Obama apinga (kura ya Veto) Saudi Arabia kushitakiwa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Raisi wa USA Barack Obama amepiga veto kupinga nchi ya Saudi Arabia kushitakiwa na Congress ya USA!
Congress ya USA ilikuwa inataka kuishitaki nchi ya Saudi Arabia kwa ushiriki wake wa Septemba 11, ambapo Majengo ya World Trade Center yalishambuliwa na kuangusha na magaidi wa Kiarabu au niseme Magaidi waliotokea tu kuwa na asili ya Uarabu, ambapo watu wengi walipoteza maisha na wengine kulemazwa!

Hali hiyo ya Obama kuveto Sheria ambayo ingewezesha Saudi Arabia kushitakiwa imeshangaza wengi, na Seneta mmoja wa USA ajulikanye kama Chuck Schumer (Democrat) amenukuliwa akisema kwamba kama nchi ya Saudi Arabia haikuhusika na Septemba 11 hakuna haja ya Raisi Obama na Ufalme wa Saudia kuhofia Sheria hiyo na kama walihusika basi ni lazima hatua dhidi yao zichukuliwe!

Huo ndiyo unafiki wa Wanasiasa, wanajifanya (Obama) kutoa machozi mbele ya Kamera, kumbe huku wao wenyewe wanazuia wahusika kushughulikiwa!

Obama's veto of 9/11 bill aimed at Saudi Arabia sets up standoff with Congress

obama-saudis.jpg



barack-obama-fuerchtet-einen.jpg


Raisi wa USA Obama akijifanya kutoa chozi la kinafiki huku akiveto wahusika kushitakiwa!
barack-obama-0-800.jpg
 
wamarekani wamefulia wanatafuta njia za kupata pesa tu
wangeleta mashitaka feki mwishowe wangedai fidia ya mabilioni ya dola
Libya eti wanadaiwa hela ya kumng'oa Gadaffi,wanatoa mafuta bure mpaka 2050
 
wamarekani wamefulia wanatafuta njia za kupata pesa tu
wangeleta mashitaka feki mwishowe wangedai fidia ya mabilioni ya dola
Libya eti wanadaiwa hela ya kumng'oa Gadaffi,wanatoa mafuta bure mpaka 2050
Wewe na marekani nani kafulia???? Ukute hata "HARRIER" huna ila unajikuta kuikandia marekani eti imefulia.
 
Back
Top Bottom