Mkuu Indume Yene kwa kweli inasikitisha sana,Mara ya kwanza nilipoisikia hii habari niliingia woga,Wazungu wengi ni Wabaguzi, hichi kitendo cha Barack Obama kufanikiwa kuwa Rais wengi hawakukipenda.Hivi sasa Vitendo vya kibaguzi vinaonekana wazi na kuripotiwa kila mahali.......Hata maandamano na mikusanyiko mingi inayoendelea hivi sasa kuhusu "Bima ya Matibau/Afya" inaendeshwa kibaguzi zaidi,haingii akilini mtu badala ya kulalamika uchaguzi wa Bima anayotaka au Daktari anayemtaka,anabeba Bango lenye maelezo ya kibaguzi na kuhusisha Utawala wa Obama na Usoshalisti.
Bado Ubaguzi wa Rangi ni tatizo kubwa Marekani,Si rahisi mtu aliye nje ya Nchi hii kuliona...Wanatumia vyema vyombo vya habari kuonyesha kama kwamba Ubaguzi hauna nafasi katika Marekani.Hata Rais Obama hana nafasi kubwa ya kuuelezea Ubaguzi, nafikiri kuuzungumza/Kuujadili Ubaguzi ni jambo linaloogopwa kama TUSI,huu ni Utamaduni wa Wamarekani weupe na Weusi,haya mambo ya Ubaguzi hayajadiliwi mpaka litokee tukio linalohusu hali hiyo.