Ofisi za Q-NET Kilimanjaro na Arusha zafungwa. DC Sabaya apongezwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wakati Serikali na vyombo vya dola vikiendelea kuchunguza uhalali wa uwepo wa kampuni ya biashara za mtandao ya Q-NET inayodaiwa kuwatapeli wananchi mamilioni ya fedha,ofisi za kampuni hiyo ziliopo mikoa ya Arusha na Kilimanjaro zimefungwa na Wafanyakazi wake hawajulikani walipo.

Awali mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliibua utapeli wa kutisha unaofanywa na kampuni hiyo kwa kuwatapeli walimu ,wastaafu na wafanyabiashara wilayani himo ambapo Sabaya aliamuru kukamatwa na kuhojiwa na Wafanyakazi wa kampuni hiyo na vyombo vya dola.

Baada ya kukithiri kwa madai ya wananchi na kuongezeka kwa mijadala kwenye mitandao ya kijamii, kufuatia DC Sabaya kuweka wazi kilio cha wananchi wakidai kutapeliwa na kampuni hiyo mkoani Kilimanjaro, Jeshi la Polisi limeamua kuingilia kati.

Baadhi ya WANANCHI waliotapeliwa bado wanahaha kujua hatima ya fedha zao walizopanda ikiwemo kushinda wamekaa katika ofisi hizo ambazo zimefungwa wakiwasaka Wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Q-NET ili warejeshewe fedha zao.

Baadhi ya wahanga wa kampuni hiyo wamempongeza DC Sabaya kwa ujasiri alioufanya kwa kuibua madudu yanayofanywa na kampuni ya Q-NET inayoogofya hapa nchini na kusaidia kunusuru WANANCHI wengine wasiendelee kutapeliwa.
 
Hawa jamaa kweli ni matepeli lkn utapeli wanaofanya hamna sheria inaweza kuwafunga kwa Tanzania labda sheria zibadilishwe. Njia rahisi ya kuwazuia ni TCRA kuzuia hiyo playform (QNET.COM) ya kieletronic wanayoitumia kama wanaweza fanya hizo.
 
hawa jamaa kweli ni matepeli lkn utapeli wanaofanya hamna sheria inaweza kuwafunga kwa tanzania labda sheria zibadilishwe. njia rahisi ya kuwazuia ni TCRA kuzuia hiyo playform (QNET.COM)ya kieletronic wanayoitumia kama wanaweza fanya hizo.

Ukisema hakuna sheria inayoweza kuwafunga una maana gani? Hakuna kosa la kujipatia hela kwa udanganyifu?
 
Wafungwe hao waliotapeliwa liwe fundisho, ukiona mtu anataka kukupa sijui diri au utafanikiwa ukifanya hivi, piga keleleeee za kuomba msaada
 
Hawa jamaa kweli ni matepeli lkn utapeli wanaofanya hamna sheria inaweza kuwafunga kwa tanzania labda sheria zibadilishwe. njia rahisi ya kuwazuia ni TCRA kuzuia hiyo playform (QNET.COM)ya kieletronic wanayoitumia kama wanaweza fanya hizo

Rejea maswali ya Sabaya ndio utajua alikuwa akiwasanua wengine kwamba sepeni, mkizubaa tusilaumiane.

1. Mmesajiriwa brela, na mnalipa kodi?
2. Mnafanya biashara gani, yaanj mnauza nn?
3. Makao makuu ya kampuni yenu ni wapi?

Serikali ikiona wewe ni pasua kichwa unakula uhujumu uchumi au utakatishaji fedha. Sema kwa vile hata hao wanaopiga piga kelele kwenye mabanda yao nao ni masikini tu wahanga, ndio maana wakawaacha tu.
 
Hakuna utapeli. Hii yote ni kutaka pesa kwa njia rahisi. Wangefanikiwa wangekuja hadharani kusema? Wangelipa lipa kodi TRA? Lazima watu tufanye kazi na tusome yale small prints.
 
Back
Top Bottom