Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Mficha maradhi kifo humuumbua. Huu ndio ukweli ulioniongoza kuandika tafakuri hii kuhusu October 29 angalau tujifunze jambo la kutusaidia baadaye.
Nini kilitokea October 29, hautakuwa mjadala wangu wa leo. Utashi wangu unaniongoza kuwa hiyo si habari mpya tena, kila mtanzania aidha ameathirika yeye mwenyewe, au ameona kwa macho, au amesikia habari au ameonja joto la lock down, internet shutdown pamoja na kufungwa kwa biashara ya petrol. Mjadala wangu leo utakuwa tulifikaje hapo?
Vuguvugu kuhusu kuwepo kwa maandamano katika siku tajwa lilianza muda mrefu, kwa maoni yangu, tangu CHADEMA wamalize uchaguzi mkuu wao pale mlimani city. Pale campaign ya "No reforms, No election" ndipo ilipohuishwa. Kama hatua ya kujibu mapigo CCM, wakaja na "Oktoba Tunatiki"
Itakumbukwa hata Kikwete alizitambua "No reforms, No election " na "Octoba Tunatiki" kama ndizo kambi zilizokuwa na ushindani wa kweli kuelekea October 29. Ni wazi kuwa matokeo ya uchaguzi huu, kipimo chake hakikua nani amechaguliwa bali kama uchaguzi umefanyika au haujafamyika, pengine ndio sababu INEC wamekuja na takwimu ya kura milioni 32.
No reforms, No election ilianza kupata sura mpya baada ya Bishop Gwajima kujitokeza kusema kipo kikundi "untouchable" kinachoratibu utekaji wa watu, akafuatiwa na Balozi Polepole kupinga uteuzi wa Rais Samia kupeperusha bendera ya CCM akimtuhumu kukiuka utaratibu na kuwalinda watu aliowatuhumu kuwa mafisadi, baadae akajitokeza Captain Tesha kutaka jeshi lizuie uchaguzi kwa madai hayo hayo ya kuwepo ufisadi na ukiukwaji wa demokrasia na mwisho Mange kuwahimiza watanzania waandamane kuchukua nchi yao akidai ufisadi umekithiri serikalini. Kwa maoni yangu, hayo ndiyo yaliyochochea maandamano ya October 29.
Jambo la kushangaza ni kuwa, pamoja na kuwa taarifa hizi zilikuwa wazi mitandaoni kwa muda mrefu, vurugu zilipoanza ilikuwa ni kama tulishitukizwa vile, kwani mpaka zinadhibitiwa tayari katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Mara, Geita, Arusha na Songwe mauaji, kujeruhiwa na uharibifu mkubwa wa mali tayari ulikuwa umetokea. Mambo ambayo kwakweli yameziacha pande zote za jamii yetu kuwa ni sehemu ya lawama kwa haya yaliyotokea.
Kwanza ni upande wa waandamanaji; kudai katiba mpya, kudai tume huru ya uchaguzi, kudai kukomeshwa kwa utekaji pamoja na kupinga ufisadi ni mambo ambayo ni ya msingi na yanazungumzika. Lakini kujeruhi, kuua, kuiba, kuchoma mali za watu, kuharibu miundombinu ya serikali huo ni uharifu kama uharifu mwingine, na kwakweli kwa waliothibitika kufanya hivyo ni wazi watakutana na mkono wa sheria. Wakati mwingine ikitokea hoja na haja ya kuandamana, kama ilivyo ni haki ya kikatiba, ni sharti kila muandamanaji awe mlinzi wa mwenzake kuhakikisha maandamano hayo yanabaki kwenye agenda yake na sio kufungua mlango wa uvunjifu wa sheria, vinginevyo police watakuwa na "reasonable excuse" ya kuzuia kuwepo kwa maandamano yoyote yale.
Pili ni vyombo vya ulinzi na usalama; kwa dhati ya moyo wangu kwenye hili mm siwapongezi. Haiingii akilini hata kidogo, jambo ambalo tishio lake limekuwepo wazi kwa zaidi ya miezi kadhaa likatokea kama lilivyopangwa na kuleta madhila haya. Tutafakari, Jeshi la polisi hususani kitengo cha doria mtandaoni, Je, hakikuiona hii mipango ya maandamano mitandaoni? Je, kilichukua hatua gani kudhibiti uchochezi uliokuwa ukiendelea? TISS, Je, hawakuwa informed na haya maandamano? Je, walichukua hatua gani kuyadhibiti kabla hayajatokea? Idara ya uhamiaji, kama ni kweli wapo wageni walioshiriki kuleta machafuko, wao walikua wapi mpaka wageni wameingia? Ukweli ulio wazi ni kuwa vyombo vyetu vili "underestimate" threat. Madhara yake ndio hayo tunayoyaona, hatimaye ikahitajika nguvu kubwa kutumika kudhibiti ghasia. Kwa akina siye tuliokuwa tumejifungia ndani pengine sio sawa kushauri nini kingefanyika, maana hatukuwepo kwenye uwanja wa mapambano, ila maoni ya wengi ni kuwa mabomu ya machozi na maji ya washawasha yangeweza kuwa mbadala wa risasi za moto ambazo zimesababisha mauaji na majeruhi kwa waandamanaji na wasio waanamanaji. Mwisho itoshe kusema, tunamshukuru Mungu sasa utulivu umerejea.
Tatu ni INEC na Msajili wa vyama vya siasa. Chanzo kikuu cha yote haya kilianzia na vyama vya upinzani mathalani CHADEMA kudai hawatendewi haki. Hiki ndicho kilichozaa "No reforms, No election" Karibu vyama vyote vikubwa kwa nyakati tofauti vimeilalamikia ofisi ya Msajili na INEC kutokutenda haki. Changamoto ya kuwepo kwa malalamiko yanayopuuzwa kwa muda mrefu ni kuzaliwa kwa uasi. Inapofikia hatua hii kuendelea kuwa wababe kwavyovyote vile kutazaa machafuko. Mpaka hivi sasa sioni sababu na siamini kama kulikuwa na ulazima wa tume kutunishiana misuli na CHADEMA kuhusu kanuni za uchaguzi au Msajili kuelekeza Mpina akatwe. Wakati mwingine tunahitaji hekima na busara zaidi kushughulika na migogoro kuliko kusingizia sheria ambazo sisi wenyewe tunao uwezo wa kuzibadilisha.
Nne ni CCM na serikali; hawa nawaweka pamoja kwani katika hoja za kisiasa wao ni kitu kimoja. CCM wamekuwa na kawaida ya kujitathimini angalau kila baada ya uchaguzi mkuu, ni imani yangu, baada ya uchaguzi huu watajitathmini pia, hususani kuhusu yaliyotokea. Kwa maoni yangu, machafuko haya, msingi wake ni hoja za kisiasa ambazo CCM ama haikubaliani nazo au hazijajibiwa na kufafanuliwa vya kutosha. Kwa mfano; Balozi Polepole alimtuhumu Rostam kujinyakuli mgodi wa makaa ya mawe na mwingine wa almasi. Rostam alijitokeza, akaeleza kuwa migodi hii iliinunua kwa wawekezaji, sio kutoka serikalini, baada ya hapo hoja hii ilikufa. Sasa, Angela Kiziga alikwama wapi kutoka na kusafisha hali ya hewa? Rais halindwi kwa bunduki tu, haiba yake pia inapaswa kulindwa! Hii ndio sababu Rais Kikwete alimwambia Prof. Tibaijuka ampishe! Inapotokea msaidizi wa Rais kusemwa ni vizuri majibu yanayojitosheleza yakatolewa, vinginevyo tutakuwa tunaharibu haiba ya Rais wetu. Hoja zisizojibiwa ndizo zinazozipa post za akina Mange nguvu na kuonekana kama zina ukweli. Tutafakari, hivi ni kweli kuwa hatuna majibu ya hoja za Bishop Gwajima mpaka tufunge makanisa yake? Je, hatuna majibu kwa hoja za CHADEMA, angalau japo kwa kiasi ambazo zingetufanya tushikane mkono na mambo yakiendelea? Changamoto kubwa tuliyonayo, hoja zinapoibuliwa na wapinzani wetu, badala ya kuzijibu tunawakejeli na kuwadhihaki. Mm nadhani, ingawa CCM ndio wengi, haitapoteza chochote kwa kuwasikiliza wapinzani wake, hata kama ni kwa kiasi ilimradi tupate maridhiano yatakayodumisha utengamano wetu.
Tano na mwisho ni vyama vya upinzani hususani CHADEMA. Haya maandamano ni zao la mwisho ya campaign ya "No reforms, no election" Swali la msingi tujiulize tumenufaika nini kwa haya yaliyotokea? Vurugu hazina mshindi, maadam mmeamua kufanya siasa hamna budi kuwa wavumilivu na wastahimilivu. Rais wa Zambia, ndugu Hakainde Hichilema aliwaasa akisema, yeye amekuwa mpinzani kwa miaka mingi, amepoteza chaguzi nyingi, lakini hata alipohisi kuibiwa hakupeleka watu barabarani na hatimaye sasa ni Rais. Ni vyema tukajijengea utamaduni wa kumaliza sintofahamu zetu kwenye meza ya mazungumzo.
Ni imani yangu sasa tumejifunza wapi tulipoangukia, sasa tuinuke na tusonge mbele.
View: https://vm.tiktok.com/ZMATLExe5/