Ofisi ya CHADEMA kanda ya Serengeti iliyopo Shinyanga Mjini yanusurika kuchomwa moto

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
4,344
6,403
IMG_0542.jpeg

Ofisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara zilizopo Mjini Shinyanga imenusurika kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 25,2020.

Taarifa ya Ofisi ya CHADEMA kunusurika kuchomwa imetolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami leo Jumapili Oktoba 25,2020 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Shinyanga.

“Leo majira ya saa saba usiku ofisi yetu ya Kanda ya Serengeti imenusurika shambulio la kuchomwa moto. Tulipewa taarifa na walinzi wetu kwamba kioo cha dirisha la ofisi ya Katibu kimevunjwa,na baadaye tumejaribu kuangalia labda ni vibaka walitaka kuiba lakini tulivyoingia ndani tukakutana na hali ambayo inaonesha kulikuwa na watu wenye nia ovu ya kulipua kwa petroli. Tumekuta chupa yenye mafuta ya petroli kiasi cha lita moja na nusu na utambi ndani na ukiwa umeunguzwa kidogo ikionesha kwamba huyo mtu alikuwa amewasha moto na bahati nzuri moto huo haukuwaka”,ameeleza Mnyawami.

Aidha Mnyawami amelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha na kwamba wameliachia jeshi la polisi kuendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo.

“Kwa kweli kwa tukio hili la uchomaji Tunalishukuru sana jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano wa kutosha waliotupatia. Mtu wa kwanza kufika hapa baada ya sisi kutoa taarifa polisi ni OCD pamoja na askari wake , tunawashukuru sana. Lakini pia nimshukuru Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga amefika eneo la tukio kujionea hali halisi. Polisi wametoa ushirikiano mzuri na mambo mengine ya Kiupelelezi tumewaachia wao”,amesema Mnyawami.

Mytake
Sina shaka ni katika mbinu za kuwaondoa kwenye mikakati ya kutafuta ushindi, kwenye uchaguzi ujao!
 
Ofisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara zilizopo Mjini Shinyanga imenusurika kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 25,2020
Chama cha Mapinduzi kimegeuzwa kuwa Chama cha kihuni ndani ya miaka mitano tu.
 
Chadema ni watu wa vurugu na uongo

Kiofisi utafikiri gest bubu
Pamoja na mwonekano wa ofisi je,hujaona yanayoratibiwa na ofisi unazozitusi kila uchao.Hizo ndio zina kukimbiza mchakamchaka Hadi unavurugigiwa.
Mnatengeneza matukio kama la Arusha. Mnatuaibisha sana sisi wanaCdm wastaarabu.
Kwani uchovu bado upo tuu ndugu yangu,nakushauri upumzike vya kutosha uweze kwenda kupiga kura kesho kutwa, usipitiwe uasingizi
 
Huyu lissu ndio akimbize Ccm mchaka mchaka ?

Mmeanza siasa mwaka huu bila shaka
Pamoja na mwonekano wa ofisi je,hujaona yanayoratibiwa na ofisi unazozitusi kila uchao.Hizo ndio zina kukimbiza mchakamchaka Hadi unavurugigiwa.
Kwani uchovu bado upo tuu ndugu yangu,nakushauri upumzike vya kutosha uweze kwenda kupiga kura kesho kutwa, usipitiwe uasingizi
 
Kufika wanaweza kufika tu na habari ikaishia hapo.
Kawaida mnafiki ni zaidi hata ya mchawi,kwani lazima aonyeshe yupo pamoja nawe ilhali yupo na nia ovu juu yako,hayo sii ya kuyashaangaa kwa tulipofikia.Ila mwisho wao uukaribu Sana 28Oct.2020.Twende na mwendo wa haki wa umoja wetu kama Tanzania.
 
Unashangaa nn?? Mlimdanganya jpm ati chadema ingelufa by 2020 lkn umeshuhudia kaka yenu alojiita ati yeye ni jiwe kwelikweli akipiga magoti kuomba pooo.

Husicheze na lissu we ngedere madoa
Huyu lissu ndio akimbize Ccm mchaka mchaka ?

Mmeanza siasa mwaka huu bila shaka
 
View attachment 1611503
Ofisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara zilizopo Mjini Shinyanga imenusurika kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 25,2020.

Taarifa ya Ofisi ya CHADEMA kunusurika kuchomwa imetolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami leo Jumapili Oktoba 25,2020 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Shinyanga.

“Leo majira ya saa saba usiku ofisi yetu ya Kanda ya Serengeti imenusurika shambulio la kuchomwa moto. Tulipewa taarifa na walinzi wetu kwamba kioo cha dirisha la ofisi ya Katibu kimevunjwa,na baadaye tumejaribu kuangalia labda ni vibaka walitaka kuiba lakini tulivyoingia ndani tukakutana na hali ambayo inaonesha kulikuwa na watu wenye nia ovu ya kulipua kwa petroli. Tumekuta chupa yenye mafuta ya petroli kiasi cha lita moja na nusu na utambi ndani na ukiwa umeunguzwa kidogo ikionesha kwamba huyo mtu alikuwa amewasha moto na bahati nzuri moto huo haukuwaka”,ameeleza Mnyawami.

Aidha Mnyawami amelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha na kwamba wameliachia jeshi la polisi kuendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo.

“Kwa kweli kwa tukio hili la uchomaji Tunalishukuru sana jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano wa kutosha waliotupatia. Mtu wa kwanza kufika hapa baada ya sisi kutoa taarifa polisi ni OCD pamoja na askari wake , tunawashukuru sana. Lakini pia nimshukuru Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga amefika eneo la tukio kujionea hali halisi. Polisi wametoa ushirikiano mzuri na mambo mengine ya Kiupelelezi tumewaachia wao”,amesema Mnyawami.

Mytake
Sina shaka ni katika mbinu za kuwaondoa kwenye mikakati ya kutafuta ushindi, kwenye uchaguzi ujao!
Asante kwa kutujuza. CDM tutawashinda CCM hata kwenye mitaro, hakuna wasiwasi.
 
Back
Top Bottom