Ogopa sana MACHOZI ya Binadamu

Ogopa sana MACHOZI ya Binadamu

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,673
Reaction score
14,052
Naam machozi....ni kwa muda mrefu sana nimefuatilia pasi kuwa na shaka,hakuna kitu hatari chini ya jua hili hili tunalolijua kama machozi ya binadamu naam hasa ya mtu mzima haijalishi ni mwanamke au mwanaume.

Kiuhalisia machozi si lazima uone yale maji yanayotiririka toka machoni la hasha,....kuna machozi yasiyo onekana kwa macho mtu anaugulia kwa ndani tu...lakini moyo wake unatiririsha machozi mpaka ya damu.

Mbaya zaidi ukute mtu huyo ukiwa nae anatabasamu tu...wala hakuambii manake unajua ubaya unaomfanyia.

Hii si kwenye mambo ya mahusiano tu ni mpaka makazini..wewe bosi amekupa kazi anakulipa kwa wakati lakini wewe ndiye mtu wa kwanza kunajisi ofisi, hila, fitna, maneno ya chinichini na umbeya usiokua na maana ule wa kubomoa bila kujua hiyo ni sehemu ya kupatia riziki.

Pia wale ndugu wanaokaa kwako / kwenu mnawanyanyasa kwa siri hawana wa kumwambia lakini machozi yao yako ndani kwa ndani hii ni hatari, balaaa kubwa manake hakika machozi haya huwa hayaendi bure.
 
Back
Top Bottom