Ofisi za DECI zavamiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi za DECI zavamiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Jun 9, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna taarifa kwamba ofisi za DECI zilizopo Mabibo, Dar es Salaam, zimevamiwa na watu waliofika na magari na kurusha mawe.

  Wakati hayo yakitokea, viongozi wote wa DECI walikuwa wameitwa na vyombo vya dola kwa "kazi maalumu".
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  jamani mbeguuuuu........ops! mpanzi alipanda kwenye mwamba...
   
 3. R

  REOLASTON Member

  #3
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbegu zimegoma kuota.
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inawezekana wenyewe wametengeneza fujo maana walijua leo wanafikishwa mahakamani. Waliitwa kwenye kikosi kazi cha serikali maeneo fulani jijini Dar es Salaam, karibu na Kariakoo, ambako walikuwa hawajiamini na hivyo kuibua wasiwasi mkubwa kwa watendaji wao na wanachama wengine.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Too bad!
   
 6. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jamani watanzania tuchape kazi. Hata Mungu alisema utakula kwa jasho lako, angalia kitabui cha mwanzo sina hakika na mstari wa ngapi. Sasa hawa DECI wanapingana na agizo la Mungu la watu kula kwa jasho?
   
 7. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  dah! sijui itakuwaje? nilikuwa nimepanda kama laki mbili hivi jamani,uuuuuuuuuuuuwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwi lazima pesa yangu irudiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Walitegemea ziote....eeeh!

  BWT: Smart people these days play with people's minds especially of the poorest....!
   
 9. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo itakuwa imekula kwao!!"
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  apo ikawa rahisi kwa ndege kuziona, wakazila, nyingine zikakauka kwa kukosa udongo mzuri....
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Mkuu Halisi, these DECI guys know exactly what they are doing....sana sana wanaombea Mungu hii hali ya mashaka iendelee ili wajustify kuingia mitini na hela za 'wanachama' wao....too bad
   
 12. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kama inawezekana kupanda mbegu na zikazaa basi tukubali vilevile tunapozipanda na zikafa. Hiki ni kifo cha mbegu zetu, tuandae mazishi na watu waabiwe hakuna matanga.
   
 13. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wapanzi wa mbegu wamechemsha....
  Afadhali ya yule jamaa aliyekuja kung'oa kiyoyozi (Air Condition) na kutambaa nayo.......
   
 14. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #14
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa upande wangu nawachukulia waathirika wote wa mchezo huu kama watu wanaostahili kuonewa huruma na kuliwazwa, kwa kuwa waliingia in this scam out of ignorance.

  Ninachoamini ni kuwa majority ni wale kina mama zetu, dada zetu na wadogo zetu ambao kutokana na kuwa so desparate na maisha, they were easily convenced with fruitful promisses from their mbegu's.

  Cha msingi hapa ni kuwa wanapataje japo punje tu ya pesa zilizookolewa na serikali? Kwa maana sote tunajua kuwa walizuia akaunti za Deci pamoja na zile binafsi za viongozi.

  Sikumbuki sawasawa ilikuwaje uamuzi wa those days on "Women empowering Women scheme" ya kina Madabida and others waathirika walilipwaje.
   
 15. M

  Maktauwo Member

  #15
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajukwaa,
  Nimefuatilia suala la DECi kwa shauku toka kabla halijaanzwa kuandikwa na magazeti na hata baada ya hapo. Ninashawishika kusema kuwa kuna habari nyingi sana tunafichwa juu ya suala hili lote hasa kwenye fedha. Habari zilizopo ni kuwa wanachama wa DECI ni zaidi ya 700,000 na kwa kuwa fedha kama ya kiingilio (isiyorudishwa) ni Shilingi 20,000 kuna Shilingi Bilioni 14 (ambazo ndizo zinazotajwa). Hapa hatutaji mbegu ambayo mimi nafikiri ni fedha nyingi sana na za kutisha kwa sababu ukichukua idadi ya wanachama 700,000 ukazidisha kwa kiasi cha kama 100,000 (kama kiwango kidogo cha wastani cha mbegu) naona kiasi kinatisha (700,000,000,000)!!
  Pili jambo hili halihusishwi na money laundering? Na ninazidi kutishika ninapofikiria jinsi ilivyoweza kufanya kazi muda wote wa zaidi ya miaka miwili bila ujasiri wa kuisimamisha. Na natishika zaidi kufikiria Kenya ilikuwepo kama hii.
  Mnaonaje wanajukwaa?
   
 16. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali haitakuwa na uwezo wa kufanya, cha msingi tuiombe serikali waongoze ugawaji wa pesa zote walizozizuia. Pesa zikimalizika wahusika wafunguliwe mashtaka.

  .......KITU CHA MSINGI HAPA, PESA ZILIZOPO KWENYE AKAUNTI WAGAWIWE WAPANZI.............. Napenda kutoa hoja.
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  thats deep thinking.
  Kuna kitu kinafichwa hapo, na hatujui hizi taarifa zinafichwa kwa faida ya nani???

  Au serikali imeamua kutumia msuli kukopa hela za hawa jamaa??? na kama kesi ikianza kusikilizwa basi wanachama wajue hela zao ndo vile tena kwani zitabidi zitumike kama vielelezo mahakamani na hatujui kesi itachukua muda gani.

  Tuwape pole ila najua wabongo hatujifunzi kwa makosa...
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama munakumbuka haya, niliyoyasema hapo nyuma, sasa tayari viongozi wa DECI watano wamekwisha kufikishwa mahakamani KIsutu. Maelezo zaidi baadaye.
   
 19. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hiyo pesa ya DECI hawa watu hawawezi kuipata. Ukijua jinsi upatu unavyofanya kazi. Hivi hao waliokuwa wakivuna na wanaojisifia kuwa wamenunua magari na kusomesha watoto shule na kujenga nyumba unafikiri hela waliipata wapi? Ni mbegu za hawa wanaolia lia sasa eti warudishiwe mbegu. Hilo halipo.

  Monkey accounting zilizokuwa zinafanyika pale, mipesa inarundikwa tu mahali, huyu akileta zinawekwa, huyu akija na receipt analipwa. Sasa hayo mabilioni mnayopigia mahesabu eti yapo, yametoka wapi? Zilizobaki zitakuwa haziwezi kutosha kuwarudishia mbegu hata nusu ya wapandaji. Mgogoro najua hapa itakuwa ikiwa mbegu itarudishwa utatumia criteria gani kumrudishia mbegu huyu na si yule?

  Pesa iliyopo lazima ni ndogo ukilinganisha na wanaodai. Sababu ni kuwa waliokuwa wameshagawiwa mavuno yao, walikuwa wakigawiwa mbegu za wapandaji ya baadaye. Ndiyo hizo wanazopigania eti zirudishwe. Akiweza kurudishiwa kila mtu hata robo ya kile alichotoa, washukuru. Lakini vinginevyo watu laki saba ukiwagawia bilioni 14 sawa sawa kila mmoja atapata elfu ishirini tu.

  Kwa hiyo hawa watu wajue kile ambacho hawajaambiwa bado. Mbegu zao zilishavunwa na hao waliovuna. Kwa hiyo ikiwa watabahatika watapata asilimia kidogo sana ya hiyo walopanda. POLENI.
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapana bwana kwa kiasi fulani Serikali imesaidia kufa kwa taasisi hiyo maana baada ya habari ile kutoka ndio ukawa wakati mgumu kwa DECI!!
   
Loading...