Obasanjo: Ufisadi ni tatizo kubwa Afrika

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Obasanjo: Ufisadi ni tatizo kubwa Afrika

na
Kulwa Karedia na Ramadhan Siwayombe, Arusha
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

RAIS mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, jana alitoa kauli nzito dhidi ya viongozi wa Afrika na kuwataka kupambana na rushwa katika nchi zao, hata kama zinawahusu viongozi wakuu waliopo madarakani na wale waliostaafu ndani ya nchi zao.

Obasanjo aliyasema hayo wakati akitoa nasaha katika siku ya kwanza ya mkutano wa nane wa Leon Sullivan, unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), kabla haujafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete jana jioni.

"Ili mataifa ya Afrika yaweze kupata maendeleo lazima viongozi wake wakubali kupambana na wala rushwa katika nchi zao, hata kama ni wakuu ndani ya nchi zao," alisisitiza Obasanjo.

Kauli hiyo ya Obasanjo ilisababisha ukumbi mzima kupiga makofi na kumshangilia, kitendo ambacho kilionyesha jinsi suala la ufisadi linavyoshabikiwa na watu wengi.

Obasanjo, ambaye amewahi kuwa kiongozi wa kijeshi, kabla hajagombea urais kupitia chama cha siasa nchini mwake, alisema mataifa ya Afrika hayawezi kupata maendeleo, bila viongozi wake kukubali kupambana na rushwa.

Alibainisha kuwa, nchi nyingi za Kiafrika zinakabiliwa na tatizo la rushwa miongoni mwa viongozi wake, na kusema kuwa wakati yeye akiwa rais, alidiriki kuwafikisha mahakamani hata mawaziri waliotajwa kuhusika na kashfa za rushwa.

"Inabidi tukubali na tuwe tayari kuwafikisha mahakamani hata mawaziri na wakuu wa polisi kama wamehusika na vitendo vya rushwa, ndipo tutaweza kujipanga na hatua nyingine ya kukuza uchumi wa nchi zetu," alisema Obasanjo.

Akiitolea mfano nchi yake, Obasanjo alisema wakati anaingia madarakani, hali ilikuwa mbaya mno kwa upande wa uchumi, lakini baada ya kuanzisha mapambano dhidi ya mafisadi, nchi ilibadilika na kuanza kuingiza mapato mengi ambayo awali yalikuwa yakipotelea mikononi mwa mafisadi.

"Baada ya kuanzisha vita hii, serikali ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kurudisha mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakipotelea mikononi mwa mafisaidi," alisema.

Alisema baada ya kumaliza kipindi chake cha utawala, alifanikiwa kuiachia nchi yake akiba ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 40, ikiwa ni zaidi ya akiba katika nchi kama Uingereza.

"Wakati naingia madarakani nilikuta hali mbaya sana, kwani kulikuwa na akiba ya dola za Marekani bilioni 16 tu, lakini nimeondoka madarakani na kuacha akiba ya dola bilioni 40, ikiwa ni rekodi ya akiba kuizidi nchi kama Uingereza," alisema Obasanjo.

Akizungumza na gazeti hili katika viwanja vya AICC, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema kuwa maneno hayo ya Obasanjo yanapaswa kupewa kipaumbele na viongozi.

Alisema ingawa suala la ufisadi linazungumzwa sana hivi sasa na viongozi, hakuna matokeo ya maana, kwa sababu vita dhidi ya ufisadi inachukuliwa kisiasa zaidi.

"TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania) inasukumwa tu, si kama Nigeria… kazi bado kubwa hapa Tanzania," alisema Warioba.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu wa Jamaica, P.J. Patterson, alimmwagia sifa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kusema kiongozi huyo ataendelea kukumbukwa kwani alijenga misingi imara, ikiwemo ya kupambana na umaskini kwa watu wote.

"Nawaomba wajumbe wote wa mkutano huu tuutumie kumuenzi (Nyerere) kutokana na mchango wake mkubwa, alijenga misingi imara kila nyanja, alipambana na umaskini bila kujali itikadi," alisema Patterson.

Alisema Afrika inayo nafasi kubwa ya kuondokana na umaskini kutokana na rasilimali nyingi zilizopo, sambamba na kuuza mali nje ya nchi zao.

Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, alisema serikali inaifanyia kazi kauli hiyo ya Obasanjo na kwamba wale wote wanaotuhumiwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, na inapobidi watafikishwa mahakamani.

"Kwa vile suala hili linakwenda sambamba na uchunguzi, wale wote wanaotuhumiwa kwanza tunawapatia nafasi ya kujieleza, ili kupima uzito wa tuhuma zao, lakini baada ya hapo wakibainika na tuhuma watafikishwa mahakamani," alisema Simba.

Alisema hivi sasa uchunguzi unaendelea katika mikataba mbalimbali, ili kubaini ni nani aliyehusika, huku sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano mwaka 2007 ikitoa nafasi ya kuwashughulikia zaidi wale wote wanaotuhumiwa.

Kauli hiyo ya Obasanjo inaweza kuibua joto la mjadala wa ufisadi, ambao umepamba moto nchini, huku viongozi kadhaa, hasa wa Serikali ya Awamu ya Tatu, wakielekezewa tuhuma nyingi za ubadhirifu wa mali za umma.

Hivi majuzi, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi, alithibitisha kukamilisha kulipitia faili lenye tuhuma za ufisadi dhidi ya mmoja wa mawaziri wa serikali hiyo, na kusema limeshapelekwa TAKUKURU kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.

Aidha, kauli hiyo ya Obasanjo, imekuja wakati marais kadhaa wastaafu wa Afrika, akiwamo yeye mwenyewe, wakiwa wanatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka walipokuwa viongozi.

Pamoja naye, orodha ya marais wastaafu wanaokabiliwa na tuhuma hizo ni pamoja na Benjamin Mkapa wa Tanzania, Frederick Chiluba wa Zambia na Bakili Muluzi wa Malawi.
 
Obasanjo: Ufisadi ni tatizo kubwa Afrika

na
Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, alisema serikali inaifanyia kazi kauli hiyo ya Obasanjo na kwamba wale wote wanaotuhumiwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, na inapobidi watafikishwa mahakamani.

“Kwa vile suala hili linakwenda sambamba na uchunguzi, wale wote wanaotuhumiwa kwanza tunawapatia nafasi ya kujieleza, ili kupima uzito wa tuhuma zao, lakini baada ya hapo wakibainika na tuhuma watafikishwa mahakamani,” alisema Simba.

Duh! Huyu mama ni kigeugeu kweli kweli!!! Mwizi anatakiwa akajieleze mahakamani siyo ajieleze huku akiendelea kuwa huru.
 

Aidha, kauli hiyo ya Obasanjo, imekuja wakati marais kadhaa wastaafu wa Afrika, akiwamo yeye mwenyewe, wakiwa wanatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka walipokuwa viongozi.


Ona sasa!!!!!!

Hivi inawezekana katika jamii ya mashetani, kuna ambao wanawakamata na kuhukumu wahalifu wao???%!^&!$%&
 
Obasanjo na mtoto wake watueleze US$ 14 Billion kwa ajili ya umeme wa wananchi wa Nigeria wamezipeleka wapi..........watu wamechoka na umeme wa mgao na matumizi makubwa ya generators!!!!!!
 
Obasanjo:

“Inabidi tukubali na tuwe tayari kuwafikisha mahakamani hata mawaziri na wakuu wa polisi kama wamehusika na vitendo vya rushwa, ndipo tutaweza kujipanga na hatua nyingine ya kukuza uchumi wa nchi zetu,” alisema Obasanjo.

Bado kabisa Tanzania kufikia hatua ya kuwaweka vigogo ndani kwa ufisadi. mheshimiwa naya amekuwa mwoga sana action zinachukuliwa kichinichini, kwakweli Kama Obasanjo anavyosema inabii Watz tubadilike sana.
 
Mtashangaa bure, get the popcorn and Pepsi to enjoy the reality show. Wote hawa wamechukua "kihalali" wakijua kuwa hakuna Sheria itakayowafunga ila ni kulaumiwa kwa uzembe! Wamejifunza kutoka kwa Mwalimu wao Tony B.
 
Obasanjo kama mtu mwingine anakushoto na kulia.

Mtizamo wake na jinsi alivyojipresernt kwnye ss ..alikuwa nafuu sana kuliko viongozi nwengi.

Aliioyesha wazi kuwa Dhana na kujitegemea ni muhimu. JK alishiundwa kabisa hata kutoa dalili zaidi ya kuoba n akushukuru mpka kupitiliza.

Obasanjo... alionyesha umuhimu wa kutokuwapigia magoti WB na IMF.. na kaonyesha walivyofanya Nigeria...Tangu JKN aondoke hakuna mtzanzania mwenye dhubutu..kutoa maoni yake hadahhrani hata kama yanapingana na ya Hao wakuu wa Fedha.

Obasanjo... Alionyesha kuwa Waafika ..They are not There to be told what tod...lakini hata wao wanachakusea....hence..the CONCEPT YA PATNERSHIP.....Yule mzee alito chalenge za kutosaha na safi kabisa...

Obasonjo... alionyesha kuw apamoja na hawa waamerika weusi kuja na misaada...etc...but waafeika wa AFRICA ..pia wameendelea na wanamarafiki wengine..wachina..waasia etc..so sio kuwa bila hawa SS we are goin to die...yuo see ni mtu wmenye character.

Personaly.... ningekuwa na President wangu mefanya hivyo..thern ndipo akaendelea na kuoba..na kushukuru.... ningejona wa dhamani zaidi.

and

Tusisahau kuwa...

Kunatetesi kuwa Obasanjo alifanya urafiki wa karaibusana na mke wa mtoto wake...etc..

Pamoja na hayo..

Obasanjo..ameonyesha ukomavu na typical character.
 
Hivi Obasanjo ni msafi kiasi gani mpaka asimame Altareni na kuzungumza maneno mazito kama hayo?
Kama kweli atakua ni msafi kiasi cha kujiamini kiasi hicho (maana sifahamu vizuri habari zake iwapo zipo zihusianazo na ufisadi) Basi atakua ni mmoja kati ya maelfu ya viongozi wa Afrika wenye mapenzi mema na nchi zao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom