October 30: Uso kwa uso na bunduki

October 30: Uso kwa uso na bunduki

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,369
Reaction score
80,048
OCTOBER 30: USO KWA USO NA BUNDUKI.

Anaandika: Robert Heriel
Mtibeli.

1. Nitafupisha Sana kadiri iwezekanavyo maana wasomaji wangu wengi wenu hampendi vitu virefu.

2. Usiku wa tarehe 29 nyumbani kwetu ambapo nilisema ni karibu na barabara ya Morogoro yaani mita hamsini tuu;

3. Kulikuwa na muziki wa mabomu, risasi na fataki zilizokuwa zinarindima.

4. Majira ya saa 1-2 unusu usiku tulizoea kelele na hekaheka za magari barabarani huku kunguru weusi wakitusumbua. Lakini sio hiyo kunguru walikuwa likizo. Nakuambia kunguru walihama mtaa wetu muda huo.

5. Kwa macho yangu nilishuhudia mafungu kwa mafungu ya kunguru yakiruka kwa hofu bila kuelewa hatma yao. Je ni mwisho wa duniam hakuna aliyekuwa anajua.

6. Unajua sisi waandishi hasa waandishi wa aina yangu tunapenda kuchukua vitu in details hata kama ni kidogo kiasi gani.

7. Nilitaka nishuhudie kila kitu huku nikihatarisha usalama wa maisha yangu. Nafahamu risasi ni kitu gani lakini uchu wangu wa kupata historia kwa macho yangu mwenyewe ilinishinda. Hicho ungeita kihere here wala nisingekulaumu.

8. So muda mwingi nilikuwa nje. Huku na huko. Na mara moja moja nillirejea nyumbani kuangalia usalama wa familia yangu.

9. Mabomu ya machozi yaliendelea kurushwa na mara nyingi yalianguka aidha juu ya bati letu au ndani ya uzio wetu. Kifuatacho ni moshi. Kukohoa, machozi na mafua kwa watoto.
Wakati huo eneo letu lote lilikuwa giza kutokana na umeme kukatika. Hili nilishasema.

10. Milio ya risasi ilipungua saa tatu usiku hiyohiyo tarehe 29. Nikatoka kinyemela.

11. Aiseeh! Sasa nilijiona kwenye filamu ya kutisha kama mhusika katika filamu ya hollywood.
Mtaa upo na giza. Hakuna nyumba hata moja inayoonyesha uhai wa mwanga ndani yake. Sisikii hata kelele ya hatua zangu achilia mbali mapigo yangu ya moyo.

12. Barabara ya Morogoro road ilikuwa haipiti chochote kile. Giza!
Nikatokea barabarani kinyemela huku nikijua lolote linaweza kunikuta.
Sikudanganyi na napenda nikiri nilikuwa naogopa sana. Lakini nilipenda hali ile ambayo nilizoea kuiona kwenye fikra zangu nikiwa naandika simulizi zangu au nikiwa na tazama filamu. Sasa nilikuwa live naam Mubashara.

13. Hakuna popo, hakuna mdudu yeyote. Nikawa nimetulia kwenye ngema moja hivi pembeni ya barabara nikitaka mazingira yale yanizoee na mimi niyazoee ili nipate kuwa sehemu yake. Kwamba kitu kigeni kikitokea nijue kwa wepesi.

14. Ng'ambo ya barabara kulikuwepo gari ndogo ambayo ilikuwepo tangu mchana. Mbele yake yalikuwepo malori mawili. Yote wakati wa asubuhi niliyaona yakiwa yanakuja yakitokea upande wa Morogoro yakienda mjini.

15. Nikaangalia upande huo bado kulikuwa kimya. Hapakuwa na uhai wala dalili ya kiumbe chochote. Nasema chochote.

16. Milio ya risasi bado naisikia upande wa Ubungo Kibo na upande wa Kimara Mwisho.

17. Nikavuka barabara. Nilikuwa nimevaa Flana ya pamba hivi yenye rangi ya kijani ya kijeshi. Chini nimevaa pensi nyeusi. So ukiwa kwa mbali sio rahisi kuniona ukizingatia umeme ulikuwa umekatika na eneo lilikuwa giza. Chini nimevaa raba fulani ninazotumiaga kufanya mazoezi ya kukimbia.

18. Ghafla kwa mbali upande wa Ubungo kuna gari ilikuwa inakuja polepole. Wala sikutaka kujiuliza nilijua ni gari ya kina nani. Nikakimbia ng'ambo nikajificha kwenye kile kigari kidogo. Haikuchukua dakika moja lile gari lilifika usawa wa eneo nililopo. Hapo mapigo ya moyo sasa. Puu puu puu!

19. Ikasimama, hapo nami nikawa nimeshika pumzi yangu. Nikawa nachungulia. Ilikuwa gari ya polisi ambayo nyuma ni pickup ambayo ilisheheni polisi wanne kama sio watano walikuwa wamevaa sare na mikono wana silaha.

20. Redio call ilikuwa inaongea kutokana na ukimya wa eneo lile nilikuwa naisikia l. Inataja baadhi ya barabara kwa kutuma code na baadhi ya majina. Sijui kazimoto, na majina mengine ambayo nafikiri ni codename.

21. Sikuwaona wakizungumza. Gari muda huo inaenda mwendo wa adoado. Mara moyo wangu inalipuka puuu! Baada ya kusikia fataki likipigwa. Nusu nikimbie. Haaa! Wakapiga zingine mbili. Kisha wakaondoka.

22. Nikatoka kwenye ile gari ndogo niliyokuwa nimejificha. Nikawa nasogelea. Yale malori mawili. Palikuwa kimya. Nayapita mara nasikia sauti Oya Oya! Nashtuka. Nusura nianguke.

23. Kumbe ni dereva wa lori. Narudi. Wananiambia wananjaa hawajala tangu mchana. Wanataka niwape maelekezo wapi wanaweza kupata msosi. Nawaambia sijajua ila wakinipa pesa nitaongea na mke wangu apike then nitawaletea. Sasa ishu ikawa kuniamini kwamba kweli mimi ninakaa mtaa ule au ninaweza kuwaibia. Nikawaambia kama hawataki sio kesi. Nikawaacha.

24. Nikatokea mtaa wa Kimara Bucha ndanindani. Huko nikakutana na vijana wanafanya biashara ya Bangi. Wapo uwanjani. Nafikiri njia ya kuelea Golani eneo lile wanaita Matete kambi ya jeshi. Wale vijana nusura wafe kwa nilivyotokea kama mzimu. Hawanijui siwajui. Hatujuani

25. Zilikuwepo pikipiki tatu lakini vijana walikuwa kama kumi na moja hivi. Stori kuu zilikuwa matukio yaliyokuwa yanaendelea tangu mchana na usiku huo.

26. Biashara ya bangi na madawa ya kulevya ndivyo vilivyokuwa vinafanyika. Mara huyu anampigia aliyepo Tegeta. Mara huyu anampa taarifa wa Buguruni. Hapo ni kuleta biashara au kupeleka mzigo.

27. Gram moja ya bangi siku ile iliuzwa Tsh buku tatu. Kwa jinsi nilivyowasikia wale vijana.

29. Simu yangu ilionyesha ni saa nne na nusu.
Nikaona nirudi home.

30. Nikapitia njia nyingine. Milio kwa mbali inasikika na ni mara moja moja. Ni kama utulivu wenye hila ulikuwa umerejea lakini bado mitaa ilikuwa giza yenye ukimya wa kuzimu.

31. Nyumbani nakuta watoto wamelala, mke wangu ndiye hawezi kulala ananisubiri. Ule moshi wa mabomu ya machozi ulikuwa umeshaisha lakini hofu iling'anana katika kuta na mapaa ya nyumba.

32. Nikachukua ndizi nne. Nikamwambia mke wangu kuna madereva pale nje hawajala tangu asubuhi. Hapa ni wageni acha niwapelekee ndizi. Akanizuia akinisihi ni hatari. Nikatoka.

33. Sasa nilikuwa sio mwoga sana nilijiona sasa mimi ndiye naogopwa na waliojifungia ndani ya nyumba. Kumbe mwenyewe nilikuwa naogopa kupasuliwq ubongo.

34. Nikafika, nikagonga kwenye kioo cha dirisha la lori. Nikaona taa inawaka ndani kisha wanafungua mlango. Nawapa ndizi wanashukuru nikaondoka zangu. Na kurudi nyumbani. Usiku huo nilifikiri mambo mengi sana. Nilifikiri mambo ya nchi yetu. Sikujua hatma yake itakuwaje.
Niliomba Mungu kisha nikalala. Hapo ni saa sita kasoro.

35. Asubuhi ya tarehe 30. Ilikuwa asubuhi nzuri tuu kwa upande wa familia yangu.

36. Hofu ilikuwepo, simu za kujuliana hali wazazi, ndugu jamaa ziliendelea.

37. Geti letu la mbele linaloangalia barabara ya Morogoro road lilivunjwa kile kidanga na waandamanaji siku ya jana yake tarehe 29. Kwamba polisi wakija waandamanaji walikuwa wakikimbia hovyo hovyo na kwa vile nyumba yetu ilikuwa ipo karibu basi walivunja.

38. Nikachungulia nje nikakuta bado kuna watu barabarani pembezoni.

39. Nikatoka lakini mke wangu ananizuia. Nikamwambia maelekezo ni yaleyale. Usitoke nje. Usifungue pazia kuchungulia ukisikia huko nje watu wakikimbia.
Ujifiche kwenye ukuta usioangaliana na dirisha.
Usifanye movement yoyote wewe na watoto. Kwa sababu jana yake tuliona kilichotokea risasi zilikuwa zinarushwa hovyohovyo.

40. Nikatoka. Siku ya pili ilikuwa tofauti kidogo. Nitaeleza;
a) kwanza hapakuwa na waandamanaji isipokuwa magari ya doria ya askari yaliyokuwa yakienda na kurudi. Ni kusema barabara hazikuingiwa na waandamanaji

b) Nguvu iliongezwa nafikiri kutokana na hakukuwa na uchaguzi na uchaguzi ulikuwa ushaisha. Hivyo askari wengi walikuwa barabarani kufanya doria.

c) Mabomu ya machozi hayakuwa mengi wala fataki ila risasi ndio zilikuwa nyingi.

41. Basi nimesimama pembeni ya barabara. Mbele ng'ambo ile gari ndogo na yale malori mawili bado yapo.

42. Tukiona magari ya polisi yakija kwa. Mbali tunakimbia yakipita tunarudi. Hivyohivyo.

43. Sasa nilijua hali ile haitaendelea vile. Lazima wangebadilisha mbinu. Kwani mchezo ule kwao ulikuwa unawagharimu mafuta.

44. Wakija na magari wanapiga risasi weee wakiwa juu ya magari yao sisi tumekimbia mitaani na kujificha. Wakimaliza wanaondoka wanaenda upande wa kimara mwisho ambao nako kuna watu hivyohivyo.

45. Tulikuwa tumekariri yale magari.
Saa tatu hiyo asubuhi tarehe 30.

46. Ikaja gari moja nyeusi Nisani sijui kitu gani. Bio tinted. Hizi hatuzikimbii. Magari ya kawaida ambayo ndani yana wanajeshi pia hatukimbii. Tulikuwa tunakimbia gari za polisi zilizokuwa labelled. Na nyingine zenye pickup nyuma wakiwepo Polisi.

47. Kumbe Polisi nao wakaona hapa watakesha na sisi wakiendelea na mbinu hiyohiyo.

48. Ndio hiyo gari Nyeusi Nisani yenye muundo wa Toyota Fortune ikawa inakuja polepole ikitokea uelekeo wa mbezi.

49. Ule mwendo wa polepole mimi nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu. Na Mungu aliniongoza.

50. Wengine hawana habari lakini bado wanaitazama sio kwa uzito.

51. Ile gari ikafika usawa wetu. Tukawa wote tunaitazama.

52. Taratibu kioo kinateleza kwenda chini. Nilipoona hivyo. Kwa upesi nikainama chini nikiwa natambaa nikisema anapigaaa! Sasa wale wengi walichelewa kama nukta mbili au tatu kuelekea sekunde moja. Kabla sijamaliza kuzungumza nikiwa natambaa chini kama nyoka nikiburuzika kukimbia nasikia mlio wa risasi twaaa! Kisha kelele na vijana kukimbia. Muda huo nishaipata kona ya bar tuliyokuwepo.

Tayari ashapigwa mmoja ya mguuni.

53. Ile gari ikaondoka. Walipiga moja tuu. Nafikiri ilikuwa kama warning.

54. Sasa ndio kuhangaika na yule kijana aliyepigwa risasi. Kwanza wengi hatujuani. Sijui wale vijana wengi wao walitoka wapi. Tuliokuwa tunajuana tulikuwa wachache na ni wakazi wa nyumba za barabarani.

55. Akapelekwa Hospitalini.

56. Sasa nilielewa somo. Nilijua Polisi wamebadili mbinu. Na round hii hawatanii.
Kumbuka mitandao imezima hivyo hatujui upande wa pili nini kinaendelea.
Wanaopiga simu sio rahisi kuwaamini asilimia mia moja tofauti na mitandao ya kijamii ingekuwa on tungejionea kwa macho hatari iliyopo.

57. Hata hivyo hatari hata ingekuwa binafsi nilikuwa na mambo yangu nataka nipate uhalisia wa mambo sio kwa kusimuliwa.

58. Watu wakajaa tena palepale.
Mimi sikwenda. Nilijua kama wametumia mbinu hiyo ni kwamba round hii watakuja na gari yoyote au wanaweza wakatokea hata nyuma yetu yaani wakatuzungia.
Kwamba wanaweza baadhi wakashukia kituo cha bucha au hata baruti alafu wakaingia mtaani wakaja nyumanyuma mpaka pale tulipo.

59. Mawazo hayo yakanipa onyo na kuniambia nisikae pale. Kuna kijana mmoja ambaye ni jirani yetu nikamwambia hapo sio salama kwa sasa. Nikajaribu kumfafanulia kwa kiasi lakini mimi sio mzuri wa kuongea labda ningemuandikia.

60. Sijui hata kwa nini nilimuambia yeye. Hata hivyo wengine pia walikuwa wakisikia.

61. Nikarudi ndani. Mke wangu anajiuliza. Vipi mbona siendi. Namuuliza siendi wapi. Ananiambia si huko kuangalia kinachoendelea. Nikacheka nikamwambia sasa hivi huogopi eeh!

62. Nikamuelezea scenario na hisia zangu jinsi zinavyonituma. Ananiamini! Na nilieleza jambo lenye Logic kama nilivyoeleza hapa sababu ya kutokukaa au kusimama pale pembeni ya barabara.

63. Nikatoka lakini wakati huu nikiwa ndani ya Uzio wa nyumba. Uzio wetu upande wa barabara ya Morogoro road unasenyenge hivyo unaona barabara. Nikakaa kwenye varander ya nyumba nikiwa naendelea na kuchezea simu. Nacheza gemu.

64. Saa nne unusu ghafla naona gari aina ya land cruiser zile hardtop kama ambulensi imesimama barabarani kama mita. Sabini tokea pale wanapokuwa wanasimama watu.

65. Wale vijana wakakimbia wanajificha kama kawaida. Mimi naangalia iwe gari.
Wanashuka askari sita. Watano wamevaa sare mmoja hajavaa. Wamebeba silaha na wapo kivita.

66. Mwendo waliokuwa wanatembea nao wakichukua position na Kasi yao ilinipa onyo na kuniambia kuna jambo baya llinaenda kutokea.

67. Wale vijana wanaendelea kukimbia. Na milio ya risasi inaanza kurindima.

68. Kijana mmoja ambaye ni wamtaa uleule akafungua geti letu akaingia sasa akiwa amejificha nyuma ya banda.
Wengine wakawa wanakimbia kimbia hivyo.

69. Wengi wao hawakujua kama wale askari wanakuja

70. Nikamwambia yule kijana ambaye ni bodaboda pale mtaani aliyejiingia getini kwetu. Nikamwambia wanakuja nikiwa nami nimesimama. Nilihisi ule mwendo na miachiano ya nafasi wanayoifanya wale askari ni miondoko ya kupiga mtu risasi.

71. Yule kijana akawa akawa anataka kutoka getini akimbie. Nikamwambia kwa sauti ya msisitizo utachelewa hutoboi.
Nikamwambia ingia ndani. Akaingia.

72. Mwingine kwa nje alikuwa kajificha kwenye tanki la maji upande wa pili kwa jirani nikampa Ishara akawa hanielewi. Nikapaza sauti. Kimbia wanakuja.

73. Akachomoka. Risasi bado zinalia na tayari wameshakaribia.

74. Mmoja akashuka na barabara ya chini, mwingine akaenda barabara ya msikitini. Mmoja akasimama kwenye kiungo cha Y kwenye hiyo barabara

75. Ghafla geti linapigwa teke uso kwa uso naangaliana na askari aliyevalia nguo za kiraia akiwa ameninyooshea bunduki.

76. Nyuma yake akaingia mwingine amevalia sare za kijani za polisi. Wote walikuwa weusi tii na sura zao zilikuwa kali zenye kiu ya kupiga risasi.

77. Nikawa nawatazama huku moyoni nikimwomba Mungu na kuagiza atulize viumbe wake wasinidhuru.
Unajua muda huo sijui kwamba wanaingia mpaka kwenye nyumba za watu. Hayo mambo tumekua. Mtandao ulivyokuja ndio tunasikia kwa wengine.

78. Mmoja akawa anatazama mlango ambao nilimuingiza yule kijana ambao ulikuwa umefungwa robo na ndani yake kuna pazia.

79. Nikawasalimu. Vipi? Nikiwa nawaangalia usoni moyoni nikikemea pepo la mauti.

80. Unataka Kufa? Unataka kufa eeh? Yule askari aliyevaa nguo kiaskari akaniuliza akiwa amenikaribia kama hatua tatu tuu ameninyooshea bunduki.

81. Muda huo bado nasikia upande wa chini milio ya risasi.

82. Sikujibu chochote. Nikawa namtazama. Yule aliyevaa nguo za kiraia akaniambia kwa nini sipo ndani. Yule mwingine anarudia unataka kufa unataka kufa. Ni kama alikuwa anajichochea hasira na kujipa ujasiri ili afyatue.

83. Mara upande wa nje ya geti inasikika redcall ikisema. Kigogozeru ongeza nguvu kigogorezu. Haraka haraka.

84. Macho yetu yote yanaenda kwenye dirisha baada ya kuona pazia linacheza. Kumbe mke wangu na jirani yetu alikuwa anatazama. Lakini hatukuwaona. Nilijua. Walipoondoka.

85. Una bahati sana. Ingia ndani usitoke wakaamrisha huku wakiondoka na kutoka getini wakarudishia geti.

86. Huuuh! Nikashusha pumzi. Nawaona wanapanda gari lao hao wanasepa.
Mara mke na jirani wanatoka. Na yule kijana wanapumua utadhani walinyooshewa bunduki wao.

87. Tunasikia kilio upande wa pili msikitini huko. Ninatoka . Ooh! Ni yule kijana ameuawa kwa kupigwa risasi ya tumbo. Kijana yule yule niliyemuambia asikae pale eneo lile sio salama tena.

88. Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
89. Wahanga wengine ni wale waliokuwa wakirudi kutokea walipokwama siku ya tarehe 29 hawa wengi walikipata pata na wengi walilala nje.

90. Tuendelee kuiombea nchi yetu. Nimechoka kusimulia. Mungu wa mbinguni awabariki.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Dogo unajipa sana umuhimu ambao huwa ahuna. Kaza kazana huenda ukafikiwa na wewe ukalamba asala ya pesa ya damu

Mindset yako hiyo. Unatafsiri watu kulingana na mawazo yako. Yalivyo. Unafikiri ulivyo wengine wapo kama wewe.
 
Aisee...kwa hamaki hii Kuna uwezekano Kuna vitu tumeona vimekuogofya...si bure.

Alafu Morogoro road kuanzia Corner, baruti, Bucha, Korogwe, Kimara hekaheka zilikuwepo mchana tuu. Usiku sio kivile.
Askari hawakukamia show.

Kuna jirani yetu nyumba yake haina uzio naye alikutwa akiwa anahamisha jicho akaulizwa swali hilohilo unataka kufa unataka kufa. Ikapigwa mashine juu lakini hakuuawa.
 
Chai
Nyoko wewe ulitoka wapi wakati mlijificha, umesoma visa vya watu umeunga unga ukajiweka wewe ndo staring..!! Chidanga mkubwa 😡
Huyu watu wasipo kuwa makini, atawalengesha kwenye mfumo. Toka mwanzo wake huyu dogo nilimuona ni mtego huu wa wahuni uliojileta kwa picha flani, ni kina Yeriko type
 
Mkuu tuwekee hata picha ama video, si una camera hapo nyumbani. Mbona mnakuwa waogawaoga kuachia matukio.

Hadithi zako zingekuwa na picha ungetisha sana mkuu.

Bahati mbaya maneno matupu tu.
 
Unajipa umuhimu ambao huna unahaingaika hovyo hovyo reputation huna tena manyoko
 
Who cares ? Hii ungeshare na ukoo wako, sisi haituhusu
 
Back
Top Bottom