Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Alipotangaza alikuwa amemaliza Ni mweshimiwa makamba tu kama kawaida yake inawezekana alikuwa hajasoma katiba ya CCM ili atoe taarifa bungeni.
Huyu Mbunge inaonekana alitangaza kujiuzulu kwake kwa vyombo vya habari,
hajakiankikia barua chama chake na Ofisi ya Bunge ndio kwa maana Bunge bado
linamtambua kuwa ni Mbunge. Clever Guy!!!!!
Katiba ya CCM inasema mtu akijiunga na chama kingine anapoteza unachama. Mpendazoe kajiunga na chama kingine bado mnataka na aandike barua ya kuwaaga? Aweke na terehe?
Kwa upande wake Katibu wa Kamati Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilgati alisema suala hilo haliwahusu wao kwa kuwa, Mpendazoe aliwambia kwa heri na wao wakamwambia asante.
"Hilo ni suala lake binafsi na mamlaka ya bunge, sisi hatujamfukuza ila yeye ndiye alituaga na sisi tukamwambia asante, hatuna ugomvi na wewe," alisema Chiligati.
"Kama tungemfukuza uanachama sisi ndio tungelazimika kuiandikia ofisi ya bunge kuwa huyu si mwanachama wetu tena, lakini kwa vile yeye mwenyewe ndiye amehama chama, suala hilo ni la kwake na mamlaka ya bunge watajua namna ya kulimaliza," aliongeza Chiligati.
Mimi nawatakia kila la kheri wanaona Mpendazoe alivyofanya ni sahihi, lakini msimamo wangu ni kwamba alikurupuka kama alivyokurupuka Augustion Lyatonga Mrema.
Na historia hiyo haitafutika daima...
Hayuko makini period.
Ni kuwa bunge linamtambua kwa sababu hajapeleka taarifa za kimaandishi, kwa hiyo hakuna jambo la ajabu hapo.
Mzee Mwanakijiji,
Kuna njia mbili za kuisha kwa ubunge wa Mpendazoe:
1: Yeye mwenyewe kulijulisha bunge kwa maandishi kuhusu kujiuzulu kwake kwasababu amehama CCM
2. CCM kulijulisha bunge kwamba Mpendazoe sio mwanachama wao tena
Mpendazoe ndiye katangazia umma kuhama chama na kuachia ubunge; anashindwa nini kuliambia bunge? CCM hawajamfukuza, hivyo hawana haraka ya kujadili kuhusu kujiuzulu kwake.
Jibu: Hapana.
Mzee Mwanakijiji, post zako zote za katiba ziko right!!! Tatizo hapa ni umakini tu wa Shujaa Mpendazoe katika ku-execute hayo anayosema... ni vyema tuendelee kumshangilia ili aendelee kuona alichofanya ni sahihi... Lakini moyoni mwake anapata shida sana... angekuwa shujaa barua kwanza kwa Bunge then Shinyanga kwa Wapiga Kura wake... then habari maelezo.
Hata hivyo tunamtakia kila la kheri lakini lets wait and see, yuko wapi Mrema, yupo wapi Njelu Kasaka.
mpaka sasa watoto wachache wameshaona kwamba mfalme hajavaa nguo muda si muda mtoto atapiga makelele kwa umati unaomshangilia mfalme ambaye hajavaa nguo.
Hapana.. Ziko njia zaidi ya moja ya kupoteza ubunge wake katika mjadala huu amefanya hivyo kwa kupoteza uanachama wa chama chake cha siasa. Amepoteza uanachama wa CCM siyo alipotangaza hadharani bali pale alipoamua kujiunga na chama kingine. Ukiondoa njia hiyo nyingine ni kufukuzwa, kuvunja masharti ya katiba na hata kufa.
Hakuna mahali popote kwenye Katiba panaposema Mbunge anapoteza Ubunge kwa kulijulisha Bunge!
Hiyo ni kutoa taarifa tu; atakuwa ameshapoteza ubunge kwa kujiunga na chama kingine.
Kama Mpendazoe kashatangaza kuwa ameacha CCM na tayari amejiunga na chama kingine, kwanini awaandikie na barua ya kuwajulisha wakati jukumu hilo ni la chama kilichompoteza. Vinginevyo Mpendazoe hatowaambia na watamlipa kwa muda ule na anaweza akatokea siku moja moja Bungeni kukusanya posho.. CCM ndio wanatakiwa kutoa taarifa kwa Bunge kuwa Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wao kajiunga na chama kingine na hivyo siyo mwanachama wao tena.
Ni sawa na ndoa, wewe umeamua kumwacha bwana, badala ya kwenda kuomba talaka, unataka bwanako ndiye akaombe. Akiamua na yeye kukaa kimya, hiyo ndoa haijavunjwa.
Uamuzi wake ni wa kishujaa kwa kuwa aliamua kukacha mahela yote hayo ili kupigania ustawi wa demokrasia.Kosa lake alikurupuka, angetafuta walau mwanasheria mmoja akamuuliza nini hatima ya kujitoa CCM na mustakbali wa ubunge wake, basi angengoja.
Milioni 45 si mchezo kuzikosa, na ubunge ndio keshaukosa maisha yake.
Ndo manake best hapa si kwamba tunajadili watu tu bali kila kitu. Tunajadilili bila kificho. Kimsingi huwezi kuongelea maisha na maendeleo yoyote bila WATU. So dude unless it's a forum people must and should be discussed!wabongo bwana.....mnapenda kweli thread za kujadili watu