OCD au OCS anapokataa kumtolea mtu mdhamana

spacing

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
265
110
Naomba nifunguke wakuu,

Kuna jamaa yangu kawekwa lockup almost five days kwa kosa la kumdhamini mtoto wake aliyekuwa anafanya kazi ya ununuzi wa pamba katika kampuni fulan.

Kampuni liko mkoa wa Singida, watuhumiwa ni wakaaji wa mkoa Shinyanga Kishapu, mlalamikaji(agent wa kampun) kamuweka lockup katika kituo cha polisi cha
Kishapu takribani siku tano.

OCS wa
Kishapu hataki mtu adhamini kisa file liko Singida. Mtuhumiwa hapelekwi Singida anasota tu lockup,
 
Hivi nini kifanyike ili mtu apate mdhamana kama hawa watu hawataki kuruhusu mtuhumiwa awekewe mdhamana kwa civil criminal

uko wapi mkuu,muone mkuu wa wilaya huyo ndo mwenyekiti wa usalama wilaya.kama uko usukumani najua huwez coz ngosha waoga sana hata kama ni haki yake
 
Dhamana ni lazima.ikifika saa 48,lazima mtuhumiwa akashtakiwe mahakamani au apewe dhamana akisuburi kupelekwa mahakamani
 
Hakuna civil criminal case. Halafu,dhamana ya kituo cha polisi au mahakama si lazima kutolewa. Kuna vigezo na hoja za kujenga
 
uko wapi mkuu,muone mkuu wa wilaya huyo ndo mwenyekiti wa usalama wilaya.kama uko usukumani najua huwez coz ngosha waoga sana hata kama ni haki yake

tatizo siyo kabila,kuna ukiukwaji tu wa kanuni na sheria za nchi,mtu huwez kung'ang'ania akae lock up wakati hata jinai wanatoa mdhamana
 
Polisi hili walitizame upye.. kuna ukakasi mkubwa sana kwenye dhamana ya watuhumiwa... kumbukeni hawa ni watuhumuwa tu bado msiwahukum kabla....
 
civil criminal ndo nn? Dhamana ni haki ya MTU tena ya kikatiba, makosa yenye kutopewa dhamana ni kosa la mauaji,uhaini,uhujumu uchumi,money laundering, wizi wa kutumia silaha (robbery), madawa ya kulevya,. makosa mengine yanadhamana.kutokumpa mtu dhamana ni kukiuka katiba na haki za binadamu.
 
mlalamikaji anapokuwa karibu na hawa watu mtuhumiwa ananyimwa haki kwa makusudi kabisa
 
hujasomeka mkuu,hata jinai wanatoa dhamana

ndg yangu usiwe unapinga kila kitu. Dhaman ni haki ya mtuhumiwa lakn utambuew kuwa sio kila mtuhumiwa anastahili dhamana. Kuna mengne kutokana na aina ya ushahidi unavyotafutwa mtuhumiwa ananyimwa dhamana ili kuepuka kupoteza ushahidi.
 
sawa,lakini kwa mda gani??
 
Hivi nini kifanyike ili mtu apate mdhamana kama hawa watu hawataki kuruhusu mtuhumiwa awekewe mdhamana kwa civil criminal

mkuu hawa jamaa wana njaa sana kama vipi mwanga unga hadharani ni ocs wa wap na ni kesi gani anakusumbua
 
majipu kama haya yakitumbuliwa raia watakuwa na ahuen sana,si kila aendaye lockup ana makosa,is just a suspect
 
Pole sana mwananchi mwenzangu kwa matatizo yanayokusibu ila ili nikupe msaada wa kisheria inabidi uweke wazi kesi inayomkabili ndugu yako na siyo kama hivyo ulivyoeleza criminal civil kwakuwa haileti maana yoyote.Pia weka kwenye akili yako kuwa kuna vigezo vimewekwa ili upewe dhamana ya polisi.kumbuka tu kila penye haki pana wajibu hivyo usishangae kuikosa haki yako usipotimiza wajibu wako.
 
Back
Top Bottom