Ofisi za AG na DPP kuna nini?

Mmm, DPP ni department ndani ya ofisi ya AG?

Binafsi huwa naamini, ukimwacha Rais DPP ndiyo mtu mwingine mwenye mamlaka mikubwa sana ktk nchi hii.
 
Well noted.
 
DPP asiwe bwege, unakuwaje mwendesha mashitaka ikiwa hauna wapelelezi wako?
 
Nyie lawyers mbona mnaongea kama laymen?Ebu shusha vifungu vya katiba mana nafasi zote hizo zimeanzishwa na sheria.
 
kikubwa hapa nikuwaita AG na DPP aongee nao kuondoa zile misunderstanding zao ili mambo yaende vizur kuliko kubaki na msuguano unaorudisha nyuma maendeleo kwa taifa.
 
kikubwa hapa nikuwaita AG na DPP aongee nao kuondoa zile misunderstanding zao ili mambo yaende vizur kuliko kubaki na msuguano unaorudisha nyuma maendeleo kwa taifa.
...Kwa jinsi nilivyofuatilia mjadala hapa, naweza kuhitimisha bisha mashaka kwamba tatizo siyo kwa wawili hawa kuitwa pamoja, kuongea nao au kuwapatanisha, it wont help kwa sababu mzizi wa tatizo ni muundo wenyewe kama ambavyo tumeonyeshwa hapa kwenye hiyo structure. Suluhu ya kudumu ni kwa vyeo hivyo viwili kutenganishwa na kila mtu awe na ofisi yake inayojitegemea, na hata uteuzi wao uwe kwa competence na kupitishwa na bunge.
 

...Aisee what a pierce of information!...Many thanks mkuu.
Sasa mtihani ninaouona hapa ni who should initiate the move to separate the two and form two independent offices? Unajua tokea jana (na ndiyo maana nikaleta huu uzi) nimetafakari sana kwa nini Mhe rais pamoja na kuliweka hili jambo hadharani, na akasisitiza ''kila mtu anajua kuwa hawa watu hawaelewani!! hata Waziri unajua!! sikuona akiweka hitimisho la kudumu juu ya suala hili (zaidi ya kusema kaeni mlimalize). Nilitegemea angesema kuanzia leo....au naanzisha mchakato wa kutenganisha ofisi hizi etc.
On the other hand nilidhani maybe tatizo ni between the two due to their personal issues, lakini nimejifunza hapa kwamba it is more related to the structure of the two posts.
 
...Very well said. Sasa mkuu ikiwa katiba inawatambua kama watu 2 tofauti why mmoja akamtia kwapani mwenzake? Kwa nini AG alivyojinasua toka wizara ya katiba na sheria hawakufikiria kuwa na two separate offices? (ya AG na DPP i mean).
 
...Very well said. Sasa mkuu ikiwa katiba inawatambua kama watu 2 tofauti why mmoja akamtia kwapani mwenzake? Kwa nini AG alivyojinasua toka wizara ya katiba na sheria hawakufikiria kuwa na two separate offices? (ya AG na DPP i mean).
nadhani uliiona ile organisation structure ya ofisi ya AG niliyoiweka hapo awali ambayo inaonesha kuna DIRECTORATE OF PUBLIC PROSECUTION ndani yake suala gumu siyo structure bali suala gumu ni kwamba hawa wote wanapatikana kwa kuteuliwa na raisi huku ikitegemewa kuwa(kwa mujibu wa organisation structure) DPP awe chini ya AG wakati wote wapo kwenye level moja hapo ni sawa na kuchukua watoto waliozaliwa siku moja wakati mmoja halafu unalazimisha mmoja amwite mwenzie kaka

Busara hapa ni kuzitenganisha hizi office yaanai kuanzisha ofisi ya CHIEF PUBLIC PROSECUTOR lakini ni kweli usiopingika kwamba baadhi ya nchi public prosecution inafanywa na ATTORNEY GENERAL hivo mi nashauri busara itumike kwenye kuhandle hili swala. hawa watu watenganishwe tu kwa sababu wananchi tunataka matokeo mazuri ya utendaji wa serikali na sio kushuhudia bra bra zao
 
Birds of the same feather, fly 2gether! Ndio wale wale Villains; yule mama mjane kawaanika kisawasawa!

Ndugu ungeomba uelezewe ni wapi ulipokosea katika point yako..ila katika kukusaidia ofisi ya DPP ipo chini ya ofisi ya AG.hao mawakili wa serikali ambao unasema ndiyo wanaongoza kesi badala ya mapolisi wapo kwa AG na wengine wapo kwa DPP lakini wote kwa ujumla bosi wao ni AG. DPP ni cheo ambacho ni department ndani ya AG.Kabla hujaandika ni vema kufanya research kwanza na unapokosolewa na mtu mmoja ni vema ujihakikishe kwanza kuliko kuendelea kuongea.utaoneka mweupe juu.
 
Mimi nimeliona kosa langu baada ya mwana JF mwenye akili kuweka hapa Organogram ya ofisi ya AG, Tatizo lenu wengine woote mliokuwa mnanikosoa ukiwemo wewe mlikuwa mnaadress kosa minor mnaacha hoja ya msingi ya mleta mada kuhusu chanzo cha kusigana baina ya vigogo hao AG na DPP, mnaishia kusema sijui ninachosema lakini hamsemi kilicho sahihi! Hata wewe sasa hivi hujajibu hoja hiyo ya msingi! Funguka vinginevyo hata wewe tutakuona Mweupeee peee!
 
Wewe inaonekana hujui DPP sio polisi. Elewa kuwa DPP ni sehemu ya idara ndani ya AG, ila ktk idara kadhaa ndani ya AG ni DPP pekee ndio anateuliwa na rais. Vita iliyopo nadhani ni hiyo kuwa wote ni wateule wa rais nani atamwajibisha mwenzie. Kingine nilisikia ni kuwa DPP hataki kuwa chini ya AG bali awe idara huru. Yaani ni balaa ya kutaka full power
 
Kipindi cha DPP FELESHI AG alikuwa Werema na sio Masaju. Masaju alishika kwa kipindi kifupi baada ya Werema kujiuzuru kwa ESCROW. Hivyo kipindi kitefu cha mgogoro AG alikuwa Werema na DPP Feleshi
 
hao wawili wana matitizo yao personal wala hayana uhusiano na kazi,
 
...Very well said. Sasa mkuu ikiwa katiba inawatambua kama watu 2 tofauti why mmoja akamtia kwapani mwenzake? Kwa nini AG alivyojinasua toka wizara ya katiba na sheria hawakufikiria kuwa na two separate offices? (ya AG na DPP i mean).
hahaha, hicho kitu ukiongea mbele ya AG kama siku hiyo hajaamka vizuri anaweza kukurushia makonde (kidding). Kati ya sababu kubwa ya ugomvi ni DPP kuweka mapendekezo kuwa ajitenge iwe ofisi inayojitegemea, na ndilo bifu lililomsumbua sana Feleshi. AG anataka dpp awe chini yake na kwa vile ni mwajiriwa wake ndio anataka aendelee kuwa chini yake. kwa uzoefu ninavyoangalia nchi zingine, ofisi ya DPP inajitegemea. Pamoja maneno yoote waliyomsema Feleshi, wakitaka tatizo hili litatuliwe once and for all, wamwite Feleshi awape ushauri kwasababu yeye ndiye alipata shida sana na hiyo ofisi ya boss wake AG, na Feleshi alijitahidi sana kupambana ijitenge iwe kama ilivyo nchi zingine ili ufanisi uwepo, lakini alipoondoka tu, yote aliyokuwa ameimarisha feleshi yamenyang'anywa kwa Mganga na yamerudishwa kwa AG. ofisi hiyo kufanya bila kuwa independent ni ngumu sana. ndugu zetu wanafanya kazi hapo, tangu Feleshi aondoke hapo kwa dpp, kila kitu kimelala na yamebaki mapambano tu ya mamlaka, na anayeonewa ni DPP. AG awe na ofisi yake na DPP awe na ofisi yake kama kitengo ndio ataweza kutoa maamuzi kwa uhuru na ufanisi, kama sivyo hivyo, tutaendelea kuona yanayoendelea.
 
Unafahamu Vizuri Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu? Bila shaka usingeandika hivi. Nashauri ufanye utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…