Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amesema kauli yake aliyoitoa katikati ya mwezi Aprili mwaka 2024 ‘Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia polisi msiwatafute”, ilitafsiriwa tofauti akidai kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kilikuwa ni sehemu tu ya mazungumzo yake aliyoyazungumza kwa kirefu
Burhan ameyasema hayo akizungumza na mtangazaji Chief Odemba wa kipindi cha Medani Kuu cha runinga ya Star TV siku ya Jumamosi ambapo hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi Watanzania waliokwazika na kauli hiyo na kurejea msemo wa ‘Yaliyopita si ndwele tugange yajayo’