Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Vizuri mwandishi inavutia kusoma na kutunza hadhi ya jf makala Nzuri.

Sent using Iphone 7+
 
Mchambuzi yuko vizuri, Roma yuko vizuri, GENTAMYCINE , ni rahisi kusema kuliko kutenda. Roma amejibu kile mlichotaka kusikia, sasa badala ya kumsifia unamponda? Yuko wapi Ulimboka , mbona hajawahi kutuambia waliomteka? Mpeni sifa zake Roma, kwa kweli hata huu wimbo ni kwamba amewataja waliomteka, amewakemea, na amewashauri. Pia amewaonya kwamba hayo wafanyayo , yana mwisho kwani Mungu wa Yohana ndo huyo huyo wa Daudi! Twende Zimbabwe!!!
 
Nilishasema na leo narudia tena kusema kwamba Roma Mkatoliki ni Mpuuzi tena wa kutupwa na akae atambue kuwa siku ile ya Press Conference alituangusha mno Watu tuliokuwa nyuma yake na ambao pia tulipaza sauti zetu nchi nzima ili apatikane.

Hivi umeshateswa nusura au karibia ya Kufa halafu umeachiwa bado tena unapewa fursa ya kuongea na Watanzania ili useme ukweli ili yajulikane na mengine yaliyojificha Yeye alichotufanyia pala ni kutuonyesha tu minjino / mimeno yake na kijijeraha uchwara na alama za mgongoni na kutembea kiupande upande utadhani Lori la Bedford limekata spring na bandage yake Ugokoni.

Kuna Wapuuzi fulani wakasema kuwa eti kama angesema ukweli angekufa je Mke na Watoto wake wangeishije? Hapa ndipo niliwashangaa baadhi ya Watanzania na Roma Mkatoliki mwenyewe na kugundua kuwa kumbe kuna Watu humu Mashuleni tuliwasoma sana Mashujaa wetu lakini hatukujua nini maana ya Shujaa.

Hivi Watu Mashujaa kama Nelson Madiba Mandela na Patrice Emelly Lumumba achilia mbali akina Chifu Mkwawa wasingejitoa mhanga kwa ajili ya Waafrika Kusini, Wakongo na Wahehe wakati wa Mapambano ya Kudai uhuru na haki leo hii wangekuwa wanakumbukwa na kuitwa Mashujaa?

Hivi Mandela au Lumumba au Mkwawa wao hawakuwa na Familia zao? Hivi Msanii Roma Mkatoliki ni mkubwa kwa hao niliowataja hapo juu hasa Kiushujaa? Kwani siku ile ile ya Press Conference yake angefunguka tu na kusema ukweli halafu hata kama angeuwawa / angeuliwa bado asingebaki kuwa / kuitwa Shujaa na Watanzania wengi waliopaza sauti zao juu ya kule Kupotea / Kutekwa Kwake?

Kwa Upuuzi huu nawalaumu sana Watekaji kwani ni kheri tu wangemaliza shughuli mapema tu huko huko Ununio mkabala na Mahaba beach. Yaani unateswa hadi kuumizwa nusura ya Kufa halafu unapewa platform ya kutiririka na kuserereka Wewe unabaki kujibinua binua tu katika Kiti.

Niliacha rasmi kutompenda na kumshabikia Roma Mkatoliki siku ile ile aliyofanya Press Conference yake baada ya kutoka Kutekwa na Kuteswa na kama ni kumpenda au kumshabikia basi nitafanya hivyo kwa Mke wake mzuri na mrembo hasa Nancy kwani ana kila aina ya ushawishi ambao utasabisha Mimi kumkubali.
Kunywa maji mengi ili upeleke mkojo mwenyewe bila kufatwa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchambuzi yuko vizuri, Roma yuko vizuri, GENTAMYCINE , ni rahisi kusema kuliko kutenda. Roma amejibu kile mlichotaka kusikia, sasa badala ya kumsifia unamponda? Yuko wapi Ulimboka , mbona hajawahi kutuambia waliomteka? Mpeni sifa zake Roma, kwa kweli hata huu wimbo ni kwamba amewataja waliomteka, amewakemea, na amewashauri. Pia amewaonya kwamba hayo wafanyayo , yana mwisho kwani Mungu wa Yohana ndo huyo huyo wa Daudi! Twende Zimbabwe!!!
Sijamponda mtu mkuu Labda sema sijamsifu Roma kwa utunzi makini wimbo Mzuri.

Sent using Iphone 7+
 
Andiko bora

*IMBA ROMA; MUNGU WA PAULO NDIYE WA DAUDI NA JOHN*

Na Luqman Maloto

Usiyaone ya jirani ukashabikia tu, vifua vina mengi yanafichwa ndani yake. Si kila ukatili ambao mtu anatendewa lazima atoke na kuusema kinaga ubaga. Inawezekana ni hatari zaidi kupayuka kuliko kunyamaza.

Wake za watu wangapi wanabakwa na wapangaji wenzao kwenye nyumba za kupanga lakini wanaamua kunyamaza? Hawaendi polisi na inabaki siri yao. Ukimya wao haumaanishi kufurahia tendo, isipokuwa wanawaza athari za baada ya kutamka.

Ni wanawake wangapi waliopoteza ndoa zao baada ya kusimulia jinsi walivyobakwa? Waume zao waliwaacha kwa taadhira juu utadhani walifurahia kubakwa. Mke wa mtu anawaza aseme iwe aibu mitaani kisha na kwenye ndoa aachike? Anaamua kunyamaza japo inamuuma moyoni na hasira juu kwa aliyembaka.

Wanawake wangapi walibakwa, badala ya kuwahurumia ikawa simulizi ya kuwanyooshea vidole? Mtu anapita barabarani watu wananong'onezana "yule, yule", nani anapenda aibu hiyo? Anaamua kunyamaza ili iwe aibu kwake mbele ya yule tu aliyembaka.

Si mjinga yule mwanamke aliyebakwa ofisini na bosi wake au mfanyakazi mwenzake kisha akanyamaza. Si kwamba alipenda iwe siri yake mbakwaji na aliyembaka, bali alifahamu athari yake kuwa angegeuzwa ubao wa matangazo kwa wafanyakazi wenzake, kisha mchumba au mume wake angemhukumu na kumwacha.

Vipi yule mwanaume aliyetekwa na kulawitiwa? Unadhani asingependa waliomfanyia kitendo hicho wachukuliwe hatua? Hata hivyo upande wa pili anawaza aibu ya matokeo baada ya kutamka.

Mwanaume gani aliyenyooka (straight), angependa ijulikane kuwa alilawitiwa na wanaume wenzake? Kwa mwanaume aliyenyooka, tendo la kulawitiwa hutafsiri kama kudhalilishwa kuliko kukubwa kuliko aina yoyote ile ya udhalilishwaji. Hivyo anaamua kunyamaza ili iwe siri ya wachache.

Ni shoga pekee ndiye anaweza kukiri mbele za watu kuwa amelawitiwa. Hilo lipo wazi. Ni kama ambavyo ukimbaka mwanamke kahaba na usimpe chake, hataona aibu kukujazia watu na kila mtu atajua umetembea naye. Kwake watu kujua si aibu.

Mwanamke anayejiheshimu huogopa hata kumsimulia rafiki yake mwanaume aliyechepuka naye kwa kuhofia kuonekana kiwembe. Ukiona mwanamke anataja hovyo anaowapitia bila aibu, ujue huyo ameshapoteza sifa ya kawaida ya kike.

ACHA ROMA AENDE ZIMBABWE

Nimeanza na utangulizi huo kujiweka sawa na safari ya mguu kwa mguu na Rapa Ibrahim Mussa Mshana 'Roma Mkatoliki', kwenda Zimbabwe. Ndani ya wimbo mpya wa Roma unaoitwa Zimbabwe, ameonesha kuwa anayo mengi angependa aseme.

Hata hivyo, Roma anajibu kwa verse hoja zote zenye kumtaka aseme kile ambacho kilimtokea alipotekwa na watu wasiojulikana. Roma anasema kuwa yeye si rapa tu, bali ni baba wa familia. Je, akisema halafu akiuawa nani atakayebeba majukumu yake ya kifamilia? Mama na mtoto wake watalelewa na nani?

Wewe ambaye unataka Roma amtaje aliyemteka, anakuuliza kuwa mtekaji akiiteka ripoti ya upelelezi itakuwaje? Ukifika hapo unapata majibu kuwa Roma aliumizwa sana lakini anashindwa kusema yote hadharini. Anasema yeye haogopi kufa.

Sababu ya kuhofia kusema si nyingine bali ni maisha yake binafsi. Anauliza faida ya kutamkwa tu alikufa mwanaharakati wakati nyuma yake atamwacha mama yake na mtoto wake wakiwa hawana matunzo.

Ni ujumbe unaochoma sana. Tafakari mwandishi na mwanaharakati wa Nigeria, Ken Saro-Wiwa, aliyeuawa kwa kunyongwa mwaka 1995 na Serikali ya Nigeria iliyokuwa chini ya utawala wa Dikteta Sani Abacha, kama si kampuni ya mafuta ya Shell iliyoilipa fidia familia yake kwa msaada wa Marekani, familia yake ingekuwa imeambulia patupu.

Shell walitoa fedha dola 15.5 milioni, sawa na Sh34.7 bilioni kwa familia ya Saro-Wiwa na ndugu wa watu wengine nane jamii ya Ogoni, Niger Delta, Nigeria, waliouawa wakati wa kupigania fidia ya madhara ya kiafya na kimaisha baada ya kuharibiwa mazingira kutokana na kazi ya uvunaji wa mafuta ya Shell.

Roma yeye akiuawa leo nani atailipa familia yake fidia? Ndiyo maana anahoji yule ambaye atamlea mwanaye au mama yake? Hapohapo anakumbusha kuwa alipokuwa anauguza majeraha baada ya kuachiwa na watekaji, watu hawakwenda japo kumjulia hali, je, wanasubiri afe waende msibani?

Ipo hoja kwa Roma, harakati bila matumizi bora ya ubongo ni hasara ya mwanaharakati. Dunia imejaa ubinafsi, faida ya mwanaharakati ni vile ambavyo yupo hai na anadunda. Mwanaharakati akishalala watu huwa hawana habari naye kabisa.

Tajiri nambari moja Afrika kwa wakati wake, Chifu Moshoob Abiola, aliamua kutojali utajiri wake na kujikita kwenye harakati za kuubadili utawala wa kijeshi Nigeria hadi utawala wa kidemokrasia, matokeo yake alifia jela mwaka 1998 na fedha zake zilichotwa benki na watawala wa kijeshi. Familia yake ikabaki maskini.

Kuna wakati harakati zinakata stimu mpaka basi ndiyo maana watu wengine huamua kuwa wabinafsi kwa kufanya harakati za matumbo yao na familia zao na kuachana na zile za ukombozi wa jamii. Tafakari, familia za wazee akina Oliver Tambo, Walter Sisulu na wengine zinaishije leo, wakati Rais Jacob Zuma anafanya ufisadi wa mali za Waafrika Kusini.

Familia ya Bibi Titi Mohamed inaishi vipi leo, wakati ambao kuna akina mama ambao hawajui japo tone la jasho la ukombozi wa nchi, waliposhika nafasi nyeti serikalini waliamua kuwasaliti wananchi na kufanya ufisadi? Wajukuu zake wanajisifu tu kuwa na bibi mwanaharakati na mkombozi wa nchi.

POTEZEA HASIRA KWANZA

Imeeleweka kuwa Roma anazo sababu za msingi za mambo mengine kunyamaza, maana viatu alivyovaa siri yake anaijua yeye zaidi kuliko mwingine yeyote. Hatari ya kusema na usalama wa kukaa kimya, mjuzi wa undani zaidi ni yeye.

Hata hivyo, daka mstari ndani ya wimbo, Roma anasema kuwa hakuona nyota begani lakini anaamini kuwa aliyemteka ni askari. Swali ambalo lipo kichwani kwa Roma ni kuwa hajui kama aliyemteka alitumwa au alijituma mwenyewe.

Tunarejea kule ambapo maswali yalikuwa mengi kuhusu aliyemteka Roma. Wengi walisema ni polisi, kuna waliowataja maofisa wa Usalama wa Taifa, hadi mjadala ukatikisa Bunge kuwa maofisa usalama walikuwa wakiteka na kutesa watu.

Walikuwepo waliodai Roma alijiteka mwenyewe ili kupata umaarufu. Wengine wakadai Roma alipewa fedha ili ajipoteze, lengo likiwa kuiweka nchi kwenye hali ya wasiwasi. Kila mmoja na alichosema, mimi nashika mstari wa Roma kuwa hakuona nyota begani ila anaamini aliyemteka ni askari. Kuhusu kwamba alijituma au alitumwa, hilo tusiumizane vichwa!

Halafu naongeza kwa mkazo kuwa kutekana ni uhuni wa kishamba. Kila mmoja anapaswa kufurahia uhuru wa nchi yake. Ikiwa Tanzania huru watu wanajiona hawapo huru, kuna sababu gani kuisifu nchi kwamba ipo huru? Uhuru wa nchi unapaswa kudhihirika kwa watu wake.

Haitakiwi mtu awe anaogopa kutoa maoni au kuzungumza chochote kwa hofu ya kutekwa. Raha ya uhuru ipo wapi? Mbaya zaidi mpaka mbunge analalamika bungeni kuwa alitekwa na maofisa wa Usalama wa Taifa. Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alitoa machozi bungeni.

Sehemu ambayo inaumiza zaidi ni pale ambapo anasema kuwa mama yake alikwenda mpaka kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti na kukagua miili ya marehemu ili kuangalia kama mwanaye anaweza kuwemo. Unaweza kujiuliza ni kwa kiasi gani mama yake alikata tamaa mpaka kufikiria kuwa mwanaye alikuwa ameshauawa.

Hutapata hisia za kukaribiana na hali halisi kama huwezi kumuwazia mwanaharakati kada wa Chadema, Ben Saanane jinsi familia yake na marafiki zake walivyopatwa na wasiwasi kiasi kwamba wakaanza kuhisi kuwa miili ya watu waliokuwa wanaokotwa wakiwa wamekufa Mto Ruvu, pengine mmoja wao ni Ben. Wakataka wakague.

Ni kwamba unapopotelewa na ndugu, wasiwasi unakuwa mwingi. Unakwenda kila sehemu kuulizia hupati majibu. Ni mtu mzima na akili zake ni timamu, haiwezekani apotee kienyeji. Sasa inapotokea unamsaka kila upande humuoni, mwisho unawaza kwenda vyumba vya kuhifadhia maiti hospitalini.

Hatua ya kufikiria ndugu au rafiki yako yupo chumba cha kuhifadhia maiti, hivyo kuvamia majokofu na kukagua miili, maana yake ni kwamba umeshakata tamaa na umeingiwa na hisia kwamba tayari ameshafariki dunia. Kuwaza tu hilo maumivu yake ni makubwa sana.

Ben yupo wapi? Tangu Novemba mwaka jana. Kwa hiyo ana miezi tisa sasa hayupo. Utata ni mkubwa sana. Kapotezwa, kajificha au nini kingine? Suala la Ben kutopatikana na ukimya uliopo linazalisha uchungu, hasira, mawazo, wasiwasi na woga mkubwa.

TURUDI KWA ROMA

Baada ya kuyatafakari maumivu ya mama yake Roma, mke wake na ndugu zake wote wanaompenda sana, jumlisha na hali ambayo Roma alikuwa nayo baada ya kuachiwa na watekaji. Unaweza kuutafakari wakati mgumu ambao staa huyo aliukabili.

Ni kipindi ambacho anamsikia mama yake anamsema kwa ukali na msisitizo: "Si urap kama Joh Makini? Mbona yeye anarapa soft na maisha yake yanaendelea vizuri?

Roma akigeuka kushoto anakutana na sura ya upole ya mkewe yenye kushawishi kwa huruma, inamwambia: "Baba Ivan achana na mistari yako ya lete wajeda, lete mapongo, lete mamwela, lete wajomba. Andika tu mistari ya kunisifia mimi kama Diamond anavyomsifia Zari. Utauza na tutaishi kwa amani."

Ameseme mwenyewe kuwa yeye siyo rapa tu, bali ni baba wa familia, ni mtoto kwa mama yake, ni kaka kwa dada zake, ni mkwe kwa wazazi wa mke wake, watu wote hao muhimu kwake wamzunguke na kumwambia nyamaza, wewe upo Kibonde Maji unapaza sauti: "Roma mshamba, angemtaja aliyemteka." Wakati huo anaumwa hata pera humpelekei.

Hapo ulipo hujui ni kwa kiasi gani Roma alishawishiwa mara ngapi aachane na muziki. Tena waliomshauri ni watu wenye manufaa ya moja kwa moja kwake. Watu ambao hawakulala kipindi Roma katekwa. Siyo wewe ambaye wakati Roma anamenyeka na mateso ya watekaji, ulikuwa unabadili milango ya gesti na kushurutisha wahudumu wa baa wakufungulie vizibo vya bia.

SASA TWEN'ZETU ZIMBABWE

Yule Roma jasiri, mnyoosha mistari bila hofu. Roma aliyesema hata Ikulu anaipiga chata akiwa amevaa mlegezo kwenye ngoma Mathematics, siyo huyu wa sasa. Roma mpya anasema bora tu aende zake Zimbabwe.

Ni sanaa tu imetumika. Ielewe Zimbabwe ya sasa chini ya Rais Robert Mugabe. Halafu mtoe Roma, weka neno sisi. Hiyo sisi itumike kwa kutujumuisha sisi Watanzania. Je, Roma anamaanisha tunakwenda kufanana na Wazimbabwe chini ya Mugabe? Siku akijisikia kujibu atajibu!

Zimbabwe ni ngoma nzuri. Roma amethibitisha uwezo wake wa kuandika. Hajafyatuka kama alivyofanya kwenye 2030, Viva na nyingine sumu, lakini ameandika kwa tahadhari na ujumbe umefika. Ameahidi kuwa hata makinikia anayatengenezea mapini pia.

Roma amefanya kazi bora, ujumbe ufike kila upande. Ninyi wateka watu acheni huo uhuni wa kishamba. Acheni ushindani wa hoja uchukue nafasi. Siyo ukikosolewa kidogo unatuma watu wamteke aliyekukosoa, huo ni uzezeta.

Hapa nasisitiza kuwa yeyote aliyehusika na kumteka Roma na wenzake, aliye nyuma ya kupotea kwa Ben Saanane, hata awe mkubwa kama tembo, ajitambue kwamba yeye ni mshamba. Yaani bonge la mshamba!

Ujumbe kwa washabikia mambo na kutaka kilichomo kwenye akili zao ndiyo hichohicho kifanyiwe kazi na wengine bila kuvaa viatu vya wahusika kujua wanapitia magumu kiasi gani, waache ushabiki maandazi.

Mijeledi aliyopigwa, kisago alichopokea hukumsaidia, kwa hiyo hujui maumivu yake. Usikae tu pembeni na kupaza sauti. Ulimwengu mpya unakataza ushabiki. Siri ya mtungi aijuaye kata.

MUNGU WA PAULO

Hapa mimi sitii neno zaidi ya kukubaliana na Roma kuwa Mungu wa Paulo ndiye huyohuyo Mungu wa Daudi. Hakuna mabadiliko yoyote, kwani Mungu wa Daudi ndiye Mungu wa John ambaye Wayahudi humwita Yohana.

Mungu huyohuyo ndiye wa Roma na wengine wote duniani. Hivyo kila mmoja lazima atambue kuwa hakuna binadamu mwenye leseni ya kuwanyanyasa wenzake. Hayupo binadamu mwenye ubinadamu kipeuo cha pili, hakuna binadamu wa lumbesa na mwingine wa kawaida, wote ni sawa. Mungu ni mmoja, tusinyanyasane na vijibunduki vyenu.

Mungu Ni Mwema
Roma yuko sahihi

Poowaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyu jamaa nikiboko...anasem...mungu wa paul ndio mungu wa daudi na ndio mungu wa john wanaomwita yohana...WAYAHUDI ...kuna sarcasm hapo ya hatari...yaani waliotajwa hapo ni wayahudi walimtesa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
mungu wa Paulo (makonda) ndo mungu wa Daudi (bashite), ndo mungu wa John (makofuli) mnayemwita Yohana wayahudi (mnayemwita rais watz)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo sehemu unaitaji akili zako changanya na za kupewa utaelewa, Sanaa inafikisha Ujumbe.Mimi nimeelewa navyojua mimi.
wewe je?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom