Ofisi za Serikali huwa wanakataliwa kupokea simu au ni kiburi tu?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,802
Wanabodi,

Ofisi za serikali kutokupokea simu kwao ni jambo la kawaida sana. Kama unashida wizara yoyote ya serikali au idara yoyote ile jaribu kupiga simu, kamwe simu haitapokelewa.

Unaweza ukapiga asubuhi, mchana mpaka muda wa kutoka simu hazipokelewi. Hizo simu huwa zinawekwa wapi?

Unaweza kuwa upo Arusha unashida wizara fulani ni lazima uende ofisini au umuagize mtu aende ofisini au kama kuna mtu unamfahamu pale ndio umpigie simu yake ya mkononi. Ukituma email ndio sahau kabisa, hujibiwi milele. Wenzetu private ukipiga ikiita sana mara mbili na email zinajibiwa ndani ya masaa 24.

Kwa mnaofanya kazi ofisi za serikali mtusaidie, huko wenzetu huwa mnakataliwa kupokea simu za wananchi mnaowahudumia au ni kiburi tu.?
 
Pole sana mkuu.Wafanyakazi wengi wa serikali wameigeuza ajira ya serikali kama shamba la bibi.Hawaitilii maanani maadamu mwisho wa mwezi pesa ipo.Uwajibikaji mbovu kabisa katika sekta mbali mbali
 
Wanabodi,

Ofisi za serikali kutokupokea simu kwao ni jambo la kawaida sana. Kama unashida wizara yoyote ya serikali au idara yoyote ile jaribu kupiga simu, kamwe simu haitapokelewa.

Unaweza ukapiga asubuhi, mchana mpaka muda wa kutoka simu hazipokelewi. Hizo simu huwa zinawekwa wapi?

Unaweza kuwa upo Arusha unashida wizara fulani ni lazima uende ofisini au umuagize mtu aende ofisini au kama kuna mtu unamfahamu pale ndio umpigie simu yake ya mkononi. Ukituma email ndio sahau kabisa, hujibiwi milele. Wenzetu private ukipiga ikiita sana mara mbili na email zinajibiwa ndani ya masaa 24.

Kwa mnaofanya kazi ofisi za serikali mtusaidie, huko wenzetu huwa mnakataliwa kupokea simu za wananchi mnaowahudumia au ni kiburi tu.?

Hili nalo ni neno. Na mimi nilisema, wakati utaratibu wa kuhamia Dodoma ukiendelea, mawasiliano ya simu, email na websites kuwa up-to-date ni muhimu yakaboreshwa saana. Ingewezekana hata kuanzishwa kitengo maalumu cha mawasiliano (Call Center) cha serikali yote kuu cha kupokea na kudirect watu kwenye vitengo sahihi.

Pia taratibu za kupokea fomu na applications mbalimbali kwa njia ya posta na internet nao ungeboreshwa sana. Ufanisi maeneo ya kazi bado sana nchi hii, siyo serikalini, siyo sekta binafsi.
 
Ni ukweli mtupu kabisa...
Landline nyingi hazipatikani, na ikipatikani haipokelewi kwamwe...

Email ndiyo sahahu kabisa ukituma...

Ndiyo maana ofisi nyingi za serikali, hawaangaiki kusema tuma email au piga simu... Utasikia rudi tarehe fulani...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom