Ofisi ya taifa ya takwimu(NBS) yaitaka kampuni ya Geopoll kufuata taratibu zilizoainishwa katika sheria ya takwimu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Ofisi ya Taifa ya Takwimu(TBS) imeitaka Kampuni ya Geopoll yenye ofisi zake za Ukanda wa Afrika Mashariki, Nairobi nchini Kenya imewataka kufuata taratibu zilizoainishwa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu.

tak.jpeg
 
Sasa kama wao wanakidhi vigezo watoe wao basi, sisi tunataka data, kwani TBS inawapa hela au wanajitolea
 
Nilitaka kushangaa eti Tbc ipo tatu bora, ni kitu ambacho hata kwa kufikiria hakiwezekani
 
Siku hizi Kupata data sio lazima uzunguke na makaratasi kama mwendawazimu, huo uwendawazimu mmeachiwa nyie TBS. Siku hizi tuko kwenye dunia ya digitali makaratasi ni kupitwa na wakati. Tulieni tuli muonyeshwe data zinavyokusanywa ndani ya sekunde nyie bakini na kuwatuma kina maimuna kuzunguka mtaani na makaratasi na kalamu za BIG
 
Published on 7 Aug 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

Ofisi ya Takwimu waukataa utafiti wa Geopoll Kenya kuhusu vyombo vya habari

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania National Bureau of Statistics | Statistics for Development imekanusha takwimu zinazotolewa na kampuni ya GeoPoll yenye makao yake kikanda jijini Nairobi, Kenya ambazo hutolewa kwa njia ya mitandao ya kijamii kila baada ya miezi mitatu juu ya vyombo vya habari Tanzania, kwa kusema kuwa takwimu hizo sio rasmi na hazina viwango http://knowledge.geopoll.com/tanzania-media-measurement-kgmm-report-0-0 . Na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Tanzania Dr. Alibina Chuwa ametoa angalizo na taadhari kali kwa GeoPoll kuacha kujiweka katika nafasi kama wawakilishi wa takwimu rasmi za Tanzania.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema taarifa za GeoPoll hazitambuliwi na serikali ya Tanzania na pia watumiaji wa takwimu hizo za GeoPoll GeoPoll Mobile Survey Research Blog | Tanzania watambue kuwa takwimu hizo ni batili na wala hazina viwango vya kimataifa ili kuweza kulinganisha nchi na nchi.

Mfano utafiti wa hali ya umasikini nchi nzima ya Tanzania pamoja na kutumia teknolijia unagharimu shilingi za Tanzania Bilioni 10 na usipo tumia teknolojia gharama inapanda mpaka Bilioni Tshs. 20. Lakini GeoPoll ya Kenya wanafanya utafiti wao kienyeji kwa kutumia rejea za administrative records yaani'' takwimu za utawala'' GeoPoll - Understand the world , lakini GeoPoll ikitaka kupata takwimu sahihi inabidi kuja Ofisi ya Takwimu ya Taifa Tanzania kupata taarifa sahihi.

Source: Millard Ayo
 
Yan kweli eti Clouds inaongoza? wapi na wapi TV ya wavaa vyupi na watu waliokaa uchi kuongoza kwa utazamaji? television pekee yenye mwenendo wa kiueledi ni ITV ikifatiwa na Azam 2
 
Naona kuna jambo nyuma ya kauli hii ya Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania maana hili la kutetea tu media za Tanzania lazima kuna ripoti zingine kama za ''Umasikini'' , ''Njaa'' n.k lakini taarifa hii kwa umma juu ya utafiti wa ''vyombo vya media Tanzania'' imetumiwa tu kufikisha ujumbe kwa wale wanaotoa takwimu za ku- ''abuse nchi'' kuhusu masuala yaliyogusa awamu ya tano ziwe za ukweli au za kupikwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Kasome sheria ya takwimu iliyo fanyiwa marekebisho 2015 utaelewa ni wapi Geopoll walikosea....si kila mtu ana ruhusiwa kutoa takwimu bali kuna taratibu zake.....
 
Back
Top Bottom