Obama Hebu Njoo Haraka Walalahoi Tupumuweeee!!!

Obama Hebu Njoo Haraka Walalahoi Tupumuweeee!!!

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
77,371
Reaction score
111,682
DSC_0024_728ec.JPG

DSC_0029_319eb.JPG

Picha ya Juu:
Askari wa jeshi la POLISI wakilinda usalama kwa wenzao wa Jeshi la Mgambo wakati wa kampeni ya usafi wa mazingira na kuondoa vibanda vyote vya biashara vilivyopo kandokando ya Barabara.
 
Kwa mtindo huu hadoi anafika tutakuwa tusharudishwa MIKOANI kwetu.....KWa walala hoi kama sisi; mambo ni MGENI NJOO MWENYEJI AKOME!!!!
 
Sijui ndio mambo ya mgeni njoo mwenyeji apone, kuna barabara sasa zimefungwa kwa muda ili walau chepeo na sururu zipite kufanya ukarabati...hii ni Kilwa Rd

ASANTE+OBAMA.jpg
 
Sasa hivi hapa Posta mpya pametakata kama jiwe la kufulia nguo mtoni...
Wale wafanyabiashara ndogo ndogo,wauza magazeti na vocha eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam wamedai kunyanyasika na mgambo wa jiji kupitia msako mkali unaofanyika.

Mathalani kuna jamaa mmoja ni muuzaji maarufu wa CHIPS DUME & Dagaa Mchele hapa karibu na Parking za Posta ilipo Alpha Dry Cleaners, kijiwe chake kilisambaratishwa na miundombinu yake kusombwa na Mgambo.

Kaka mkubwa Mentor sijui kama umepona hapo kijiweni kwako

E84A0334.JPG
 
Last edited by a moderator:

we watu8 kumbe uko hapo jengo la NSSF looh ndo nini umenipiga picha nikiwa navuka barabara na sketi yangu ya purple na miwani yangu. Ndo nilikuwa natoka kuangalia dagaa na mihogo kwa yule babu kumbe wamemmuvusisha sasa leo imebidi ninywe chai tuu lunch hii. Na yule wa mahindi pia hola daah wamemtoa ntapata wapi tena mahindi ya kuchoma yenye pilipili hapa mjini?
 
Last edited by a moderator:
Ndo hapo watu kama kina sakapal wanafurahia kuja kwake wengine tukipata shida!!!

Mentali usiwe na wasi ntafanya mpango kwa kuwa nshapata vibali vya kukutana na Obama ntafanya mpango kibanda chako kitarejeshwa ila vingine vyote vitatoka, sanasana kikirudishwa tutakipaka rangi ya ofisi ninayofanyia kazi ili kisionekane shida kwa mkuu wa nchi looh.
Ila akiondoka mavumbi ya Obama mtayapata so uvumilivu tuu kila mmoja.
 
Hahaha kumbe wewe ndio huo mdada....loh!
Yule jamaa wa mahindi bado yupo best...si unajua huwa anajibanza hapa karibu na Embassy Hotel...

we watu8 kumbe uko hapo jengo la NSSF looh ndo nini umenipiga picha nikiwa navuka barabara na sketi yangu ya purple na miwani yangu. Ndo nilikuwa natoka kuangalia dagaa na mihogo kwa yule babu kumbe wamemmuvusisha sasa leo imebidi ninywe chai tuu lunch hii. Na yule wa mahindi pia hola daah wamemtoa ntapata wapi tena mahindi ya kuchoma yenye pilipili hapa mjini?
 
tukiamua usafi tunaweza lakini si mpaka aje mgeni

Ile pita shoto ya pale Mlimani City (Total Gas Station) na hapa Mwenge Mpakani zimepigwa rangi ya njano na nyeusi...

Halafu hapa Ubungo Mataa, pembezoni mwa barabara kwenye vile vinguzo vya kutenga barabara kuu na ile ya waenda kwa miguu navyo vimerembwa kwa rangi nyeusi na njano...
 
  • Thanks
Reactions: awp
Hahaha kumbe wewe ndio huo mdada....loh!
Yule jamaa wa mahindi bado yupo best...si unajua huwa anajibanza hapa karibu na Embassy Hotel...

wacha nikachukue mawili ya kula kwenye foleni hadi nifike mwenge yatakuwa yameisha, ila mie huwa nachukulia kwa yule aliye nje ya alpha dry cleaners karibu na exim bank, embassy mbali na parking yangu
 
Raisi wa dunia yle lazma mazingira yawekwe vizuri.
 
Nenda kabla hajafurumushwa tena loh...maana mgambo wana hasira hao....

Btw...tutafutane best best maana naona wote tunacheza mitaa ile ile

Back
Top Bottom