Ogopa sana kusaidia mtu ndiye atakayegeuka kuwa nyoka kwako na kutaka kukuangusha

Granted Faith

Member
Jul 4, 2021
57
292
Tuwe Makini sana Kusaidia watu kwa njia yeyote ile mwishoe anageuka kuwa nyoka na kukung’ata bila huruma yeyote huyo huyo uliyemsaidia ndo huyo atakae kuua huku unaangalia.

Aisseee imefika stage now sitaki kumsaidia mtu yeyote yule kwenye haya maisha kila mtu apambane na hali yake siwezi kujitengenezea nyoka mwenyewe hili aje kuning’ata bila huruma.

Ndio haya ya Diamond Platnumz kumsaidia Harmonize leo anamuona takataka.

Binadamu ni sawa na Mbwa wasiokuwa na Shukrani
 
Hii ilinikuta. Jamaa alikuwa msafisha ofisi nikamfundisha ujuzi wambao ulifanya niajiriwe pale. Baada ya kuwa vizuri akanipakazia kwa boss. Matendo yalionesha kwamba sihitajiki. Nilijiondokea nilimsamehe.

Muhimu, watu hutofautiana.

Saidia tu.
 
Hakuna mafanikio kwa mwanadamu bila ya KUSAIDIWA NA WENGINE......

Muhimu umakini
Muhimu kanuni.

Ila tusisahau kuwa tumezikuta SADAKA NA ZAKA katika nyumba za ibada na huwa tunazitoa bila ya KUTEGEMEA "IN RETURN".....

Waswahili wanasema "Riziki ya mtu iko kwa mtu"

#KaziIendelee
 
Nakupinga, Tatizo letu binadamu tunasaidia tukitegemea malipo mazuri wakati ulishaambiwa "Tenda wema Nenda zako" Vitu vyote vipo planned tayari kwamba mtu huyu atapita hapa, atasaidiwa pale ili afike pale hivyo ukiwa na moyo wa kusaidia we saidia uende zako, Usisubiri malipo.
 
Ila sis binadamu sijui tunashida gani
Unatengeneza chuki kwa mtu aliyekuwa anakupa msaada siku zote kisa tu ameshindwa kukupatia kile unachohitaji kwa siku moja
 
POle sana mkuu
Ni kitu kimoja kinauma sana pale kinapotokea

Lakin tusiache kusaidiana pale inapowezekana
 
Tuwe Makini sana Kusaidia watu kwa njia yeyote ile mwishoe anageuka kuwa nyoka na kukung’ata bila huruma yeyote huyo huyo uliyemsaidia ndo huyo atakae kuua huku unaangalia.

Aisseee imefika stage now sitaki kumsaidia mtu yeyote yule kwenye haya maisha kila mtu apambane na hali yake siwezi kujitengenezea nyoka mwenyewe hili aje kuning’ata bila huruma.

Ndio haya ya Diamond Platnumz kumsaidia Harmonize leo anamuona takataka.

Binadamu ni sawa na Mbwa wasiokuwa na Shukrani
Jifunze kuishi kipebari ubinafsi ndio njia nzuri ya mafanikio we unaishi maisha ya kijamaa utabaki maskini na utasambaritika kama USSR
 
Lugha nyepesi tu mtu akikuomba msaada Mwambie huna. Waswahili walinena Huruma uzaa dhambi ama ukimfurahisha kila mtu utakufa maakini.

Mimi Sasa hivi hata sigara nikiombwa sitoi
 
ukiamua kumsaidia mtu msaidie tuu....usitegemee asante....wote tu wahitaji...kwa namna tofauti...
 
Mkaldayo bana haya saisia kila mtu tuone sasa

Sipingani na hoja, ila nimepuuza mfano wa Harmonize sijui Mayonnaise.

Wale wanashindana kibiashara, huwezi kusema mmoja kakosa fadhira…. huko ni kutaka kutukuza mmoja kisa alikusaidia hatua fulani.
 
Lugha nyepesi tu mtu akikuomba msaada Mwambie huna. Waswahili walinena Huruma uzaa dhambi ama ukimfurahisha kila mtu utakufa maakini.

Mimi Sasa hivi hata sigara nikiombwa sitoi

IMG_1867.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom