Ofisi ya Bunge yakanusha ongezeko la Posho

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
41774_100001490228404_276_n.jpg


TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya wabunge kuwa posho ya vikao vya bunge imeongezeka kutoka Sh 70,000/= hadi kufikia 200,000/=.

Suala la mabadiliko la bosho za vikao vya bunge lilijadiliwa katika mkutano wa wabunge November 08, 2011 walipoiomba serikali iangalie upya suala hili ili kuboresha. Hadi tunapotoa taarifa hii serikali haijatoa taarifa kama posho hizo zimeongezeka kutoka kiwango cha awali na kufikia laki mbili.

Tunasikitika na kushangaa sana kwa kauli hii kwani inajenga chuki baina ya wabunge na wananchi waliowapigia kura.

Posho inayotolewa kwa sasa ni ile iliyoainishwa kwenye waraka wa Rais wa October 25, 2010 ambayo iliridhia posho ya vikao kuwa 70,000/=

Kwa hiyo taarifa iliyotolewa siyo sahihi.

Imetolewa na
Dr. Thomas D. Kahililah
Katibu wa Bunge


Bofya link ya kijani hapo chini habari hii ilivyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi kupata mengi zaidi.

Bunge latoa tamko nyongeza ya posho
 
(habari hii nimeifupisha kwa vile nimeisoma toka kwenye taarifa yake ambapo sikuwa na nafasi nzuri ya kutoa rudufu yake kuiweka hapa)
Asante CS! Sasa tunaomba vyombo vya habari vitwambie vilipata wapi hizi habari! Kuna watu wengi wametoa maoni!wengine wameng'aka na kufoka kumbe habari zenyewe uhongo!ngoja tuone vyombo vya habari watatwambia nini!
 
Tuna kila sababu kua na mashaka na kauli hii ya bunge kwa sababu nyingi, habari hizi zilitoka zaidi ya siku kumi zilizopita kwanini hazikukanushwa mara moja habari hizi. Au nazo zilikua zinahitaji tume?

Hapa naweza kusema ya kua serikali na CCM walikuwa wameamua kupandindisha viwango hivyo kimya kimya wakifikiri ya kua hazitavuja baada ya kuvuja na reactions ya wananchi na wadau mbalimbali wakaamua kubadili kibao au kauli. Vitendo ambavyo ni kawaida kwa chama tawala na serikali yake.

Mungu ibariki Tanzania
 
How long it takes kwa bunge kujua posho imeongezwa au la? Habari za kuongezeka kwa posho ni kama 'zilipendwa' huyu Dr Kashilila alikuwa wapi?
Lakini huyu Dr Kashilila amejijengea sifa kubwa sana ya kuwa mwepesi kugundua wabunge 'ma-mbumbumbu' (maneno yake) wasiojuwa taratibu za kibunge, kutoa maelezo na hata kulumbana na wabunge kuhusu mijadala/miswada inayojadaliwa bungeni. Sote tunakumbuka aliyojitekeza mbele ya vyombo vya habari kuhusu muswada wa katiba. Sasa imekuwaje kwenye hili la posho amechukuwa zaidi ya week nzima kutoa majibu?

omething is very wrong here, na nahisi kuna ajenda ya siri ya ku-reward wabunge wa CCM na washirika wao ili waendelee kuwasaliti wananchi kwa manufaa ya wachache. Dr Kashilila anatakiwa atoe maelezo yenye kichwa na miguu. Kuna mbunge yoyote anaweza kutuambia bank statement yake ina-figure gani kwenye posho hasa mwezi mmoja uliopita? Na ikigundulika amedanganya basi huyu Dr Kashilila aondelewe kwenye hiyo nafasi
 
Asante CS! Sasa tunaomba vyombo vya habari vitwambie vilipata wapi hizi habari! Kuna watu wengi wametoa maoni!wengine wameng'aka na kufoka kumbe habari zenyewe uhongo!ngoja tuone vyombo vya habari watatwambia nini!

Ukiisoma vizuri habari hii kuna kitu kinazungukwa na ukweli kwamba vyombo vya habari vimeandika ukweli wa kilichojilia bungeni wakati bungeni wawakilishi wa wananchi waliridhia posho za vikao hivyo ziongezwe.

Bunge limekubali kwamba katika kikao cha bunge kilichopita waliomba serikali kuangalia upya posho za wabunge kwa maana ya kufanya uboreshaji kwa kuongeza kiwango chake. Nakumbuka Speaker Makinda alisema atachukua hatua stahiki baada ya wabunge kujadili jambo hilo. Wengi hatukuelekeza akili na masikio Dodoma wakati huo kutokana na kuelekea Arusha kwenye maandamano ya Chadema yaliyoleta purukushani pale uwanja wenye historia ya mageuzi ya kisiasa nchini.

Cha msingi serikali bado kuridhia, isipokuwa ukweli ungali pale pale kwamba wabunge wameomba kuongezewa posho za vikao kwa maana kwamba hawaridhishwi na posho za vikao wanazopata za sasa.
 
Nimeamini kuna media ambazo zinatumiwa na chadema kuipaka matope serikali.
 
Naanza kupata wasiwasi na Gazeti la Mwananchi, limekua sehemu ya udaku
 
Kashilila
kama u0ngo mtavifanyaje vy0mbo vya hbr?

kaka soma hii habari vizuri huku ukiitafakari vizuri hiyo habari, hiko so fishing. wanahabari kazi yao ni kuripoti tu kinachozungumzwa
na pia kuchokoza pia ni moja ya kazi zao. imewachukua muda mrefu sana kukanusha habari hii pia huyu kashilaha alishaulizwa before kuhusiana na issue hii akasema yeye sio msemaji wa bunge kwahiyo kesi hii bado haijafungwa.
 
Nchi hii haina watendaji walio serious kuiendeleza. Na kama wapo wanavunjwa moyo na kundi kubwa ndani ya serikali linaloshikilia nafasi mhimu kimagumashi bila kuwa na sifa, uadilifu pamoja na kujua kile wanachotakiwa kukifanya kwenye nafasi zao. Kama Katibu wa bunge yuko miaka 20 iliyopita, unategemea tutafika lini karne ya 21?

I am scared with this shit! watu wamepoteza muda wao kujadili inshu ya posho, wajue kabisa leo hii watu wanakila acess to information na kurespond mara moja, inapotokea kitu kinachohusu taasisi fulani nyeti kama bunge inaathiri shughuli nyingi, na hivyo ni mhimu kujibiwa haraka ili kutuliza joto na kuepuka hasara inayopatikana kutokna na watu kutofanya kwa 100% efficient.
 
Oooo Ghosh!!!!!!!!!!!!!!!!! nilipanga kikao cha january niongeze nyumba ndogo nyingine,
but mr. Kashililah can you came again on this important issue imetustua sana sisi wabunge, presha inapanda presha inashuka.
 
hata 70,000 wanayolipa haistahili. Ukiwa mbunge maana yake uhudhurie vikao vya bunge. Ndo kazi yako. Sasa kwa nini ulipwe?
 
Namwamini sana ZITTO asingesema uongo Bunge limekuwa na tabia ya kukanusha mambo mengi hata ya ukweli ngoja tuwa ulize wabunge wenyewe waseme
 
Back
Top Bottom