Obby anapoanza kutapatapa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,927
22,077
Obama aanza kusaka raia wa kigeni Marekani Send to a friend Wednesday, 11 May 2011 21:25 0diggsdigg

WASHINGTON, Marekani
RAIS Barack Obama wa Marekani,ameamua kuimarisha ulinzi wa nchi yake na tayari ametangaza mageuzi makubwa na ya haraka, katika mfumo wa uhamiaji.Hatua hiyo, inakuja wiki moja baada ya Kikosi Maalumu cha Jeshi la Marekani, kumuua aliyekuwa akiongozi wa Kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, katika mji wa Abbottabad, nchini Pakistani.

Akizungumza katika Jimbo la Texas juzi, Rais Obama alilitaka Bunge la nchi hiyo, kuwachambua raia wanaoishi Marekani kwa kuhamia, ili kujiridhisha na uhalali wao.Inasemekana kwa sasa Marekani ina watu milioni 11 wanaoishi kama raia wa kuhamia.Hata hivyo, Rais Obama ametaka watu hao wafuatiliwe upya na kuthibitishwa uraia wao.

"Tuna nguvu na ulinzi wa kutosha katika mipaka ya nchi yetu hata watu wengi wanaamini hivyo. Kilichobaki ni kuwaoatia vibali wahamiaji wanaoishi hapa nchini kwetu,"alisema kiongozi huyo wa Marekani.

Rais Obama alisema mageuzi katika mfumo ya uhamiaji, pia yataleta manufaa ya kiuchumi kwa watu wa tabaka la kati na katika nyanja ya biashara.Alisema mageuzi ya mfumo huo, yataimarisha pia usalama wa kitaifa.
Alisema kwa sasa sera ya uhamiaji ya Marekani si nzuri na kwamba inapaswa kufanyiwa marekebisho ya haraka hasa ikizuingatiwa kuwa Marekani ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya wageni wanaotaka kupewa uraia wa kudumu.

Obama alisema hiki ni kipindi cha kila mtu kuangalia uchumi na kwa msingi huo, sera ya uhamiaji lazima izingatie hilo na kwamba kuwanyima watu vibali, ni kuzorotesha uchumi wa nchi.Alisema sekta ya uhamiaji ni ya muhimu katika kila nchi inayowajali watu wanaohamia wakiwa wana kila sifa ya kupewa vibali.

Wakati huo huo, Marekani imeimarisha msimamo wake wa kuikosoa vikali China kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Washington.Akizungumza mwishoni mwa mkutano huo wa siku mbili wa kila mwaka kati ya nchi hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema nchi hizo zinapaswa kuzungumzia wazi wazi tofauti zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Clinton aliilaumu China kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba nchi hiyo, itakuwa inafanya makosa ikifikiri inaweza kuzuia mageuzi huku maandamano ya kupigania demokrasia yakiendelea katika mataifa ya kiarabu.
Katika mkutano huo, Marekani pia ilisaini mkataba na China kuhusu uchumi unaonuiwa kuboresha uhusiano kati ya dola hizo kuu kiuchumi duniani.
 
Na kama anataka mwisho wa dunia aguse upuuzi wake china aone
 
Na kama anataka mwisho wa dunia aguse upuuzi wake china aone

yaani aanzishe vta na china ama awatoe wachina wote wanaoishi usa.
Nwy me nahc ni woga tu Obama anao after UBL kuuwawa (not surely) i think al kaida comes 2 revange 4 their lost man of hope.
 
China needs US for its exports. US needs China for its cheap imports. Both US and China needs each other. Hakuna ubishi.
Huyo mwandishi wa Mwananchi alietafsiri hiyo habari nafikikiri ana mapungufu makubwa ktk translation na analysis. Naona taaluma ya journalism imevamiwa na vilaza.
Obama juzi alikuwa TX kwenda kuipigia debe kule Congress ile issue ya legalization of apprx. 12 million illegal aliens currently living in the US mostly latinos. Na amefanya hivyo makusudi ili kuwabana GOP na kutafuta support ya latino votes in 2012
Sasa huko kutapatapa kunakuja wapi?
Ama ndio hizo hasira zenu kwa kuwa Osama kaliwa na samaki? Na hao wazee wa mafeki (China)nyie mnawaona wa maana sana kwa kutuletea na kutujazia mafeki, madanguro,na wamachinga hapo bongo na kutujengea barabara zinazoumuka kama zimetiwa hamira?
Hawana mpya zaidi ya kuiibia Africa na hasa TZ. Elimikeni
 
Na kama anataka mwisho wa dunia aguse upuuzi wake china aone

Pdidy umeona hilo... Nashangaa hata wana jamii wengi kua na confidence kubwa saana kwa US kua China hawezi react... wale watu ndo saizi yao US... Waarabu wameshindwa because hawana umoja wala hawajitambui, maana wangekua wanajitambua US angekua hawagusi... But hata hivyo naona all for the best maana hypothetically speaking siku mwarabu akija kua a world power... we will immediately cease to exist...
 
Oooooyeeaaaahhhh aisha
hapo ume nena mi nakwambia natamani kweli aonje asali ya china aone moto wake..nafikiri obby kajisahau kidogo
 
Mimi sijaona kama Obama hapo anatapatapa, bali animarisha usalama na ulinzi wa nchi yake kwa kuelekeza kuchambuliwa na kutoa vibali kwa wahamiaji wanoishi katika nchi yake kihalali. Wale ambao sio halali warudishwe kwao au wafuate taratibu nzuri kuomba uraia. Kuna nchi yoyote inayoruhusu watu kuingia na kuishi kiholela?
 
China needs US for its exports. US needs China for its cheap imports. Both US and China needs each other. Hakuna ubishi.
Huyo mwandishi wa Mwananchi alietafsiri hiyo habari nafikikiri ana mapungufu makubwa ktk translation na analysis. Naona taaluma ya journalism imevamiwa na vilaza.
Obama juzi alikuwa TX kwenda kuipigia debe kule Congress ile issue ya legalization of apprx. 12 million illegal aliens currently living in the US mostly latinos. Na amefanya hivyo makusudi ili kuwabana GOP na kutafuta support ya latino votes in 2012
Sasa huko kutapatapa kunakuja wapi?
Ama ndio hizo hasira zenu kwa kuwa Osama kaliwa na samaki? Na hao wazee wa mafeki (China)nyie mnawaona wa maana sana kwa kutuletea na kutujazia mafeki, madanguro,na wamachinga hapo bongo na kutujengea barabara zinazoumuka kama zimetiwa hamira?
Hawana mpya zaidi ya kuiibia Africa na hasa TZ. Elimikeni

I concur enterely!
 
Wanaweza kuwa na silaha feki hao!!!

haaa!
Si umeona ile chopper ya US ilioanguka kule Pakistani jinsi wanavyoiwinda ili wai-copy? Badala ya kubuni zenu mnavizia mpaka kwenda kukopi za wenzenu? Hawa wazee wa mafeki kila kitu urojooo tu
 
Back
Top Bottom