumaini ushauri huu unaweza kufaa
 
Inawezekana huyo dada ameuingia wokovu kwa pupa.. manake inabidi asome biblia vizuri aelewe. Anashindwa kubalance familia na ulokole. Makanisa mengine ya kilokole yanatoaga mafundisho tofauti.. usipokuwa makini unaweza kuacha hata kwenda kazini ukawa unashinda kanisani. Sina hakika kama anasali makanisa ya kilokole au vp. Huo ni mtazamo wangu kuhusua wengi wanaochipukia wokovu. Unakuwa unaona kama dunia ndio inafikia mwisho.. yaani tabu juu ya tabu
 
Back
Top Bottom