Poise
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 7,633
- 7,907
Napenda kuwatakieni uhitimisho wa wiki mzuri, kwa wengi wanaita mapumziko ya wiki [furai dai] haa haaaa.
Ila turudi sasa katika mada yenyewe, mada yenyewe ni kuhusu nywele za bandia kama wingi na kuweka dawa za kurefusha nywele.Nimepitia maeneo mengi hapa barani Afrika hali niliyogundua ni kuwa asilimia 95% ya watu wanaweka nywele bandia.
Hapa Afrika hasa kusini mwa jangwa la sahara na Tanzania ikiwemo, kwa mfano tu nchi zilizokuwa chini ya utawala wa kikoloni wa mfaransa ndiyo janga chini ya jua maana ni wote wanaume kurefusha, kuzipaka rangi nywele na wanawake kuvaa nywele bandia pia kuzirefusha!
Sijaweka picha maana, kila upande utakapogeuzia macho yako utajionea mwenywe mathalani uko katika mkusanyiko wa watu wa rika tofauti pasipo kujali jinsi/jinsia zao.
Je, ndiyo kudharau uafrika na asili yetu na kuupenda sana uzungu, uchina, ujapani na ubrazilia;kama majina ya nywele hizo zinavyojulikana tofauti tofauti kulingana na muonekano wake?
Je, ni mvuto tu au ni kutojiamini kwa watu wetu wa Afrika au kuna jambo la ziada?
Asanteni, naomba kuwasilisha.