Ofisa Habari wa CHADEMA aandaa press ya Kuivuruga ACT

Ofisa Habari wa CHADEMA aandaa press ya Kuivuruga ACT

poor ACt kilianzishwa kuimaliza chadema, sasa Leo wanalia eti chadema ndio inawamaliza!
kajipangeni upya nyie wasaka tonge.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo(chadema),kimetuhumiwakusuka mkakati wa kukuvutia chama cha ACT-Tanzania kwa kutumia baadhi ya wanachama wa chama hicho.

Taarifa ambazo zimelifikia gazeti hili Dar-es-salaam jana,mmoja wa viongozi wa chama hicho,alisema kuwa wanahisi chadema wanacheza mchezo mchafu wa kuhakikisha ACT-Tanzania inaingia kwenye mgogoro.

Chanzo hicho (jina tunalo),kilisema kwa hali ilivyo kuna kila dalili ya Chadema kuhusika ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano uliofanywa juzi na baadhi ya wanachama wa ACT-Tanzania ambao wanajitambulisha kwenye vyombo vya habari kama waasisi wa chama hicho.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa taarifa waliyonayo ni kwamba mmoja wa maofisa wa habari wa chadema,ndiyo alihusika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa vinatakiwa kwenda kwenye mkutano huo wakiamini baada ya habari kutoka watakuwa wamefanikiwa kutimiza malengo yao.

Hata hivyo,chanzo hicho hakikuwa tayari kutaji jina la ofisa anayetuhumiwa kuhusika katika mkakati wa kuichafua ACT-Tanzania.
Alipotafutwa kwa njia ya simu, ofisa habari wa chadema, Tumaini Makene ili kuzungumzia tuhuma hizo, alisema hawezi kuzizungumzia maana yupo mkoani ambapo alitaka kufahamu ni nani alitoa madai hayo.
Chanzo: Gazeti la Jambo Leo tarehe 13/11/2014.

Mbona ni mapema sana ACT kuanza hizi ?
 
Kama mtu alifanya usaliti,popote aendako hawezi kuacha usaliti na haaminiki wakati wote
 
Ni sawa katika hali yoyote ACT ife tena ife kabisa. Walifanya upumbavu sana baada ya usajili. Badala ya kufanya kazi kama chama cha upinzani, wao waliamua kupambana na Chadema. Kwa hali yoyote kama Chadema wanaisambaratisha Act mimi naungana nao kwa 100% kufa Act utakutana na Ccm moto wa milele
 
Umenipotezea muda wangu buure , kumbe ni habari za jambo leo !
 
Wamevurugikiwa kwa kuwa aliewashikia akili yuko busy na ESCROW hana habari na hilo genge la mazuzu, watachaje kuvurugikiwa?
 
Mwigamba na kitila kwa nini usaliti mliojaribu kuufanya cdm mnataka kuuhamishia act baada ya kukaribishwa na 'waasisi'?
 
yaan watu ni mapunguani sana! eti chadema inaivuruga ACT? Kwanza Act ni nini? ivurugwe ili iweje? wasitafute mtu wa kufa naye! chama chenyewe hakina wanachama!

Kama hamna sera mnaweza kukifuta hicho chama chenu.
 
Hawa wasaliti nia yao kurudidha harakati za ukombozi nyuma kwa faida yao wenyewe. Wananisikitisha sana. Tunaungana kuing'o a ccm wao wanatuvuta mashati kurudi nyuma. Hivi mnata ccm iendeleee kutawala ktk hali hii kweli!
 
ACT-T will die a natural death......Huwezi kutegemea mwadamu mweinzio 100%"ukafika.
 
Na nyie nao bei yenu rahisi sana mnanunulika hata kwa mtaji wa changudoa. Jamii inawatumikisha
 
Alliance for Cowards and Traitors lazima kife maana kina undwa na wasiliti ambao mwisho wa siku lazima nao wasalitiane.

Usaliti uliofanywa na Zitto dhidi ya chadema akishirikiana na Kitila Mkumbo na Mwigamba ni usaliti ambao ingekuwa nchi za kidikteta wangehasiwa kama wanyama.

Haiwezekani tamaa ya madaraka iwafanye hawa watu wawe wehu wa madaraka hadi kuamua kwenda kinyume na katiba ya chama.
 
Mwigamba na kitila kwa nini usaliti mliojaribu kuufanya cdm mnataka kuuhamishia act baada ya kukaribishwa na 'waasisi'?

Mwigamba na Kitila hawajafanya usaliti wowote, hicho chama ni chao, wao ndio waliwatuma hao wanaojiita waasisi kuanzisha chama baadae wawakabidhi, sasa jamaa wamewageuka.

Ni sawa na wewe umtume jamaa yako akakununulie baiskeli, halafu baadae aseme ni ya kwake kwa sababu kanunua yeye, je huo ni uungwana?
 
Mshaanza kulia lia mapema kabisa. Na bado mpaka maji muite mma.
Ova
 
Back
Top Bottom