Elections 2010 Ofisi ya Msajili wa vyama ivunjwe

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Moja ya kazi za Ofisi ya Msajili wa vyama ni kusajili, kusaidia na kuvilea vyama vya siasa. Lakini kadri siku zinavyokwenda inaonekana Ofisi ya Msajili wa vyama imekuwa kama adui wa vyama vya siasa, badala ya kuwa rafiki na mlezi, lengo lake limebaki kuangali chama gani kifutwe si chama gani kisaidiwe.

Juzi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa Msajili wa vyama nchini Tendwa ameshindwa kusambaza kwenye vituo fomu za gharama ya uchaguzi kama anavyotakiwa na badala yake akazipeleka kwenye ofisi za vyama mbalimbali.

Nilitegemea Tendwa kukiri kuwa amefanya kosa kwa kuchelewa kugawa fomu hizo badala yake anatoa vitisho kwa wagombea watakaochelewa kurudisha fomu. Angekuwa kweli ni mlezi angeliangalia ni wagombea gani wanahitaji msaada badala yake yeye na ofisi yake wanasubiri kuona ni wagombea gani hawata jaza fomu vizuri wawawekee pingamizi. Incredible.

Kuna mifano mingi tu naweza kuonyesha ni jinsi gani Ofisi hii imeshindwa kukidhi matakwa ya wadau wake wakuu ambao ni vyama vya siasa. Chukulia mfano wa chama kilichokosa usajili wakudumu cha CCJ, ndio hatukatai kuna makosa ya chama, lakini, Tendwa au Ofisi yake ilitakiwa ikisaidie na kukipa mwongozo pale kilipokosea badala ya kukikejeri kwenye vyombo vya habari kuwa ni Hoax.

Ningekuwa mimi natawala ningefutilia mbali Ofisi ya Msajili wa vyama na kuipeleka NEC iwe kama kitengo cha NEC, maana kuna muingiliano wa maslahi kati ya NEC na Ofisi ya Msajili.

Kama Tendwa na Ofisi yake wanajitoa ulezi wa vyama kazi yake itakuwa nini basi endapo hakutakuwa na chama kipya kingine. Kitengo hiki ni matumizi mabaya ya pesa za serikali ningeshauri kivunjwe au kiunganishwe na NEC Taifa.
 
Back
Top Bottom