Obama aipongeza tanzania....

Obama aipongeza tanzania....

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,850
[h=2][/h]

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa pongezi na sifa kwa Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi chache duniani ambazo zimetia saini mkataba wa Ushirikiano wa Serikali Zinazoendeshwa kwa Uwazi ambao unalenga kujenga na kuendeleza nafasi ya taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa Serikali.
Rais Obama ametoa pongezi hizo kwa Tanzania leo, Jumatatu, Septemba 23, 2013, wakati akizungumza katika mkutano maalum aliouandaa mwenyewe Rais Obama kuzungumzia nafasi za Serikali katika kuunga mkono na kuendeleza asasi na taasisi zisizokuwa za Kiserikali na kuzishirikisha zaidi katika kuboresha shughuli za utawala bora uliofanyika kwenye Hoteli ya Hilton, mjini New York, Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wachache duniani walioalikwa kushiriki mkutano huo maalum ambao pia ulishirikisha wawakilishi wa asasi zisizokuwa za Kiserikali 300.
Baadhi ya nchi nyingine za Afrika zilizoalikwa na kushiriki katika mkutano huo ni pamoja na Liberia, Ghana, Benin, Libya, Tunisia, Senegal, Afrika Kusini na Botswana.
Shabaha kuu ya mkutano huo wa saa moja ilikuwa ni kutafuta namna ya kuongeza kiwango cha kuungwa mkono kwa taasisi na asasi hizo na jinsi gani ya kuzilinda ili kuziwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha, mkutano huo ulilenga kuzitaka Serikali ambazo zinaweka vikwazo kwenye utendaji wa asasi hizo kuondoa vikwazo hivyo haraka ambavyo vinahujumu utendaji kazi na mchango wa asasi hizo katika uendeshaji wa utawala bora.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Rais Obama amezisifia nchi kama Tanzania ambazo zimetia saini makubaliano ya Ushirikiano wa Serikali Wazi ambayo yanalenga kupandisha nafasi ya asasi zisizokuwa za Kiserikali katika Utawala Bora,Uwazi na Uwajibikaji katika Serikali.
Amesema kuwa binafsi alikuwa ameamua kukutana na viongozi wa asasi zisizokuwa za kimataifa wakati wa ziara yake ya karibu katika Afrika ambako miongoni mwa nchi nyingine alitembelea Tanzania.
Rais Obama alifurahi sana kukutana na Rais Kikwete. Rais Obama alimkumbatia Rais Kikwete akimwelezea kama “kaka wa karibu na rafiki mzuri” kauli na kitendo ambacho kiliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye ukumbi.
 
Jk anasemwa kwa mambo mengi mazuri na mabaya lakini jk anamzuri mengi sana na mabaya ni mchache san kama binadamu hawezi kukosa kabisa lakini ukweli hujitenga na uongo haya yako wazi kila kukicha.
 
Uwazi gani anao usema Obama? Labda uwazi wa kugawa raslimali za Asili za Tanzania kwa makampuni ya Canda na Marekani, Hajui kwamba watoto wetu wanafesli na maksi zinaongezwa? Hajui kwamba watu wanatekwa na kumwagiwa Tindikali na upelelezi hadileo hawajakamatwa hata wa kusingiziwa? Hajui kwamba Katiba imechakachuliwa kwa jamaa kuingiza vifungu bila kuwashirikisha wadau?

Nyerere aliwahi kusema yafuatayo:- "Ukimwona kiongozi Mwafrika anasifiwa sana na wazungu mambo matatu yanatokea,
1. Amani ya nchi yenu inakuwa mashakani,
2. Usalama wenu uko njia panda
3. RASLIMALI ZENI ZINAKWENDA MCHANA KWEUPE KWA ANAYEMSIFU BILA KIZUIZI CHOCHOTE"

Mchungaji Mtikila aliwahi kusema "Shida ya Watanzania ni kuwa na Upendo wa mshumaa, ambao unateketea wenyewe kwa kuwawashia wengine nuru" Tutaendelea kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa, Obama Obama, Xi Jiping na kila yeyote lakini hali ya umaskini ndo hasa imefikia kileleni, Maisha sasa ni magumu zaidi kuliko miaka mitatu na zaidi ilyopita,

Angalieni tusiwe akina Kalagabaho
 
hizi asasi nyingi zinatumiwaga kufanya intelligence issues ndio mana rais putin akazistukia amewafukuza kule urusi!!!! alafu mbona ktk nchi izo ziko za kiafrika tu inamaana ni huku afrika tu ndio tunatakiwa kufundishwa umuhimu wa izo taasisi!!!
 
Umesema kweli kabisa, mbona wao hawana NGOs katika nchi zao? Wazungu (Obama ni mzungu, kinyume cha wanavyofikiria wengi) kila siku wanabuni mbinu mpya za kuendeleza ukoloni. Wameona serikali nyingi duniani zinazidi kuwa za Kidemokrasia na hivyo kutokuwepo sababu za kuzishinikiza, ndio wanataka kutawala kupitia vinyang'arika hivi wanavyoviunda. Sisemi kuwa kusiwe na NGOs za kigeni katika nchi zetu, nisemavyo ni kuwa zote zilazimishwe kufuata sheria ya nchi na kuwe na utaratibu wa kujua namna gani wanatumia fedha zao. Serikali i za Afrika zisikimbilie kutia saini tu kila kitu, upuuzi, ndiyo maana twaendelea kutawaliwa.
Sina matatizo na NGO za nchini ila pia zijulikane nani anazifund na kwa nini. NGOs ndio hatari kubwa inayozibali serikali za Afrika katika uongozi wa nchi zao. Leo hii, serikali za Afrika hazina nguvu ya kugusa NGO ya kigeni.
 
uwazi gani anao usema obama? Labda uwazi wa kugawa raslimali za asili za tanzania kwa makampuni ya canda na marekani, hajui kwamba watoto wetu wanafesli na maksi zinaongezwa? Hajui kwamba watu wanatekwa na kumwagiwa tindikali na upelelezi hadileo hawajakamatwa hata wa kusingiziwa? Hajui kwamba katiba imechakachuliwa kwa jamaa kuingiza vifungu bila kuwashirikisha wadau?

Nyerere aliwahi kusema yafuatayo:- "ukimwona kiongozi mwafrika anasifiwa sana na wazungu mambo matatu yanatokea,
1. Amani ya nchi yenu inakuwa mashakani,
2. Usalama wenu uko njia panda
3. Raslimali zeni zinakwenda mchana kweupe kwa anayemsifu bila kizuizi chochote"

mchungaji mtikila aliwahi kusema "shida ya watanzania ni kuwa na upendo wa mshumaa, ambao unateketea wenyewe kwa kuwawashia wengine nuru" tutaendelea kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa, obama obama, xi jiping na kila yeyote lakini hali ya umaskini ndo hasa imefikia kileleni, maisha sasa ni magumu zaidi kuliko miaka mitatu na zaidi ilyopita,

angalieni tusiwe akina kalagabaho

unaona ee,obama lazima amsifie kikwete ili apate pa kuuza umeme kwa bei anayoitaka.chezea symbion wewe.kama tanesco ina uwezo wa kumlipa nimrod mkono bill 18 KWA USHAURI NA UTETEZI TU,kwa nini ishindwe kuilipa symbion ya us?, na kwa nini mkoloni asimsifie kikwete ili mambo yake yanyooke?
 
Chunguza NGO zinazofanya kazi Urusi! Ni chache sana. Nyingi zipo Africa.Tafakari!
 
Uwazi gani anao usema Obama? Labda uwazi wa kugawa raslimali za Asili za Tanzania kwa makampuni ya Canda na Marekani, Hajui kwamba watoto wetu wanafesli na maksi zinaongezwa? Hajui kwamba watu wanatekwa na kumwagiwa Tindikali na upelelezi hadileo hawajakamatwa hata wa kusingiziwa? Hajui kwamba Katiba imechakachuliwa kwa jamaa kuingiza vifungu bila kuwashirikisha wadau?

Nyerere aliwahi kusema yafuatayo:- "Ukimwona kiongozi Mwafrika anasifiwa sana na wazungu mambo matatu yanatokea,
1. Amani ya nchi yenu inakuwa mashakani,
2. Usalama wenu uko njia panda
3. RASLIMALI ZENI ZINAKWENDA MCHANA KWEUPE KWA ANAYEMSIFU BILA KIZUIZI CHOCHOTE"

Mchungaji Mtikila aliwahi kusema "Shida ya Watanzania ni kuwa na Upendo wa mshumaa, ambao unateketea wenyewe kwa kuwawashia wengine nuru" Tutaendelea kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa, Obama Obama, Xi Jiping na kila yeyote lakini hali ya umaskini ndo hasa imefikia kileleni, Maisha sasa ni magumu zaidi kuliko miaka mitatu na zaidi ilyopita,

Angalieni tusiwe akina Kalagabaho

Hivi kuna watu wengine ni wa ajabu sana humu JF , inchi za nje na taasisi zao zikisema Tanzania hamna haki wala democrasia mikono juu! hao hao wakisema serikali ya Tz imejitahidi kufanya A,B,c ohh, wanataka mali zetu , wanamsifia kikwete kwa sababu kawapa kigamboni mbona mnashindwa kutoa uhuru hata kwa fikra zenu?.

Ukitaka kubaki upande wa mistakes za serikali tu kwa kweli hutozikosa the same applies to you as an individual kama leo hii members wengine wakaamua kukuchunguza tuu jinsi unavyochangia hoja na wakataka kuangalia mistakes tu hutosalimika hata kindogo,lakini wakiangalia upande wa pili yani postive side of it watagundua kwamba kumbe kuna wakati huwa unatoa hoja nzuri na zenye kujenga.

Kosa la obama lipo wapi kumsifia kikwete ? angemsifia Dr slaa kwamba ni mtaalalmu wa maboma mngesemaje ? tupunguze unafiki japo kwa maslahi ya Taifa.
 
Back
Top Bottom