Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Raisi Obama wa USA anayemaliza muda wake, aliyebakiza kama wiki 3 tu madarakani, ameamua kwa kutumia muda wake huu mfupi uliobakia kuiwekea nchi ya Urusi vikwazo vya kiuchumi kwa kosa ambalo yeye Obama anasema nchi ya Urusi ililitenda kumsaidia D.Trump kushinda Uchaguzi wa nchi ya USA!
Sasa kilichonivutia na kunifanya nilete hapa ni ufanano wa Raisi wetu mstaafu Kikwete, ambaye alikuwa anafanya teuzi muda mchache kabla ya kuondoka madarakani, na hapa palijaa maneno ya kashfa na kejeli nyingi dhidi ya Mzee Kikwete na wengi kama ilivyo kawaida yao wakaanza kututukana Waafrika wote kwamba tuna low IQ, hatujui demokrasia ingawaje na wao pia ni Waaafrika na walienda mbali kabisa kusema Waafrika tumelaaniwa, sasa je USA nao wamelaaniwa? Kwa maana Raisi wao anafanya maamuzi kama vile Mzee Kikwete akiwa amebakiza wiki tatu tu?
Au kwa sababu ni USA ni Wazungu, basi mtawatetea na kuwatafutia sababu ili kuhalalisha na kumtofautisha na Mzee Kikwete?