Mkuu,
Magari mengi huharibika si kwa sababu ya ubovu au makosa ya mtengenezaji, bali kwa sababu ya ushauri wa kimazoea kutoka kwa baadhi ya mafundi wa chini ya mwembe.
Kauli kama “engine hii ni mbovu” au “gearbox hii haifai” au "Bongo joto" mara nyingi si za kweli. Ukweli ni kwamba baadhi ya injini za kisasa hazivumilii uzembe au matunzo yasiyo sahihi, hasa kwenye matumizi ya engine oil.
1. Hoja ya 0W-20 kuwa nyepesi kwa joto la nchi za tropiki si sahihi kitaalamu.
Joto la nje (ambient temperature) halina uhusiano wa moja kwa moja na joto la ndani ya injini, isipokuwa wakati wa kuwasha gari. Joto la ndani ya injini hufikia hadi 100–110°C, so kusema huku bongo kuna joto si sahihi coz joto letu la 30–35°C la mazingira ya hapa bongo ni dogo kuliko la ndani ya engine.
Oil ya 0W-20 imeshapimwa na kuthibitishwa kufanya kazi kwenye joto hilo la ndani ya engine.
Pia, fully synthetic 0W-20 za kisasa zina high shear stability na hazigeuki “kama maji”. Ndiyo maana Subaru, Toyota, Honda n.k hawaandiki oil tofauti kulingana na nchi au hali ya hewa. Wanataja oil moja tu dunia nzima kulingana na walivyoiunda engine.
2. Hoja ya oil clearance ndogo
Ni kweli kwamba injini ya FB20 ina tight tolerances. Lakini hitimisho la kutumia oil nzito si sahihi. Ndiyo maana mtengenezaji ametaja oil nyepesi ya 0W-20 badala ya 5W-30. Oil nzito hupunguza oil flow kwenye maeneo nyeti ya engine, huchelewesha lubrication wakati wa kuwasha, na huongeza uchakavu wa crankshaft na bearings baada ya muda.
3. Kauli kwamba “SJ5 inakula oil na head gasket inaharibika kirahisi”
Hapa mkuu matatizo mawili tofauti yamechanganywa:
a) Kula oil husababishwa na kuchelewesha kubadili oil, kutumia oil isiyo sahihi au fake, uwepo wa tope la oil kwenye engine, oil kuvuja sababu ya kuchaa kwa seal za valve n.k. Hili si tatizo la Subaru SJ5 pekee.
b) Head gasket failure mara nyingi husababishwa na overheating, oil kuchelewa kusambaa kwenye injini, matumizi ya oil isiyo sahihi kama hivyo kuweka 5W30 badala ya 0W20, tatizo la cooling system n.k
4. Hoja ya 5W-30 kuua engine
Hoja hii ina sehemu ya ukweli, si kwa sababu 5W-30 ni oil mbaya, bali kwa sababu FB20 haikubuniwa kwa oil hiyo. Uzito wake husababisha kuchelewa kwa lubrication, kuongezeka kwa msuguano na uchakavu wa bearings. Hapo lazima engine ife.
Matatizo mengi ya magari ya kisasa yanatokana na kusikiliza ushauri wa kubahatisha au kukariri teknolojia za zamani. Ukifuata maelekezo ya mtengenezaji, injini itadumu bila matatizo makubwa.
Nimetumia 0W20 kwenye RVR na Prius kwa miaka, sikuona shida. Shida inaanza ukianza kuweka ubunifu wako.