Pole sana mpendwa kwa lililokusibu wengi hukutwa na hali kama yako pindi wanaposuka mtindo huo wa kimasai,ila kwasababu umesema hutaki kunyoa japo kuna mitindo mbalimbali ya kunyoa ambayo ungependeza sana ,na hata kama ukinyoa basi unaweza kuvaa wigi kama ulivyopendekeza mwenyewe,kama hutaki kufunga lemba, sijajua upo mkoa gani lakini unapoishi unaweza kupata weaving la gharama utakayomudu endapo utapita kwenye maduka ya urembo/vipodozi.
Na pia unaweza kutumia vitu vya asili kama parachichi,,samli kama steaming pia.
Kingine kuna shampoo nyingi ambazo zinatumika kwenye saloon zipo chini ya viwango na huchangia pia kuharibika kwa nywele hivyo uwe makini na hilo.
Uzuri unao ila tayari umeshajitia kasoro mwenyewe kuwa una kichogo,kichogo si kasoro bali ni jinsi Mungu alivyokuumba