Norton82
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 721
- 620
Tarehe 01 Oktoba 2019 , mlifanya mkutano na wanakijiji kata ya Malolo wilaya ya kilosa, na wanakijiji hao walikusanywa na Diwani wa kata ya Malolo na afisa mtendaji wa kata ya Malolo, zikaibuliwa tuhuma na mkulima mmoja kuwa ng'ombe za wafugaji zinakula kwenye mashamba ya wakulima, lakini cha ajabu zaidi hao waliowakusanyia watu muongee nao ndiyo umetoa amri wakae ndani,
Ndugu zao wakifika kituo cha polisi, polisi hawatoi ushirikiano, wanajifanya wako busy, na miongoni mwa wafugaji waliokamatwa wanasema waliotakiwa kukamatwa wameachwa wamekamatwa wasiostahili , lakini cha kusikitisha zaidi mkatoa madai ya kwamba kituo cha polisi mikumi kimejaa na wanatakiwa wapelekwe Kituo cha polisi K1Ruaha, lakini askari waaminifu, wamesema hapo kituoni nafasi bado ipo,
Jambo la kuzingatia fanya kazi kwa kufuata misingi ya kazi yako, vinginevyo dunia sasa hivi ni kama kijiji,usifikiri kwa kufanyia kazi katika maeneo ya pembeni ya nchi ndiyo mwanya wa kujifanyia mambo unavyoona wewe inafaa, hao wafugaji kama wana makosa wapelekeni mahakamani ila kama hawana makosa muwaachie kwa amani.
Na katika hili ifahamike hatuitaji migogoro ya wakulima na wafugaji ila kuonekane haki ikitendeka baina ya pande hizo mbili.
Ni mimi mwanakijiji mtiifu