Josephat Sanga
Senior Member
- Aug 29, 2016
- 151
- 98
Kwa tarifa za awali zilizolipotiwa mpaka sasa watu watano wamepoteza uhai na wengine sita wamepelekwa hospitali ya wilaya Nzega, hali zao zikiwa mbaya na zoezi la uokoaji bado linaendelea.
Tarifa zaidi kujua idadi kamili ya watu waliokufa na majeruhi tutaendelea wajuza zaidi.
======
UPDATE:
Watu watano wamefariki dunia na sita kujeruhiwa vibaya baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika shimo la mgodi wa zamani wa Resolute, Nzega mkoani Tabora.
Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla alisema tukio hilo limetokea jana saa 7:00 baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na Serikali.
Alisema eneo hilo limezuiwa kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba.Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda, mkazi wa shinyanga, Mohamed Mohamed mkazi wa Singida , Manona Nyombi mkazi wa Bariadi na Modesta Leonard mkazi wa Nzega.
Waliojeruhiwa ni Kangwa Mayenga mkazi wa Bariadi, Agness Antony mkazi wa Chato, Deus Alphonce mkazi wa Igunga na aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda mkazi wa Chato.