jamani mbeguuuuu........ops! mpanzi alipanda kwenye mwamba...
mpanzi alipanda kwenye mwamba...
jamani mbeguuuuu........ops! mpanzi alipanda kwenye mwamba...
Inawezekana wenyewe wametengeneza fujo maana walijua leo wanafikishwa mahakamani. Waliitwa kwenye kikosi kazi cha serikali maeneo fulani jijini Dar es Salaam, karibu na Kariakoo, ambako walikuwa hawajiamini na hivyo kuibua wasiwasi mkubwa kwa watendaji wao na wanachama wengine.
Ndugu wanajukwaa,
Nimefuatilia suala la DECi kwa shauku toka kabla halijaanzwa kuandikwa na magazeti na hata baada ya hapo. Ninashawishika kusema kuwa kuna habari nyingi sana tunafichwa juu ya suala hili lote hasa kwenye fedha. Habari zilizopo ni kuwa wanachama wa DECI ni zaidi ya 700,000 na kwa kuwa fedha kama ya kiingilio (isiyorudishwa) ni Shilingi 20,000 kuna Shilingi Bilioni 14 (ambazo ndizo zinazotajwa). Hapa hatutaji mbegu ambayo mimi nafikiri ni fedha nyingi sana na za kutisha kwa sababu ukichukua idadi ya wanachama 700,000 ukazidisha kwa kiasi cha kama 100,000 (kama kiwango kidogo cha wastani cha mbegu) naona kiasi kinatisha (700,000,000,000)!!
Pili jambo hili halihusishwi na money laundering? Na ninazidi kutishika ninapofikiria jinsi ilivyoweza kufanya kazi muda wote wa zaidi ya miaka miwili bila ujasiri wa kuisimamisha. Na natishika zaidi kufikiria Kenya ilikuwepo kama hii.
Mnaonaje wanajukwaa?