Removers
Member
- Nov 1, 2018
- 71
- 39
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Tanzania imeshinda tuzo ya Kimataifa ya Ripoti Bora zaidi ya Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019 kwa ukanda wa nchi za Afrika zenye Taasisi za Udhibiti na Ukaguzi zinazotumia Lugha ya Kiingereza (AFROSAI-E region).
Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo inayofadhiliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Sweden, inasema kuwa ‘’tuna furaha ya kutangaza kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Tanzania ndiyo mshindi Tuzo ya Ripoti Bora zaidi ya Ukaguzi wa Hesabu kwa mwaka 2019 katika ukanda wa AFROSAI-E.
Hii ni mara ya nne kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Tanzania kushinda tuzo hii tangu ilipoanzishwa mwaka 2008 na Ofisi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Sweden.
Ripoti hiyo yenye jina ‘’Management of Water Projects in Rural Areas’’ imejikita kuangalia sekta ambayo ina uhusiano wa karibu na afya ya jamii, hivyo imeangazia zaidi mtazamo wa wananchi, inasema taarifa hiyo.
Timu huru ya Kimataifa ya Mapitio iliamua kwa kauli moja kuhusu ripoti iliyoshinda, na nchi ambazo ripoti zake zilikuwa nzuri, zenye ubora na zimebuniwa na kutengenezwa vizuri. Inahusisha mnyororo mzima wa uwajibikaji kuanzia katika ngazi ya wilaya hadi ngazi za chini za utawala. Ripoti ya Tanzania iliwasilisha mahitimisho na mapendekezo ambayo ni ya kichambuzi na yanaongeza thamani na yametokana na msingi wa masuala yaliyoibuliwa.
Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania, Bw. Charles Kachere amesema kuwa amefurahishwa sana kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Ofisi yake. ‘’Nina furaha sana kupokea tuzo hii kwa niaba ya ofisi yangu, na ninajivunia na timu nzima iliyoandaa ripoti iliyoshinda tuzo. Vilevile, ningependa kushukuru Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali wa Sweden kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kipindi kirefu, ambayo imechangia kwenye kujengea uwezo wa ukaguzi kwa Ofisi ya Taifa ya Udhibiti na Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Tanzania’’.
Jumla ya ripoti 10 ziliwasilishwa kutoka of Ethiopia, Ghana, Seychelles, Sierra Leone, South Africa, Sudan, na Tanzania kwa mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa AFROSAI-E, Meisie Nkau amepongeza Ofisi ya CAG Tanzania kwa ubora wa ripoti yake. Akizungumza wakati wakati wa kutangazwa kwa mshindi amesema kuwa ‘’Nina furaha kubwa kuwapongeza Ofisi ya Tanzania kwa mafanikio haya. Mmefanikiwa kwa mara nyingine! Pia ningependa kushukuru kwa mataifa yote kwa kuendelea kushiriki kwa kuwasilisha ripoti bora’’.