Ofisi ya usalama yashambuliwa Mogadishu

Ofisi ya usalama yashambuliwa Mogadishu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
140831101633_somali_government_soldiers_patrol_during_clashes_between_them_and_militiamen_loyal_to_a_somali_warlord_in_mogadishu_304x171_ap_nocredit.jpg



Shambulio dhidi ya makao makuu ya idara ya usalama ya Somalia mjini Mogadishu limeuwa watu 10.

Wakuu walisema saba kati ya hao ni wapiganaji wa al-Shabaab ambao waliingiza kwa nguvu gari lilojaa mabomu katika uwa wa jengo hilo ambalo lina ulinzi mkali.

Tena washambuliaji walijaribu kuingia ndani ya jengo.

Al-Shabaab ilisema ilifanikiwa kuwaachilia huru wafungwa wengi katika makao makuu hayo, ambayo yana gereza chini kwenye handaki na pahala pa kuhoji wafungwa.


CHANZO: BBC
 
Maafisa wa serikali ya Somalia wamesema wanamgambo wa kiislamu wamekivamia kituo cha ujasusi jana mjini Mogadishu na kuua watu 11.
 
Aisee! Kama vile series ya Alias vile!
Nalog off
 
Back
Top Bottom