Obama: Tulikosea kuivamia Libya na kumuondoa Gaddafi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
image.jpeg


Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.

Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.

Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.

Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.

Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.


Chanzo: BBC
 
Kosa kubwa zaidi ni kule kudhani walilokosea Libya ni kutoandaa Mazingira mazuri baada ya kuivamia na Kumuondoa Ghadafi.

Kama Libya ingekuwa inatawalika leo kwao Uvamizi ule ungekuwa halali.
Namkubali sana Donald Trump kwa kuwa Mungu kamuwezesha kutokuwa Mnafiki ana ujasiri wa kueleza hisia zake za kweli
 
barafu
Hawa jamaa sijui Mashetani???
Iraqi walikosea kumuondoa SADAM
Libya walikosea kumuondoa Col: Gaddaffi
Afghanistan walikosea kuwaondoa TALIBAN
Somaliya walikosea kumuonda SIAD BARRE !!!
Mkuu hawa Marekani ni "kirusi" cha Dunia...Wanafanya jambo halafu baadae yakiwatokea puani wanakimbia.Sio muda watakuja kusema si kweli kuwa Osama ndio alilipua Twin Towers za WTC
 
Mkuu hawa Marekani ni "kirusi" cha Dunia...Wanafanya jambo halafu baadae yakiwatokea puani wanakimbia.Sio muda watakuja kusema si kweli kuwa Osama ndio alilipua Twin Towers za WTC
Historiya imethibitisha kuwa kila Rais wa USA ni lazima afanye UKATILI fulani ....!!
ULAYA WWII
JAPAN
KOREA
VIETNAM
MIDOEAST
AFRIKA nk..nk..
 
Nikisoma ile hotuba ya mwisho ya Gaddafi inahuzunisha sana haswa pale aliposema "Leo hii majeshi ya dunia yamenizunguka na kutaka kuniua kisa sikufuata sera zao, mwanangu Obama anataka kuniua.....nilijinyima kwa ajili ya watu wangu na kuwapa nyumba, chakula na afya bure, hawakuridhika na leo hii wanadai haki kutoka America ambako mambo hayo niliyowafanyia hata huko hakuna."
 
Kosa kubwa zaidi ni kule kudhani walilokosea Libya ni kutoandaa Mazingira mazuri baada ya kuivamia na Kumuondoa Ghadafi.

Kama Libya ingekuwa inatawalika leo kwao Uvamizi ule ungekuwa halali.
Namkubali sana Donald Trump kwa kuwa Mungu kamuwezesha kutokuwa Mnafiki ana ujasiri wa kueleza hisia zake za kweli
You are as stupid as your thoughts. what is good about this stupid Trump who only dreams of building walls between him and other people? If not creating barriers, his other main dream is colonizing Africans. To hell with Trump and whoever supports him.
 
Back
Top Bottom