October 29, Tulianguka, Tumeinuka, Sasa Tunasonga Mbele

Nadhani na yeye mwenyewe Rais Samia hili atakuwa ameliona, pengine ndio maana ameahidi kuanza mchakato wa maridhiano.

..anaahidi vipi maridhiano huku ukiendelea kuteka, na kupoteza watu? Hivi kiongozi wa aina hiyo ana dhamira ya kweli?
 
Ukweli ni ukweli tu, kama huo ndio ukweli hata wajitahidi vipi kuuficha mwisho wa siku utajulikana tu. Hofu yangu tusiwazushie watu mambo ambayo hatuna uhakika nayo. Ikitokea watu wakatekeleza mobb justice based on uzushi tutakuwa tumewakosea sana waathirika.
Kwamba tunachosema kuhusu wao ni uzushi? Kama bila aibu wameweza kusema rais kapata kura 31m, jambo kubwa hivyo watashindwa kukataa ukweli mwingine?
 
comrade_kipepe kwani mimi nimeunga mkono mauaji ya raia?
Hivi haya makala yalipaswa kuandikwaje haswa ili yatoe sura ya habari niliyotaka kuifikisha?
Mauaji ni mauaji tu, hayakubaliki abadan. Muuaji yeyote, bila kujali ni police au sio police adhabu yake anayoistahili ni kunyongwa hadi kufa.
Huo ndio msimamo wa sheria zetu, na ndio msimamo wangu pia
 
Nadhani na yeye mwenyewe Rais Samia hili atakuwa ameliona, pengine ndio maana ameahidi kuanza mchakato wa maridhiano.
Maridhiano gani huyo tapeli? Wakati wa Magufuli aliingia na gia hiyo hiyo ya maridhiano, alipoambiwa asaini hayo makubaliano akagoma. Cdm wasiingie kwenye mtego wa maridhiano hewa. Kama kinawaka acha kiwake tu.
 
Siamini kama yeyote aliyethibitika kuua ataachwa bila kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo bila kujali yy ni nani. Utashi wa kisiasa wa kufanya hivyo upo, nia ya kufanya hivyo ipo na sababu za kufanya hivyo pia zipo.

..tangu Mama ichukue usukani ni miaka 4 na utekaji na upotezaji wanaharakati haujapungua bali umeongezeka. Kwa msingi huo kusema kuna utashi wa kuwashughulikia wauwaji ni kutudharau.
 
Jamaa ameandika gazeti refu but ameegemea upande mmoja. Hawa ni watu wanaotumika kuleta propaganda chafu.

Hakuna sehemu amesema serikali na vyombo vyake vichukuliwe hatua. Huu ni unafiki.

Solution ya tatizo ni rahisi.

1. Uchaguzi ni batili lazima urudiwe

2. Samia, IGP na wauji toka polisi lazima wakamatwe na kufikishwa mahakamani kama si na wao kupigwa risasi.

3. Wakuu wa mikoa na wilaya na wanakati wote wa usalama lazima wakamatwe.

4. Bila haya kufanyika tunadanganyana.
Nimesoma limakala lake refu kwa uangalifu baada ya kuona kuwa anajitanabaisha kama Dr. Kuna vipointi pointi vya hapa na pale lakini ukiwa ni chawa hata ujitahidi vipi utakuwa biased tu. Ameishia kuelemea upande mmoja tu utafikiri ni Pasko Mayala the second.

Hawa jamaa hawana uchungu utafikiri uhai wa maelfu ya vijana waliouwawa hauna thamani yo yote kwa vile tu wao wanafaidika na mfumo uliopo. It is very saddening!

➡️➡️➡️ Picha: Alipigwa risasi akapona, akatafutwa na kumalizwa kinyama
 
Switching up to English will not change a damn thing in your horribly woeful piece of shit you wrote. It's a futile ass-licking attempt geared to trying to get noticed. Make you name by being true to humanity values and not shaking your booty Infront of merciless rulers
You just made my day, sir.

Thank you 👊
 
Hebu fafanua objectively ni kwa vipi makala haya yanathibitisha uchawa?
Nadhani ulikuwa unatoroka masomo ya ufahamu, yaliyokuwa yakituelekeza kusoma hadithi kwa makini kisha kujibu maswali.
Your comment is completely off the point.
Tunashida Kama Taifa huwa tunaongozwa na miemko zaidi kwenye utoaji wa hoja badala ya kuwa na utulivu wa kiakil
..anaahidi vipi maridhiano huku ukiendelea kuteka, na kupoteza watu? Hivi kiongozi wa aina hiyo ana dhamira ya kweli?
 
Nimesoma limakala lake refu kwa uangalifu baada ya kuona kuwa anajitanabaisha kama Dr. Kuna vipointi pointi vya hapa na pale lakini ukiwa ni chawa hata ujitahidi vipi utakuwa biased tu. Ameishia kuelemea upande mmoja tu utafikiri ni Pasko Mayala the second.

Hawa jamaa hawana uchungu utafikiri uhai wa maelfu ya vijana waliouwawa hauna thamani yo yote kwa vile tu wao wanafaidika na mfumo uliopo. It is very saddening!

➡️➡️➡️ Picha: Alipigwa risasi akapona, akatafutwa na kumalizwa kinyama
Dr Uchwara huyo.

Reasoning ni zero.

Hawajali maisha ni unafiki na kujipendekeza ili wapatiwe favors maisha yeende.

Ona hii police wakiburuza mwili. Hawa watu ni wanyama aisee
 
Attachments

  • IMG_2138.jpeg
    IMG_2138.jpeg
    379.9 KB · Views: 15
Na laana iwe juu ya walitudhulumu Mo 29
 
Hatujainuka bado mpk haki ipatikane hii
nchi sio ya kundi fulani ni yetu sote

9dec
 
Mficha maradhi kifo humuumbua. Huu ndio ukweli ulioniongoza kuandika tafakuri hii kuhusu October 29 angalau tujifunze jambo la kutusaidia baadaye.

Nini kilitokea October 29, hautakuwa mjadala wangu wa leo. Utashi wangu unaniongoza kuwa hiyo si habari mpya tena, kila mtanzania aidha ameathirika yeye mwenyewe, au ameona kwa macho, au amesikia habari au ameonja joto la lock down, internet shutdown pamoja na kufungwa kwa biashara ya petrol. Mjadala wangu leo utakuwa tulifikaje hapo?

Vuguvugu kuhusu kuwepo kwa maandamano katika siku tajwa lilianza muda mrefu, kwa maoni yangu, tangu CHADEMA wamalize uchaguzi mkuu wao pale mlimani city. Pale campaign ya "No reforms, No election" ndipo ilipohuishwa. Kama hatua ya kujibu mapigo CCM, wakaja na "Oktoba Tunatiki"

Itakumbukwa hata Kikwete alizitambua "No reforms, No election " na "Octoba Tunatiki" kama ndizo kambi zilizokuwa na ushindani wa kweli kuelekea October 29.

No reforms, No election ilianza kupata sura mpya baada ya Bishop Gwajima kujitokeza kusema kipo kikundi "untouchable" kinachoratibu utekaji wa watu, akafuatiwa na Balozi Polepole kupinga uteuzi wa Rais Samia kupeperusha bendera ya CCM akimtuhumu kukiuka utaratibu na kuwalinda watu aliowatuhumu kuwa mafisadi, baadae akajitokeza Captain Tesha kutaka jeshi lizuie uchaguzi kwa madai hayo hayo ya kuwepo ufisadi na ukiukwaji wa demokrasia na mwisho Mange kuwahimiza watanzania waandamane kuchukua nchi yao akidai ufisadi umekithiri serikalini. Kwa maoni yangu, hayo ndiyo yaliyochochea maandamano ya October 29.

Jambo la kushangaza ni kuwa, pamoja na kuwa taarifa hizi zilikuwa wazi mitandaoni kwa muda mrefu, vurugu zilipoanza ilikuwa ni kama tulishitukizwa vile, kwani mpaka zinadhibitiwa tayari katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Mara, Geita, Arusha na Songwe mauaji, kujeruhiwa na uharibifu mkubwa wa mali tayari ulikuwa umetokea. Mambo ambayo kwakweli yameziacha pande zote za jamii yetu kuwa ni sehemu ya lawama kwa haya yaliyotokea.

Kwanza ni upande wa waandamanaji; kudai katiba mpya, kudai tume huru ya uchaguzi, kudai kukomeshwa kwa utekaji pamoja na kupinga ufisadi ni mambo ambayo ni ya msingi na yanazungumzika. Lakini kujeruhi, kuua, kuiba, kuchoma mali za watu, kuharibu miundombinu ya serikali huo ni uharifu kama uharifu mwingine, na kwakweli kwa waliothibitika kufanya hivyo ni wazi watakutana na mkono wa sheria. Wakati mwingine ikitokea hoja na haja ya kuandamana, kama ilivyo ni haki ya kikatiba, ni sharti kila muandamanaji awe mlinzi wa mwenzake kuhakikisha maandamano hayo yanabaki kwenye agenda yake na sio kufungua mlango wa uvunjifu wa sheria, vinginevyo police watakuwa na "reasonable excuse" ya kuzuia kuwepo kwa maandamano yoyote yale.

Pili ni vyombo vya ulinzi na usalama; kwa dhati ya moyo wangu kwenye hili mm siwapongezi. Haiingii akilini hata kidogo, jambo ambalo tishio lake limekuwepo wazi kwa zaidi ya miezi kadhaa likatokea kama lilivyopangwa na kuleta madhila haya. Tutafakari, Jeshi la polisi hususani kitengo cha doria mtandaoni, Je, hakikuiona hii mipango ya maandamano mitandaoni? Je, kilichukua hatua gani kudhibiti uchochezi uliokuwa ukiendelea? TISS, Je, hawakuwa informed na haya maandamano? Je, walichukua hatua gani kuyadhibiti kabla hayajatokea? Idara ya uhamiaji, kama ni kweli wapo wageni walioshiriki kuleta machafuko, wao walikua wapi mpaka wageni wameingia? Ukweli ulio wazi ni kuwa vyombo vyetu vili "underestimate" threat. Madhara yake ndio hayo tunayoyaona, hatimaye ikahitajika nguvu kubwa kutumika kudhibiti ghasia. Kwa akina siye tuliokuwa tumejifungia ndani pengine sio sawa kushauri nini kingefanyika, maana hatukuwepo kwenye uwanja wa mapambano, ila maoni ya wengi ni kuwa mabomu ya machozi na maji ya washawasha yangeweza kuwa mbadala wa risasi za moto ambazo zimesababisha mauaji na majeruhi kwa waandamanaji na wasio waanamanaji. Mwisho itoshe kusema, tunamshukuru Mungu sasa utulivu umerejea.

Tatu ni INEC na Msajili wa vyama vya siasa. Chanzo kikuu cha yote haya kilianzia na vyama vya upinzani mathalani CHADEMA kudai hawatendewi haki. Hiki ndicho kilichozaa "No reforms, No election" Karibu vyama vyote vikubwa kwa nyakati tofauti vimeilalamikia ofisi ya Msajili na INEC kutokutenda haki. Changamoto ya kuwepo kwa malalamiko yanayopuuzwa kwa muda mrefu ni kuzaliwa kwa uasi. Inapofikia hatua hii kuendelea kuwa wababe kwavyovyote vile kutazaa machafuko. Mpaka hivi sasa sioni sababu na siamini kama kulikuwa na ulazima wa tume kutunishiana misuli na CHADEMA kuhusu kanuni za uchaguzi au Msajili kuelekeza Mpina akatwe. Wakati mwine tunahitaji hekima na busara zaidi kushughulika na migogoro kuliko kusingizia sheria ambazo sisi wenyewe tunao uwezo wa kuzibadilisha.

Nne ni CCM na serikali; hawa nawaweka pamoja kwani katika hoja za kisiasa wao ni kitu kimoja. CCM wamekuwa na kawaida ya kujitathimini angalau kila baada ya uchaguzi mkuu, ni imani yangu, baada ya uchaguzi huu watajitathmini pia, hususani kuhusu yaliyotokea. Kwa maoni yangu, machafuko haya, msingi wake ni hoja za kisiasa ambazo CCM ama haikubaliani nazo au hazijajibiwa na kufafanuliwa vya kutosha. Kwa mfano; Balozi Polepole alimtuhumu Rostam kujinyakuli mgodi wa makaa ya mawe na mwingine wa almasi. Rostam alijitokeza, akaeleza kuwa migodi hii iliinunua kwa wawekezaji, sio kutoka serikalini, baada ya hapo hoja hii ilikufa. Sasa, Angela Kiziga alikwama wapi kutoka na kusafisha hali ya hewa? Rais halindwi kwa bunduki tu, haiba yake pia inapaswa kulindwa! Hii ndio sababu Rais Kikwete alimwambia Prof. Tibaijuka ampishe! Inapotokea msaidizi wa Rais kusemwa ni vizuri majibu yanayojitosheleza yakatolewa, vinginevyo tutakuwa tunaharibu haiba ya Rais wetu. Hoja zisizojibiwa ndizo zinazozipa post za akina Mange nguvu na kuonekana kama zina ukweli. Tutafakari, hivi ni kweli kuwa hatuna majibu ya hoja za Bishop Gwajima mpaka tufunge makanisa yake? Je, hatuna majibu kwa hoja za CHADEMA, angalau japo kwa kiasi ambazo zingetufanya tushikane mkono na mambo yakiendelea? Changamoto kubwa tuliyonayo, hoja zinapoibuliwa na wapinzani wetu, badala ya kuzijibu tunawakeleli na kuwadhihaki. Mm nadhani, ingawa CCM ndio wengi, haitapoteza chochote kwa kuwasikiliza wapinzani wake, hata kama ni kwa kiasi ilimradi tupate maridhiano yatakayodumisha utengamano wetu.

Tano na mwisho ni vyama vya upinzani hususani CHADEMA. Haya maandamano ni zao la mwisho ya campaign ya "No reforms, no election" Swali la msingi tujiulize tumenufaika nini kwa haya yaliyotokea? Vurugu hazina mshindi, maadam mmeamua kufanya siasa hamna budi kuwa wavumilivu na wastahimilivu. Rais wa Zambia, ndugu Hakainde Hichilema aliwaasa akisema, yeye amekuwa mpinzani kwa miaka mingi, amepoteza chaguzi nyingi, lakini hata alipohisi kuibiwa hakupeleka watu barabarani na hatimaye sasa ni Rais. Ni vyema tukajijengea utamaduni wa kumaliza sintofahamu zetu kwenye meza ya mazungumzo.

Ni imani yangu sasa tumejifunza wapi tulipoangukia, sasa tuinuke na tusonge mbele.
unaelewa maana ya No reforms, no election" ?!
 
Mbona hilo lipo wazi comrade! Police are not immune to criminal litigation. Kwamujibu wa sheria zetu police akiua anashitakiwa kwa murder case.
Aidha katika makala haya nimeeleza kutokuridhishwa kwangu na namna vyombo vyetu vilivyo shughulika na hili jambo zima mpaka limetokea kwa jinsi lilivyotokea.
You don't have to think too much juu ya hili

Huhitaji kutumia nguvu kubwa kufikiri juu ya chanzo cha tatizo na suluhu yake

Chanzo cha yote haya ni Bi Samia Suluhu Hassan, CCM na serikali yao kuwa na kiburi na dharau ya kutosikiliza sauti za wananchi wanataka nini!

Nyie kina Dr Adam Francis ndio hasa mliokuwa na actually ambao mpaka leo hamuelewi kwanini CHADEMA walikuja na madai ya kudai electoral reforms kwanza kabla ya kuingia kwenye uchaguzi chini ya political slogan ya NO REFORMS NO ELECTION.

It was simply because mfumo wa uchaguzi uliopo sasa una kasoro na matatizo makubwa yasiyoweza kutoa haki sawa kwa washiriki wote wa uchaguzi Ili kupata viongozi halali wenye ridhaa ya wananchi kuongoza taifa hili. Haya mauaji na uharibifu wa mali tuliouona na kushuhudia ndio matokeo na matunda ya mfumo huu mbovu wa uchaguzi na walio madarakani hawataki kuliona tatizo hata kama liko wazi mbele ya macho yao. Je, wasilaumiwe?

Kama unarusha lawama, basi unapaswa kuzilaumu mamlaka za kiusalama TISS na TANPOL kushindwa kutoa ushauri sahihi kwa mamalaka za kutoa maamuzi hususani Rais juu ya hatari iliyokuwa mbele kwa kulazimisha kufanya uchaguzi katika mazingira yaliyojaa dhuluma na kunyima haki wananchi kushiriki uchaguzi huru, haki, wazi na wa kuaminika na kukubalika na pande zote

Watu wengi wazuri, wenye hekima, busara, ufahamu na wenye kuona mbele walitoa maonyo mapema kabisa juu kitendo chochote cha kuchezea tendo la uchaguzi na kupuuza sauti za wananchi

Lakini majibu ya watawala wakisaidiwa na Polisi kina Jumanne Muliro ilikuwa ni kejeli, dharau na kubagaza sauti za wenye nchi - wananchi huku wakiapa kuvunja miguu ya yeyote atakayeendelea kuipinga serikali 🤷🏼‍♀️🤷🏼‍♀️🤷🏼‍♀️

Aidha ilionywa mapema kabisa kuwa, machafuko ktk nchi nyingi hutokea pale serikali zinapodharau na kutosikiliza sauti za wananchi wanataka nini.

Leo Tanzania ni kila anayekosoa mwenendo na matendo ya viongozi wa serikali anapigwa chapa ya "CHADEMA". That's completely ridiculous na ndio maana taifa na nchi yetu imechafuka na kunuka dunia nzima...

Kuthibitisha kuwa, hatuna watu wenye akili, busara na hekima serikalini, angalia hatua wanazochukua sasa kama namna ya kutatua tatizo lililopo.

Cha ajabu na wewe unayejiita Dr Adam Francis unapendekeza ujinga huohuo wanaofanya serikali wakidhani ni suluhu ya tatizo wasijue kuwa, wanamwaga petrol kwenye moto unaowaka tayari

Tungekuwa na serikali yenye viongozi wenye hekima na busara, cha kwanza kufanya baada ya mauaji yaliyofanyika ni kuomba msamaha na kutoa pole za dhati

Lakini badala ya kufanya hivi, wao wanawatafuta waliokuwa wanadai haki zao Ili eti wawashitaki kwa kusababisha vurugu na upotevu mali!!!

Haiwatafuti walioshika bunduki zao na kuua watu wasio na silaha badala yake serikali inawatafuta walio na msiba na kufiwa na ndugu zao Ili eti wawashitaki kwa kuvuruga amani.

Hebu niambie kwa dhati ya moyo na nafsi yako Dr Adam Francis, kwamba, Is that the right approach to heal the nation after the bloodshed of the thousands of innocent citizens?

Sikiliza ndugu Dr Adam Francis. The burden of shame, blames lie on shoulders of the President of URT, CCM and their counterparts. They're 100% responsible to the every blood drop💧 buried in the soili and for every destructions of humanity and property occured by failing to prevent this at the firsthand.

Kiburi na dharau ya Bi Samia na CCM yake itawaua na wao

Na wasifikiri hali imetulia, mambo yamekwisha. This is the beginning of their final end!!
 
Hoja ya Tume ya Uchaguzi kuipendelea ccm kwa kila kitu hadi kuiba kura imezungumzwa sana na wapinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Hoja hiyo imekuwa ikipuuzwa na viongozi wa ccm wakijitahidi kuisikiliza wanakuja na janjajanja nyingi sana. Hata kiburi cha mkurugenzi wa uchaguzi Kairima kutangaza kwamba chadema haitashiriki uchaguzi kwa miaka mitano kutokana na kukataa kusaini maadili ya uchaguzi ni kiburi tu cha 'watatufanya nini'.
Kilio cha tume kuchakachua uchaguzi ilikuwa ni ishara tosha kwamba tanzania itakuja kuingia kwenye machafuko huko mbeleni. Hili suala la kuchakachua uchaguzi wala sio kwa maslahi ya taifa ni ubinafsi tu wa viongozi wa ccm kwamba wao ndo wanastahili kuchaguliwa. Angalia hata matokeo ya samia mwaka huu, tume wamejiamulia tu kwamba hesabu ziwe hivyo basi wakatangaza, wao wanadhani wanamsadia rais lakini hawajui kwamba wanatengeneza bomu la hapo baadaye.
 
Nadhani kuna kila sababu sasa CCM kukubaliana na wapinzani wake kama tuna nia ya dhati kuepuka machafuko tena.
 
You don't have to think too much juu ya hili

Huhitaji kutumia nguvu kubwa kufikiri juu ya chanzo cha tatizo na suluhu yake

Chanzo cha yote haya ni Bi Samia Suluhu Hassan, CCM na serikali yao kuwa na kiburi na dharau ya kutosikiliza sauti za wananchi wanataka nini!

Nyie kina Dr Adam Francis ndio hasa mliokuwa na actually ambao mpaka leo hamuelewi kwanini CHADEMA walikuja na madai ya kudai electoral reforms kwanza kabla ya kuingia kwenye uchaguzi chini ya political slogan ya NO REFORMS NO ELECTION.

It was simply because mfumo wa uchaguzi uliopo sasa una kasoro na matatizo makubwa yasiyoweza kutoa haki sawa kwa washiriki wote wa uchaguzi Ili kupata viongozi halali wenye ridhaa ya wananchi kuongoza taifa hili. Haya mauaji na uharibifu wa mali tuliouona na kushuhudia ndio matokeo na matunda ya mfumo huu mbovu wa uchaguzi na walio madarakani hawataki kuliona tatizo hata kama liko wazi mbele ya macho yao. Je, wasilaumiwe?

Kama unarusha lawama, basi unapaswa kuzilaumu mamlaka za kiusalama TISS na TANPOL kushindwa kutoa ushauri sahihi kwa mamalaka za kutoa maamuzi hususani Rais juu ya hatari iliyokuwa mbele kwa kulazimisha kufanya uchaguzi katika mazingira yaliyojaa dhuluma na kunyima haki wananchi kushiriki uchaguzi huru, haki, wazi na wa kuaminika na kukubalika na pande zote

Watu wengi wazuri, wenye hekima, busara, ufahamu na wenye kuona mbele walitoa maonyo mapema kabisa juu kitendo chochote cha kuchezea tendo la uchaguzi na kupuuza sauti za wananchi

Lakini majibu ya watawala wakisaidiwa na Polisi kina Jumanne Muliro ilikuwa ni kejeli, dharau na kubagaza sauti za wenye nchi - wananchi huku wakiapa kuvunja miguu ya yeyote atakayeendelea kuipinga serikali 🤷🏼‍♀️🤷🏼‍♀️🤷🏼‍♀️

Aidha ilionywa mapema kabisa kuwa, machafuko ktk nchi nyingi hutokea pale serikali zinapodharau na kutosikiliza sauti za wananchi wanataka nini.

Leo Tanzania ni kila anayekosoa mwenendo na matendo ya viongozi wa serikali anapigwa chapa ya "CHADEMA". That's completely ridiculous na ndio maana taifa na nchi yetu imechafuka na kunuka dunia nzima...

Kuthibitisha kuwa, hatuna watu wenye akili, busara na hekima serikalini, angalia hatua wanazochukua sasa kama namna ya kutatua tatizo lililopo.

Cha ajabu na wewe unayejiita Dr Adam Francis unapendekeza ujinga huohuo wanaofanya serikali wakidhani ni suluhu ya tatizo wasijue kuwa, wanamwaga petrol kwenye moto unaowaka tayari

Tungekuwa na serikali yenye viongozi wenye hekima na busara, cha kwanza kufanya baada ya mauaji yaliyofanyika ni kuomba msamaha na kutoa pole za dhati

Lakini badala ya kufanya hivi, wao wanawatafuta waliokuwa wanadai haki zao Ili eti wawashitaki kwa kusababisha vurugu na upotevu mali!!!

Haiwatafuti walioshika bunduki zao na kuua watu wasio na silaha badala yake serikali inawatafuta walio na msiba na kufiwa na ndugu zao Ili eti wawashitaki kwa kuvuruga amani.

Hebu niambie kwa dhati ya moyo na nafsi yako Dr Adam Francis, kwamba, Is that the right approach to heal the nation after the bloodshed of the thousands of innocent citizens?

Sikiliza ndugu Dr Adam Francis. The burden of shame, blames lie on shoulders of the President of URT, CCM and their counterparts. They're 100% responsible to the every blood drop💧 buried in the soili and for every destructions of humanity and property occured by failing to prevent this at the firsthand.

Kiburi na dharau ya Bi Samia na CCM yake itawaua na wao

Na wasifikiri hali imetulia, mambo yamekwisha. This is the beginning of their final end!!
Kwasehemu kubwa nakubaliana na hoja zako. Ila si kweli kuwa CCM wamegoma kuwasikiliza wananchi. Mapungufu yapo, ila ni ukweli ulio wazi kuwa jitihada kadhaa za kuwepo maridhiano zimefanyika, mkwamo tulionao ni kila upande kushikilia msimamo wake. Panapo fuka moshi ni wazi kuwa pana moto. Ni jukumu la mamlaka kujitathimini na kujisahihisha kama wanayo nia ya dhati ya kuepuka kujirudia kwa yaliyotokea
 
Back
Top Bottom