Simu za maofisini (land line) hazifanyi kazi kwenye ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na Taasisi zake Tanzania

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,797
21,392
Ninaandika mada hii kwa masikitiko makubwa sana,ofisi za umma,mashirika ya umma na taasisi zake tanzania hazitumia simu za land line ili kuwahudumia wananchi.

Matokeo yake viongozi,watendaji wa serikali wanatembea na ofisi zao mifukoni mwao. Wawekezaji wanatafuta simu za maofisi wakiwa nje ya nchi wanapiga hadi wanakata tamaa.

Mfano. Simu za wizara ya mambo ya nje, haijulikani upige za ofisi dodoma au dar ? Ukizipiga zinaita siku Zima hakuna majibu.

Mf. Haijulikani simu ya ofisini ya Prof. Kitila Mkumbo na haipatikani Hadi mwekekezaji atafute simu ya wazirinya mkononi na sio rahisi kuipata na wakati huo huo waziri Huyo anaye secretary na Yuko ofisini anachst tu na mshahara analipwa.

Mifano ni mingi.
 
Yani inasikitisha sana!

Sasa sijui wanaweka nmba za nini?! Bora ijulikane moja kuwa hawataki kupokea na namba wasiweke!
 
Ukipiga simu inaweza kuwa haipatikani kabisa

Au

Ikipataikana itaita tu weeeee mpaka uchoke bila kupokelewa!

Halafu kuna watu wanasema eti uchumi wa kati.
 
Mwenye namba ya simu ya mkurugenzi wa TPDC naomba anisaidie.

simu yake ya mezani hata siijui.

nimepiga ya ofisi najibiwa hovyo na masekretari
 
Back
Top Bottom